nimechanganyikiwa ..naombeni ushauri wa ukweli wana JF

au ndoa zipigwe marufuku?

Hii haitasaidia kitu kwani ukizipiga marufuku zitahamia "underground" na hali itakuwa mbaya zaidi kwani hazitakuwa na mwongozo wowote wa kimaadili. Yaani itakuwa ni sawa na kuvuta bangi au kunywa gongo a.k.a. chang'aa a.k.a konyagi mwitu.
 
Kitendo cha Mungu kuumba mtu mke na mtu mume hapo inabidi usidoubt ndoa...ndivyo inatupasa tuishi otherwise ingeumbwa jinsia moja tu!
 
Jamani naombeni kuwaulizeni wanaume hivi huwa mnaoa ili nini?
Labda -upate mtu wa kusex nae siku yoyote ukitaka?
-au upate watoto?
-au kuridhisha tu jamii na wewe ulioa au
- Ulipata mwanamkeakakulazimisha umuo
- ama ni nini?
maana kiukwelipersonaly kila mtu ananipigia kelele niolewe lakini kiukweli sijui maana ya ndoa,wala nikiwauliza watu maana yake hawanipi majibu ya kuniridhisha…hata nikisemanijifunze kwa vitendo kwa kuangalia ndoa zenyewe ndo nabaki hoi kabisa…

Yes… siwezi kusema maisha yangu yapo full satisfied …naitajihappiness but sijui kama ndoa ndo itakuwa jibu au solution ya kunipa furahamaishani.....
Ngojeni niwape mifano..but msinielewe vibaya..one daynilikuwa natafuta nyumba ..nikapata nyumba moja huyo kijana alikuwa anatakakuhama ..akanitongoza lakini wiki mbili mbele ndo alikuwa anafunga ndoa ..kwelinilishangaa sana hadi sasa ananitakajust imagine ndoa changaaa eti anadai hakuniona mapema mimi wala sina uzuriwowote basi tu uzinzi wake ..nashindwa kuelewa ningekuwa na roho ya zinaanimkubali hii ndoa ingekuwaje?

Kuna Yule jirani niliwaambia nae ndoa yake changaa…wanaitana honey honey mwanamke akigeuka tu anakukonyeza nahisi hata anammendeabeki 3 wangu….hadi nahama nyumba mwezi huu maana ni usumbufu mtupu…

Nikiangalia na mashost zangu wenye ndoa ni vilio vitupu
Hebu cheki hapa hi isms ni ya shoga yangu kanitumia jmos inimebaini kuwa mume wangu anatembea na msichana wakazi.Nimeligundua hilo kwa kuwa mume wangu hatulii room wakati wa ucku,nimeamuakumbana binti akanieleza ukweli ictoshe kwa sasa mi mjamzito nifanyeje best..kiukwelinilimshauri tu abaki na mumewe na amtimue beki 3 but daaah …ni story ndefu
Hebu niambieni tu maana ya ndoawapendwa …au ndoa zilikuwa zamani?
Maana kwa sasa kila mtu anaweza kutoka na yoyote mahali popote navoona…yaanimaisha ni mambo ya kambi popote sijui... naombeni majibu....
dada pole sana kwa kusikia BAD NEWS tU kuhusu suala la NDOA. Mimi ninachokushauri ni kumuomba Mungu kw aimani yako akujaalie mwenza wako mtakayeelewana na kudumu kwa furaha, upendo na uaminifu katika ndoa yenu. Pia ukae ukijua kuwa SIO NDOA ZOTE zinakuwa na matatizo na maloloso kila kukicha, kwani kuna baadhi ya ndoa ni PEPO NDOGO ya hapa duniani. Sasa basi, hili suala lote muachie MWENYEZI MUNGU ndiye mpangaji wa kila kitu. Si umeshawahi kusikia kuwa ooh, kabila fulani hawafai wahuni sa,a, au wachawi na ishu km hizo? ila kiukweli utakuta kwamba SIO WOTE kisa ni kabila hilo wana ishu hizo.....kuwa na amani ndugu yangu, mitihani katika maisha ipo sio katika ndoa tu hata nduguzo wa kuzaliwa mwawea kuwa mwatibuana na maisha yanaendelea salama tu. MUOMBE MUNGU KWA IMANI YAKO AKUJAALIE ATAKAYEKUFAA.
 
