Nimeamua kutembea na binti wa Kazi, sina jinsi

Mwana Kwetu

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
652
562
Nina mke na watoto 3 wote tunafanya kazi. Tulipozaa mtoto wa pili wife alianza kupunguza umuhimu wa tendo la ndoa sijua ni kwa kuzoea au kuchoka.

Tumewekana vikao vyetu binafsi ili kila mmoja abainishe ni vichocheo gani vinakosekana ili tuviongeze kuboresha mchezo. Wote siyo walevi na tuko karibu kifamilia. Ukifuatilia labda mkeo ana mtu hupewi taarifa zozote mbaya. Sasa tatizo ni kitu gani hatujui. Ukimwuliza naye anakwambia mume wangu nivumilie nitajitahidi ila baada ya mwezi anarudi kule kule. Usipochombeza anaweza kupitiliza hata mwezi bila kukumbushia huku tukiendelea kuheshimiana kwa sana na peace na upendo ukitawala katika nyumba.

Hali hii imenisumbua kwa muda karibu 7 years na ili kuepuka kugombana na kuepuka kwenda nje kupata UKIMWI basi nikaamua nimweleze binti ambaye anatusaidia kazi home na akaonyesha kunisikitikia kwani mi si mtu wa baa useme ningetafuta huko na pia naogopa UKIMWI. Binti akasema anaweza ku handle hiyo situation kwa masharti kwamba ataendelea kuniheshimu mimi pamoja na wife ili chochote kisishtukiwe.

Kwa mtazamo wangu hata kama mtaniona blind ni kwamba huyu binti anatumika ku rescue hii situation la sivyo ningekwenda huko na huko kutafuta viruka njia ambao wangeniweka mahali pabaya zaidi. Tumeanza mahusiano vizuri na tunaendelea kiasi kwamba hata wife asipokuwa tayari mwezi mzima sipati shida na hii imenisaidia kuepuka ugomvi uliokuwa unatokana na tendo la ndoa kutokuwa zuri. Cha ajabu hata kama mchezo tusipofanya na wife mwezi anaona mambo iko sawa maisha yanaendelea ni kucheka na kufurahi bila kujiuliza huyu mume anaishije?

Je wadau katika situation kama hiyo ambayo mke ana behave namna hii kwa ninachokifanya nimekosea au niko sawa. Kama unafikiri nimekosea nipe ushauri kuhusu njia mbadala na jiweke kwenye position yangu.
 
Mkuu hii nimeshindwa kutoa ushauri haswa pale wake zetu wapojifikiria wao tu
 
Haujaepuka kugombana kwa sababu duniani hakuna siri, kama ipo ni ya mmoja na si zaidi ya hapo.
 
He!
Umeamua kucheat na housegirl ku'rescue' ndoa??..ryte!!!!!
Swali muhimu la kujiuliza hapa ni 'mpaka lini'???..
Lingine unaloweza kujiuliza ni 'je mkeo akijua itakuwaje kwa huyo beki3'??
My take: Two wrongs will never make it right!..umechemsha bro!
Malizana na mkeo tu na kama itabidi ufanye infedility it will slightly be justifiable kama utaenda mbali ya nyumbani kwako!!
 
Huo usajili uliompa beki3 ni kwamkopo au? Then housegirl mwenyewe kirukanjia!!!! Kuna heshima hapo tena? Afu utwambie kiwango cha huyo beki 3 kikoje?
 
teh teh teh teh basi mwenyewe unajiona bonge la kidumeeee. Na umesolv ishu kiutu uzima.. Pole yako unachokifanya wewe jua kuwa ni marudio kwa mkeo kwani mwenzako ashachukua uamuzi kama wako kitambo sana.wewe unastukia kujifunika shuka wakati?? Kumekucha...???
 
Yaani hapo kwa house girl ndio umeharibu kabisaaaaa. Mapenzi ni kikohozi, hayafichiki. Afadhali kama kweli umeshindwa ungetafuta nje, na uwe unatumia kinga.

Nikwambie, hapo ndani siku zitakavyoenda hg atakolea na atakuja mtolea uvivu "my wife wako". Halafu, huyo hg anaweza kuwa na kijana mwingine, suala ambalo ni hatari zaidi kukuambukiza magonjwa. Aidha, anaweza kuwasilimulia watu wenye nia mbaya na ndoa yenu halafu wakamshauri kuweka mambo hadharani ili mharibikiwe zaidi.

Kubwa zaidi, jiulize siku ukimkuta na mtu mwingine utamwonea wivu au utatulia tu ? Mambo ya ndoa yanahitaji utatuzi wa wanandoa wenyewe sio kumshirikisha mtu wa nje. Ushukuru Mungu kuwa umeyatoa kwa hg, ungeyatoa kwa yule Dada jirani yako, angezidisha manjonjo mpaka uonje huko, ukishaonja anaongeza manjo njo mpaka uchukue begi na kuhamia kwake kuliko sasa ulivyohamia chumba cha watoto.

Aidha, elewa kuwa wanawake wana akili sana, huenda anafahamu kuwa unakula hg ndio maana kapunguza mapenzi na wewe, kwa maana kwamba hana tena msisimko na wewe. We acha tu ampate wa nje ambaye anajituma, utamkosa hivi hivi. Wengine wanatumia...n..d..i.....m..i.
 
Uamuzi uliochukua naweza sema ni wa kijinga sana.. Alafu nakuonea huruma maana najua mahousegirl asilimia kubwa ni vicheche hawajatulia hata kama anaandaa meza huku akitembelea magoti. Alafu kingine mkeo atakuwa na tatizo kama anatumia njia za uzazi wa mpango hasa sindano chaweza kuwa chanzo.
 
Back
Top Bottom