Nimechanganyikwa naomba mawazo yenu wanajf wenzangu.

unaweza still kwenda chuo kikuu...kwa matokeo hayo hayo

hebu nenda ofisi za admissions za vyuo watakueleza how..

kama una uwezo wa kujilipia,basi nenda chuo kikuu moja kwa moja...

vyuo vipo vingi vyenye sifa

anza na udsm,nenda tumaini
halafu nenda IIT......
KUMBUKA CHUO KIKUU SIO LAZIMA KUANZA NA DEGREE...
UNAWEZA ANZIA NA KOZI NYINGINE HALAFU NDIO UKASOMA DEGREE UNAYOTAKA

ASANTE kwa ushauri wako,
kuanzia jumatatu itabidi nifanye kazi ya kuzunguka vyuoni na kuonana na watu wa administration ili nifahamishwe zaidi nitakiwacho kufanya.
Hata kwa ngazi ya cheti nipo tayari kuanza ili mradi nipate ujuzi mwingine.
SAMAHANI KWA LATE REPLY.
 
nawaunga mkono wote waliotoa maoni yao,
wasiwasi wangu ni kwa SAWEBOY anaficha nn wkt hili jukwaa letu ni la uwazi na ukweli.
Awe mwazi ili wengine nao wafaidike.Mnunu usikate tamaa bado una nafasi nzuri ya kusoma
nakupa mfano wa Hosea wa PCCB alikuwa karani wa mahakama
then akajiendeleza akawa hakimu ngazi ya mwanzo ,
hakimu mkazi na usisahau ni dr kabisa.songa mbele.
Nakupongeza kwa ujasiri wako wa kuweka wazi malengo yako yatatimia
na ukweli wako umekuweka huru.

ASANTE KWA KUNIPA MOYO ZAID,
Nimeumia sana ,PIA KUFELI KUNAUMIZA MNO,
Wakati mwingine nahisi kama naota,
Lakin sina budi kujipangusa na kuendelea na safari ya kutafuta elimu,
huku nikiamini kuwa ipo siku ntatimiza ndoto zangu.
Mawazo yenu ni fimbo yangu ya kunyanyukia, ASANTE SANA.
 
mkuu we waza kuresiti mitihan usiogope na mungu akukunyima upande wa pili mashallah komaa na shule muulize shyrose banji akwambie umuhimu wa kurisiti mtihan..

NASHUKURU SANA Pdidy,
kwa kunipa mawazo ya kuniinua tena imani yangu juu ya elimu,
na safari ya kuelimika mtu kama miye ninayehitaji sana kutoa,
tongotongo la ujinga akilini mwangu,pamoja na kuwa na ufahamu
mpana juu ya elimu.
Shukurani sana ,nimekuelewa vizuri.
 
Nnunu am so impressed; unajitegemea, ni mtegemewa, ni mama, alafu bado ni mwanamke mwenye nia na focus iliyolenga katika elimu - kweli si kazi ndogo .... HONGERA SANA. Wana Jf wametoa mawazo na ushauri mwingi ambao naamini ukiufanyia kazi (na naamini utaufanyia) utafanikiwa tu! Goodluck katika mipango yako yote...

Asante sana Asha D,
nashukuru umetambua juhudi zangu japo hazijazaa matunda mazuri,
lakin sina budi kujifunga mkanda na kuendelea.
Watu wengine wanafika kwenye vilele vya mafanikio pasipo vikwazo vingi sana,
lakin mtu kama mimi naona nahitaji kujituma na kuongeza mapambano zaidi,
ili nami siku moja nilie kivulini.
Shukurani nyingi kwa mchango wako,
samahani kwa late reply jana ilinisumbua ku log in.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom