Lukansola
JF-Expert Member
- Sep 5, 2010
- 5,437
- 1,597
Swala ni kujua chuo gani au kujua kama nilishindwa majukumu na hivyo kuachia ngazi?
pengine anataka kujua uzito wa cheo ulichokuwa nacho ili kupima kama kujizulu kwako makes any news.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Swala ni kujua chuo gani au kujua kama nilishindwa majukumu na hivyo kuachia ngazi?
Ww umeenda soma au kuzibua mitaro na kufagia?Na ndio maana viongozi vijana tunatakiwa kuonesha mfano kama mimi!
Mwaka mmoja uliopita nilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya kutunza mazingira hapa chuoni kwetu na nilipitishwa kwa kura nyingi sana na wanachuo wenzangu na kupata ushindi wa kishindo.
Lakini jana katika mkutano wa mwaka wa kamati ya kutunza mazingira, taarifa yangu ya mafanikio yaliyofikiwa na kamati yangu yameonekana kuwa kinyume na matarajio ya wanachuo wenzangu, kwani kulikuwa na malalamiko mengi sana ya uchafu katika mazingira ya chuo, mitaro kuziba kutokana na uchafu, mazalia ya mbu kutothibitiwa na hivyo kusababisha wanafunzi kuugua malaria kwa kiwango cha kutisha.
Nilikubali udhaifu wa kamati yangu katika kutekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa katika muongozo wa kamati yetu, hivyo niliamua kujiuzulu ili kupisha mtu mwingine mwenye uwezo wa kuongoza.
Nawausia wana JF wenzangu na wananchi wote kwa ujumla, muige mfano wangu, pale inapoonekana mmeshindwa kutekeleza majukumu yenu mliopangiwa hata kama ni majumbani kwenu, basi mkubali kuwajibika na kuachia ngazi.
Nawasilisha!
Miaka 3? Hicho kitakuwa chuo gani ambacho ukifika tu unachaguliwa kiongozi- mwaka wa kwanza? Au ni Madrasa?Uchaguzi wa viongozi hufanyika kila baada ya miaka mitatu, mie nimeachia ngazi baada ya mwaka mmoja tu, si ujasiri huo?
Kwani, wewe ulishindwa majukumu AU uliambiwa kuwa umeshindwa majukumu? Kwani hayo mazalio ya mbu yaliyaonekana siku ya mkutano tu ...!? YOU ARE NOT SERIOUS.Swala ni kujua chuo gani au kujua kama nilishindwa majukumu na hivyo kuachia ngazi?
Bahati mbaya hatuna sheria hiyo, maana tungekuwa nayo, sidhani kama baraza letu la mawaziri la awamu ya tatu na nne lingesalimika, tungekuwa tumewasahau zamaaani!
sifa za kijingaAngel Msoffe inabidi unipongeze kwa kuonesha mfano wa kukubali kuwajibika na kuwapisha wenye uwezo wa kuongoza, mbona simple tu, tena nimepongezwa sana na wanachuo wenzangu kwa kuthibitisha kwamba cheo ni dhamana.
Wakati unakubali majukumu ulikuwa na mpango gani wa utekelezaji? Je, ni nini kilichokukwamisha?
Kujiuzuru peke yake siyo ushujaa na wala siyo maamuzi magumu. Kumbuka kuwa umewapotezea wenzako mwaka mzima wa utekelezaji.
Kuna watu wanataka kuweka kwenye CV zao tu kuwa walikuwa viongozi na kuenjoy prevelages za ustaafu. Ninahitaji kujiridhisha kuwa wewe hauko kwenye kundi hilo, kwa sababu unaonekana kuamini kuwa kujiudhuru ni ushujaa. Ushajaa huanza na kuchukua jukumu unaloliweza, ikitokea likakushinda kama accident ndio unajiuzuru. Sio kuchukua jukumu, unalala mwaka mzima ili mwisho wa mwaka ujiuzuru na kuja JF kudai hongera!
Labda kwenu Bara, huku Visiwani hata njuka anaweza kuukwaa uwenyekiti wa kamati ndogo ndogo za chuo,(Kumbuka sijasema upresident wa chuo) kila mtu anajinadi kuonyesha uhodari wake katika kuongoza kamati ndogo ndogo za chuo na kila mwenyekiti wa kamati hutakiwa kuongoza kwa miaka mitatu,(Muda wa kukaa chuoni) lakini kila mwaka kunafanyika tathmini ya uongozi kama unafaa au la, ukifaulu unaweza kumaliza chuo ukiwa kiongozi na kukabidhi madaraka kwa mwingine.Miaka 3? Hicho kitakuwa chuo gani ambacho ukifika tu unachaguliwa kiongozi- mwaka wa kwanza? Au ni Madrasa?