labda nikuambie tu...32yrs bado unalipa saaanaa tu!
samahani dada lakini nashindwa kuelewa iweje wapenzi wanakorofishana kiasi cha kuachana. hapana naomba kuwa na hekima tofauti kidogo. nendeni kwa councellors mtapata mwongozo.
I second you on that Nyamayao,plus mdada ana kazi yake nzuri na ndio baba wa familia,achilia mbali the abuses-physically,mentally and emotionally....ah ah jamani, thats too much. There is a limit to what a woman can take in the name of marriage.
Pole sana dada yangu, sina uhakika kama nakushauri vema, lakini unaweza kujaribu yafuatayo....!Sijui nianzie wapi?? naandika kwa masikitiko makubwa, miaka 7 iliyopita niliolewa na mwenzangu ambaye nilimpenda baada ya urafiki wa miaka kama 5 japo baadhi ya ndugu zangu hawakupenda niolewe nae coz hana kazi na wala hakusoma aliishia std7 na mimi ni graduate, hakuwa mtu wa kujishughulisha na biashara wala kuajiriwa bali mishen town tu, ila mimi nilimsaidia kamtaji sababu nilimpenda sikusikia wala kuona.
Mwenzangu huyu kiukweli kuna watu walikuwa wanasema hajatulia ila binafsi kwa upofu wa mapenzi sikulijali hili, lakini tatizo la shughuli kutokuwa na shughuli maalumu nililiona lakini mwenzangu alisisitiza kuwa hawezi kusoma labda biashara japo hakuonyesha juhudi niliamini angebadilika maisha yakaendelea. mie ni muajiriwa nakipato cha kuweza kuitimizia familia hata peke yangu. Niliingia kwenye ndoa nikiamini akiwa mume na baba angebadilika
Tumeingia kwenye ndoa ndio naanza kuona matatizo mengi hap tuna watoto wawili, si muaminifu kwa pesa za watu wala zangu akiazima basi inabidi nilipe kufunika aibu, ni muongo mara nyingi ni uongo usio na sababu sijui ninini?? yote tisa kumi kesi za wanawake ni kibao na ameshaattempt kuoa mara mbili yeye nikazikamata kwenye mtandao, anakaogonjwa na wanawake wazuri na weupe (hata mimi ni mweupe na mzuri lol) so kila nikimkamata ni ugomvi tu na mwisho anaomba mara msamaha lakini anarudia tena. Biashara nilimuanzishia japo biashara yenyewe alikuja kushindwa akafanya eneo la biashara ndio kituo cha kukutana na wanawake wake mpaka nikawa naogopa kupita hiyo mitaa.
Mbali na yote haya jamaa ni abuser, physically, verbally, and emotionally,, huwa napigwa mie nikijaribu kuargue kuhusu tabia yake au mambo ya ndani, pia ananihisi hisi na anapenda kunicontrol kama mtoto. kuna events nyingi sana nikiandika nitawachosha
Sasa wandugu imefikia kipindi mimi mapenzi yameisha na tunawatoto 2, tumejenga (90% ni mchango wangu), gari (90% mchango wangu) na kulisha familia 90% ni mimi, mapenzi yameisha kabisa sio mchezo sidhani kama yatarudi na ninataka kuachana naye, ndoa tulifunga kanisani, nimejaribu kumwambia nataka tutengane kwa muda analia anaomba nafasi ya mwisho anadia ananipenda na anawapenda watoto wake hawezi kuishi mbali nao ila mimi nahisi anaogopa ukali wa maisha na sio mapenzi kwangu, japo wanae kweli anawapenda sana. Natamani nisiondoke lakini ninavyomjua huwa anaomba msamaha zikipita wiki mbili mwezi vituko vinarudi pale pale so naogopa na umri unakimbia natakiwa niwe na misimamo mapema kwani naona hata kwa malezi ya watoto si vizuri kuwa na baba mwenye sifa ya uongo na utapeli mtaani au watu wanakuja hapo kudai watoto wataadapt hizo tabia. naomba nikiri udhaifu wangu katika kupenda naomba msinirushie sana mawe kwa hilo kwa nimeshajua wapi niliteleza.
Naombeni ushauri utakaonisaidia mimi na watoto wangu, based on your experiences maana naogopa hata kuwaambia ndugu zangu kwani watanichua haraka, wameshajitolea hadi nyumba ya mimi kuishi na wanangu, na vikao vimeshakaliwa vingi na kila siku wananiambia niachane nae lakini mimi nilikuwa kichwa hakijakaa vizuri bado, yani siamini kama nitaishi hivi maisha yangu bila mume coz sipendi wala sifurahishwi na maisha ya kuwa single parent at my age of 32, na hili ndio linanifanya nifikirie sana kuhusu maamuzi yangu.
Dah! Kesi ngumu.....
Bronty, Ah no Muda wa kuwavumilia hawa watu umekwishaPole sana ndeonasi, hayo ni maisha yatapita tu, madam ni mumeo na mmefunga ndoa kanisani hukulazimishwa na mtu huna budi kuvumilia, usione wamama wamekaa kwenye ndoa zao ukaona wanafanya kazi ndogo, wanapitia mapito makubwa zaidi ya hayo,usichoke kumkumbusha mlipotoka nina imani bado mapema anaweza badilika,kama ukiona huwezi kabisa nenda kwa mchungaji aliyewafungisha ndoa mweleze akupe ushauri
Mh! Na ule ugonjwa wetu wa kisasa umeutafakari hapa!me sikushauri uachane naye since mna watoto na wanamhitaji baba yao. bali unahitaji umwonyeshe kwamba u can survive bila yeye. yaani anza kumfungia pazia. ignore kila anachofanya, ishi hapo ndani kama vile yeye hayupo but at the same time mpe respect. usihoji kuingia wala kutoka kwake. piga pamba kali, kula vizuri always tabasamu. akileta biashara za kujaribu kukupiga mpeleke kwenye vyombo vya dola.
halafu huwa simuelewi mwanamke ambaye anajimudu kwa kila kitu...kuvumilia upuuzi,tutakanyagwa mpaka lini jamani..umefika wakati tuwakanyage!Bronty, Ah no Muda wa kuwavumilia hawa watu umekwisha
Its the end of mfumo dume!
Yes 100% No coment!pole mdada...
break up inakuhusu...
bora single parent, kuliko kumvumilia m2 ambaye mwisho wa siku atakuletea maradhi...
kuna vya kuvumilia, sio hili la uzinzi...mtauana kwa magonjwa muache watoto wanateseka, mpige chini fasta uendelee na maisha yako...
Acha kufikiria watoto wewe ndio mwenye watoto katika hali kama hiyo,Asanteni kwa michango yenu, tatizo kubwa mapenzi yameisha kabisa na ikumbukwe mapenzi ndio pekee yaliyotuunganisha, mimi simfuatilii tena na hata yeye anajua mapenzi yameisha,, na nataka kuondoka kweli ndani kabisa ya moyo wangu natamani kuondoka ila nikiwaangalia watoto roho inasita! sio yeye ninayemuhurumia bali ni watoto yani simtamani hata kumuona natamani aondoke asafiri aende mbali huko.
halafu huwa simuelewi mwanamke ambaye anajimudu kwa kila kitu...kuvumilia upuuzi,tutakanyagwa mpaka lini jamani..umefika wakati tuwakanyage!