Ndoa nyingi ni kwa ajili ya kuanzisha familia
Kupata new purpose in life
Kupata companion (mwenza, mtunza siri, mtu atakayekuuguza au kukuhudumia wakati una shida)
Na pia mapenzi. (ingawa hii ndio imechakachuliwa sana)
KWANI SIS bila ndoa huwezi kuwa na familia?
kampany au mapenzi?
 
Dah! Smile mdogo wangu wa moyoni, kwanza hongera kwa kuamua kujua ukweli manake huo ni ujasiri sana. ILa pia nasikitishwa sana na haya maisha kwani yanapomfunza mtu basi mifano inayotumika ni migumu na hata kanuni pia hazi apply kabisa mwishowe unakuja gundua kuwa mwanafunzi hajaelewa na mfano bado ni complicated kwa muhusika.

Sababu kubwa zinazomfanya mtu aolewe ni kwamba ili kupata mwenza wa kushirikiana naye katika maisha. nisemapo mwenza wa kushirikiana naye simaanish kitu kingine bali mwenza wa kukidhi haja yako ya kimwili(tendo la ndoa), na zaid yako upate mtu wa kushare naye yaani msiri wako. Mambo mengine kuzaa, kufanya kazi za ndani siyo ishu sana katika hili.

Matatizo meng yanayojitokeza katika ndoa za siku hizi ni kwasababu tu ya mambo yafuatayo, mmomonyoko wa maadili kwa ujumla ila nikitaka kuyaweka mepesi sana nitasema tamaa zisizo na mpango. Binadamu tumekuwa hatuna tena hofu ya Mungu, hakuna menye kuheshimu utu wake na mwili wake. Kwangu mimi hili ni jambo baya sana.

Mfano ukimuona baba bdani ya nyumba antembea na beki 3 jua basi anawez kutembea na mwanae wa kumzaa. Kwanini nasema hivi? Binti wa kazi za ndani ni kama mtoto wako manake unabeba full responsibility juu yake kama mzazi. sasa inapotokea ukamtamani skutofautish kama na kumtamani mwanao wa kumzaa au mtoto wa mkeo. Ni taba mbaya na ya kishenzi.

Nirudi kwako mwenyewe Smile, wewe ni kwamba umefundishwa haya maisha kwa kutumia mifano migumu sana au la niseme maisha yalikufunza kabla hujafikia umri wa kupata shule. hapa naona hujanielewa.
namaanisha mfano mtoto wa miaka 5, labda mzazi analazimisha asome darasa la 1 wakati mtoto huyu ni bado yuko mdogo kiakili na hata kiuwezo wa kupambanua mambo kiasi kwamba akiwa darasani alishazoea kuandka sentensi 2 tu huko nursery hapa lakwanza anatakiwa aandike 10 ni wazi kuwa atashindwa na atakomea kwenye hizi 2 tu. na ukimlazimisha mwisho wa siku utakuja kuua kabisa nia yake ya kupenda kusoma na matokeo nikama haya mtoto kuacha shule au kukata tamaa na shule kabisa.

kwa mfano huo basi mimi nikwambie tu njia iliyotumika kwako ndio haikuwa nzuri katika kukufundisha juu ya maisha. Kuna wenye bahati mbaya ambao mwanzo mwisho wanakutana na mitihani baut hawa ni wachache na hivyo lazima wasikike sana manake wanakuwa wanahangaika katika kutafuta suluhisho la maisha yao. wale wanaopata raha ni wengi pia na hawa hawawez kusema hadharan kwan mgema akisifiwa tembo hutia maji.

Ndoa inauzuri wake sana tu, atleast unapata mtu wa kukufichia siri, kushare na wewe misha na ambaye unabeba full responsibility juu yake. Tatizo ni kwamba inapotokea kitu kibaya basi sisi binadamu hukimbilia kulaumu ndoa kuliko kuangalia nini tatizo.

