Nimeathirika

JF ni nzuuri saaana, lakini kama unaona inaingilia hata masuala yako ya kazi.....ni tatizo kwani ukikosa kazi na JF yenyewe kwaheri! Amua/tenga muda, usije rudi nyumbani Namtumbo tarafani ambako mbali na internet umeme wenyewe wa taabu mno! Pole bro!
 
Ndugu wana Jamii forums,
natangaza rasmi mbele ya kadamnasi hili kuwa mimi ni muathirika.
Nikiamka asubuhi sifanyi kitu kingine zaidi ya kuingia Jamii,
Kazi haziendi bila ka window ka jamii kuwa minimized mara maximazed.
akili yangu inawaza Jamii Forums.
Kweli mimi ni muathirika na hii kitu imemeza kabisa ufahamu wangu.
Je kuathirika huku ni kwangu mie tu au na wenzangu wapo?

Dawa ni kutoboa macho yako tuu.
 
Registered member yeyote wa JF ni mwathirika, hata mimi mwenyewe nikifungua tu Internet kwenye PC yangu, cha kwanza ni kuangalia JF kuna nini. halafu naendelea na mambo mengine.
 
Dawa ni pale bosi wako atakapokupiga memo ya innefficience kwa kuwa busy na JF.
Au wale jamaa wa IT wakaambiwa waibrock iyo site kwa wale wanaofanya kazi makampuni ya kinoko
 
hahahaha yaani mie nilivyoona heading nikajua umeathirika na haya maradhi yetu
hehehehe kuendelea kusoma kumbe ni kale ka ugonjwa ka wote

Basi nami nilidhani hivyo hivyo jamaa kishagusa mawayawaya...LOL! Siku za nyuma kuna mama mmoja hapa aliomba MODS wamfungie maana kazi zilikuwa haziendi kabisa saa zote yuko JF akijadiliana na wanajamii katika issues mbali mbali lakini hatimaye aliweza kucontrol addiction yake aliyokuwa nayo na hivyo kuweza kuja hapa na pia kufanya kazi zake zilizokuwa zinampatia mkate wake wa kila siku. Hivyo kuja hapa kama unaweza kubalance na mambo yako mengine hakuna ubaya...lakini kama yanalala then YOU HAVE A BIG PROBLEM na inabidi utafute jinsi ya kuitatua au unaweza kuharibikiwa. Nasikia wengine wanawapa watoto wao majina ya kutoka hapa ha ha ha ha ha haka katoto kanatoa points kama yule fundi mchundo wa Jamii, mama nanihii unaonaje tukakaita kwa jina la utani fundi mchundo? Hakuna shida Baba nani hii maana hata mimi yule fundi mchundo ananichengua sana kwa michango yake iliyotulia....LOL!

Good Day!

BAK
 
jamani tuwe realistic wengine wanasema wameathirika lakini ukiangalia ana Posts 2 tu kivipi aathirike? ndio maana mimi sisemi ingawa pia nimeathirika.
 
jamani tuwe realistic wengine wanasema wameathirika lakini ukiangalia ana Posts 2 tu kivipi aathirike? ndio maana mimi sisemi ingawa pia nimeathirika.

samutaimu mtu anaweza akakaa hapa JF anasoma tu bila kupositi kitu na akatumia muda mwingi kuliko hata anayeingia na kupositi kisha anayeya. Kigezo cha post nyingi hakiko ki uhalisia zaidi
 
Pole kamanda niwewahi kuasilika pia lakini nilikwenda bush moja hivi kusko na acees basi ndo pona yangu
 
Kaka mbona umetumia neno kali sana kuelezea addiction yako?
Yaani moyo ulinipasuka , nkajua ndio hivyo tena tuanze kukupa nasaha na kukufundisha chakula bora.
Bwana wee, hiyo addiction ndiyo iliyotawala hapa jamvini.
 
ha ha ha!kwi kwi,kwi1yaani mi nilikuwa mbali kabisa,nilikuwa nawaza mengine..Hauko peke yako ndugu yangu tupo wengu tumekuwa watumwa wa JF.
 
Ndugu wana Jamii forums,
natangaza rasmi mbele ya kadamnasi hili kuwa mimi ni muathirika.
Nikiamka asubuhi sifanyi kitu kingine zaidi ya kuingia Jamii,
Kazi haziendi bila ka window ka jamii kuwa minimized mara maximazed.
akili yangu inawaza Jamii Forums.
Kweli mimi ni muathirika na hii kitu imemeza kabisa ufahamu wangu.
Je kuathirika huku ni kwangu mie tu au na wenzangu wapo?
simple solution,omba ban tu toka kwa invisible atakupa mapumziko ya kutosha.utarudi ukiamua
 
Ndugu wana Jamii forums,
natangaza rasmi mbele ya kadamnasi hili kuwa mimi ni muathirika.
Nikiamka asubuhi sifanyi kitu kingine zaidi ya kuingia Jamii,
Kazi haziendi bila ka window ka jamii kuwa minimized mara maximazed.
akili yangu inawaza Jamii Forums.
Kweli mimi ni muathirika na hii kitu imemeza kabisa ufahamu wangu.
Je kuathirika huku ni kwangu mie tu au na wenzangu wapo?
Aisee bujibuji pole sana hata kuufanyia mwili usafi mara uamkapo unajisahau mpaka upate ka jf,hii ni next level ya uathilika
 
Pole bujibuji kuna ARVS inaitwa BAN tukana mtu utapewa hi habari kwa miezi kadhaa then urudi tena. Pia kuwa makini hata usiku unaweza wacha mkeo kitandani na kwenda kufungua window ya JF.
 
Mimi nakuwa online muda wote nikiwa kazini yaani masaa 40 kwa wiki - lazima kila baada ya dk 10 ni refresh page nione je wadau mmeleta kipi kipya.
 
Ndugu wana Jamii forums,
natangaza rasmi mbele ya kadamnasi hili kuwa mimi ni muathirika.
Nikiamka asubuhi sifanyi kitu kingine zaidi ya kuingia Jamii,
Kazi haziendi bila ka window ka jamii kuwa minimized mara maximazed.
akili yangu inawaza Jamii Forums.
Kweli mimi ni muathirika na hii kitu imemeza kabisa ufahamu wangu.
Je kuathirika huku ni kwangu mie tu au na wenzangu wapo?
ha haa,problem ilikuja mamaa haelewi kiswahili,akajua huwa nachat na demu mwingine mbongo online,basi wee kiliwaka sikumoja mpaka ikabidi nitafute mada moja ya kiingereza nimuoneshe asome ndo akaelewa,na ndo pale ikabidi nirekebishe muda wa kuingia hapa JF.
 
Hahaha mimi nilijua kuwa wewe ni muathirika. Kumbe lahasha. Hapana shaka ndio maana huku kunaitwa Jamii forum ndio uwanja wa usawa kwa watu wote
 
Back
Top Bottom