Pia smile maisha haya ni Mungu tu ndiye anayeongoza na si utash wa mtu pekee. So kwakila kitu mwombe yeye na tamka unataka akufanyie nini basi na si vinginevyo. usipende sana kusikiliza ushuhuda wa kushindwa kama huwez kuutoa akilini kwani utakuharibia maisha yote ma dia.Unalo tatizo tu la kisaikolojia.
 
Last edited by a moderator:
Unajua watu wanatofautiana si kila mtu ana tabia kama za wanaume ulio waelezea hapo. Kwenye ndoa inatafutwa furaha na watoto, mambo mengine ni tabia ya mtu. Naamini hata ukisubiri kwa miaka 20 ijayo hutopata mtu parfect cha kufanya ni kuomba mungu akupe mtu anaye kufanana.
 
Mdogo wangu naomba usichanganywe na vituko unavyosikia toka kwa watu wengine kwani si kweli kwamba ndoa zote ziko hivyo.Tunashuhudia ndoa nyingi tu zenye mafanikio makubwa kimahusiano(familia) na kiuchumi pia.Kikubwa tu ni kuwa wakati wako wa kufunga ndoa utakapofika basi uwe na uhakika ni kipi unahitaji katika ndoa yako na ukumbuke kuwa ndoa inalelewa jambo ambalo watu wengi wanashindwa kulielewa.Jaribu kumwelewa mwenza wako anahitaji nini nawe kuwa wazi kwake juu ya kile unachohitaji toka kwake.Ukikosea mama utakuwa sawa na mtu aliyejibebesha mzigo wa miiba kisha mzigo huo ukampasukia.Kila la Kheri mama..
yaani sijakuelewa hata tone mkuu
 
Unajua watu wanatofautiana si kila mtu ana tabia kama za wanaume ulio waelezea hapo. Kwenye ndoa inatafutwa furaha na watoto, mambo mengine ni tabia ya mtu. Naamini hata ukisubiri kwa miaka 20 ijayo hutopata mtu parfect cha kufanya ni kuomba mungu akupe mtu anaye kufanana.
Smile do smile
 
kama hakuna good men kwa nini watu wanasisitiza ndoa? hii kitu si ipigwe marufuku?
it worth it in the end, remember nothing good comes without a struggle

Mdogo wangu naomba usichanganywe na vituko unavyosikia toka kwa watu wengine kwani si kweli kwamba ndoa zote ziko hivyo.Tunashuhudia ndoa nyingi tu zenye mafanikio makubwa kimahusiano(familia) na kiuchumi pia.Kikubwa tu ni kuwa wakati wako wa kufunga ndoa utakapofika basi uwe na uhakika ni kipi unahitaji katika ndoa yako na ukumbuke kuwa ndoa inalelewa jambo ambalo watu wengi wanashindwa kulielewa.Jaribu kumwelewa mwenza wako anahitaji nini nawe kuwa wazi kwake juu ya kile unachohitaji toka kwake.Ukikosea mama utakuwa sawa na mtu aliyejibebesha mzigo wa miiba kisha mzigo huo ukampasukia.Kila la Kheri mama..
well said, let your expectations in a marriage be known and a compatible person will show up
 
Dah! Smile mdogo wangu wa moyoni, kwanza hongera kwa kuamua kujua ukweli manake huo ni ujasiri sana. ILa pia nasikitishwa sana na haya maisha kwani yanapomfunza mtu basi mifano inayotumika ni migumu na hata kanuni pia hazi apply kabisa mwishowe unakuja gundua kuwa mwanafunzi hajaelewa na mfano bado ni complicated kwa muhusika.

Sababu kubwa zinazomfanya mtu aolewe ni kwamba ili kupata mwenza wa kushirikiana naye katika maisha. nisemapo mwenza wa kushirikiana naye simaanish kitu kingine bali mwenza wa kukidhi haja yako ya kimwili(tendo la ndoa), na zaid yako upate mtu wa kushare naye yaani msiri wako. Mambo mengine kuzaa, kufanya kazi za ndani siyo ishu sana katika hili.

Matatizo meng yanayojitokeza katika ndoa za siku hizi ni kwasababu tu ya mambo yafuatayo, mmomonyoko wa maadili kwa ujumla ila nikitaka kuyaweka mepesi sana nitasema tamaa zisizo na mpango. Binadamu tumekuwa hatuna tena hofu ya Mungu, hakuna menye kuheshimu utu wake na mwili wake. Kwangu mimi hili ni jambo baya sana.

Mfano ukimuona baba bdani ya nyumba antembea na beki 3 jua basi anawez kutembea na mwanae wa kumzaa. Kwanini nasema hivi? Binti wa kazi za ndani ni kama mtoto wako manake unabeba full responsibility juu yake kama mzazi. sasa inapotokea ukamtamani skutofautish kama na kumtamani mwanao wa kumzaa au mtoto wa mkeo. Ni taba mbaya na ya kishenzi.

Nirudi kwako mwenyewe Smile, wewe ni kwamba umefundishwa haya maisha kwa kutumia mifano migumu sana au la niseme maisha yalikufunza kabla hujafikia umri wa kupata shule. hapa naona hujanielewa.
namaanisha mfano mtoto wa miaka 5, labda mzazi analazimisha asome darasa la 1 wakati mtoto huyu ni bado yuko mdogo kiakili na hata kiuwezo wa kupambanua mambo kiasi kwamba akiwa darasani alishazoea kuandka sentensi 2 tu huko nursery hapa lakwanza anatakiwa aandike 10 ni wazi kuwa atashindwa na atakomea kwenye hizi 2 tu. na ukimlazimisha mwisho wa siku utakuja kuua kabisa nia yake ya kupenda kusoma na matokeo nikama haya mtoto kuacha shule au kukata tamaa na shule kabisa.

kwa mfano huo basi mimi nikwambie tu njia iliyotumika kwako ndio haikuwa nzuri katika kukufundisha juu ya maisha. Kuna wenye bahati mbaya ambao mwanzo mwisho wanakutana na mitihani baut hawa ni wachache na hivyo lazima wasikike sana manake wanakuwa wanahangaika katika kutafuta suluhisho la maisha yao. wale wanaopata raha ni wengi pia na hawa hawawez kusema hadharan kwan mgema akisifiwa tembo hutia maji.

Ndoa inauzuri wake sana tu, atleast unapata mtu wa kukufichia siri, kushare na wewe misha na ambaye unabeba full responsibility juu yake. Tatizo ni kwamba inapotokea kitu kibaya basi sisi binadamu hukimbilia kulaumu ndoa kuliko kuangalia nini tatizo.

Pia smile maisha haya ni Mungu tu ndiye anayeongoza na si utash wa mtu pekee. So kwakila kitu mwombe yeye na tamka unataka akufanyie nini basi na si vinginevyo. usipende sana kusikiliza ushuhuda wa kushindwa kama huwez kuutoa akilini kwani utakuharibia maisha yote ma dia.Unalo tatizo tu la kisaikolojia.
kiukweli ushauri wako nimeusoma ila sijauelewa labda nina tatizo na huo msitari wa mwisho...dada
 
kweli umechanganyikiwa, na unahitaji maombi ukemewe jini mahaba lililokuoa likuachie upate kuona umuhimu wa ndoa!! ingawa vitabu vya dini vinasema kuwaaaaaaaaaaa!! and don't take this as an authority....ukiamua kutoolewa , uwe msafi usifanye ngono..that means usiwe unagawa tuu kama peremende na kufanya uzinzi wako kwa kisingizio cha kupenda kuwa singo...kuharibika kwa sekta ya ndoa kunatokana na kuingiliwa kwa sekta hiyo kwa mdudu tamaa aliyepandikizwa na shetani ili kulivuruga lengo kuu la mungu la kuunganisha wanadamu!!! kuwa makini na mawazo haya ni ya kishetani...
 
Unajua watu wanatofautiana si kila mtu ana tabia kama za wanaume ulio waelezea hapo. Kwenye ndoa inatafutwa furaha na watoto, mambo mengine ni tabia ya mtu. Naamini hata ukisubiri kwa miaka 20 ijayo hutopata mtu parfect cha kufanya ni kuomba mungu akupe mtu anaye kufanana.
Smile do smile
unataka kusema hawa woooote wanaoteseka na ndoa hawakumuomba mungu? nitajuaje na mimi mungu atanijibu?
 
KWANI SIS bila ndoa huwezi kuwa na familia?
kampany au mapenzi?

Kuna umri unaweza pata hivyo lakini at some point unahitaji kusettle. Na kwa maumbile yetu sisi binadamu kila mtu anakaubinafsi yaani unataka changu, mume wangu, watoto wangu, penzi langu na si chetu au letu. Kuna umri ambao huwezi pata wanaume ambao hawajaoa, matokeo yake utaishia kuiba waume wa watu kwa ajili ya kutimiza matakwa ya ngono.

Na kingine, mara nyingi mabaya ndio yanayosemwa hivyo mifano ya ndoa nzuri ipo tu ni swala la kumuomba Mungu. Look for real God fearing man, na si hawa wanaume ambao wengi tunakuwa attracted nao.
 
Hizo zote ulizoorodhesha ni sababu "valid" zinazopelekea wanaume na wanawake kuoana. Ila hiyo orodha yako siyo "exhaustive" kwani kama ambavyo wanaume na wanawake walivyo wengi duniani basi na sababu ziko nyingi tu za kuoa. Na mara nyingi wanaume na hata wanawake husukumwa na "combination" ya sababu zaidi ya moja kuingia kwenye ndoa.

Ila jambo moja ni hakika. Bila kujali ni sababu ipi inakusukuma kuoa, ukishaoa/olewa tu utagundua kuwa ndoa siyo "event" ila ni "process" na inakuja ikiwa na "package" ya mambo mengine mengi ambayo hayapo kwenye vigezo vya kawaida vinavyowasukuma wanaume na wanawake kuingia kwenye ndoa. Na mara nyingi hapo ndio watu wengine wanaanza kuchanganyikiwa kwani wanasahau kuwa kuoa ni "process" inayoanza mara tu padre, mchungaji, shehe, mserikali au mzee wa kimila anapowatangaza rasmi kuwa nyie sasa ni bwana na bibi. Hapa sizungumzii hizi ndoa zenu za siku hizi za kujaribishana kwanza kabla hamjazirasmisha.

Nitaongea zaidi kama utahitaji ufafanuzi kwani kuna mambo mazito ambayo itabidi tuulizane umri kwanza kabla sijaendelea.
MIMI ni mtu mzima kabisa mkuu...ongea tu
 
au ndoa zipigwe marufuku?

Halafu itakuwaje? Dar usiku si utakuwa busy kuliko mchana? Kona bar kiingereza kitatawala kuliko kiswahili maana tunaweza tukasahau line ya mwisho ya kitu tusichotakiwa kufanya. Kwa mfano wewe usipoolewa, haya mambo mengine unafanyaje? Au ni juu kwa juu tu!
 
Kuna umri unaweza pata hivyo lakini at some point unahitaji kusettle. Na kwa maumbile yetu sisi binadamu kila mtu anakaubinafsi yaani unataka changu, mume wangu, watoto wangu, penzi langu na si chetu au letu. Kuna umri ambao huwezi pata wanaume ambao hawajaoa, matokeo yake utaishia kuiba waume wa watu kwa ajili ya kutimiza matakwa ya ngono.

Na kingine, mara nyingi mabaya ndio yanayosemwa hivyo mifano ya ndoa nzuri ipo tu ni swala la kumuomba Mungu. Look for real God fearing man, na si hawa wanaume ambao wengi tunakuwa attracted nao.
sasa ukiwa na mtu haupo attracted kwake si ndo itakuwa worse kabisa...
 
Back
Top Bottom