Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Ni takriban miezi miwili sasa mgogoro huu umekuwa ukifukuta chini kwa chini na sasa imefikia mahali humu ndani hapakaliki wala hapaliki, ilimradi tafrani kila kitu vululu vululu. Nimelinyamazia jambo hili lakini sasa nimeamua kumuacha mke wangu mama Ngina ili roho yangu ipate kutulia.
Ni miaka mitatu sasa imepita mke wangu hajaenda kuwaona wazazi wake huko kijijini, na hiyo ilitokana na majukumu ya kibiashara anayoiendesha, nakumbuka mwanzoni mwa mwezi wa sita tulikubaliana itakapofika mwezi wa kumi mwaka jana aende kuwaona wazazi wake lakini ilibidi tuiahirishe safari hiyo kutokana na mimi kupata ajali na kulazwa hospitalini. Lakini tangu nipone na kurejea kazini mwenzangu kanibadilikia anataka kwenda kuwaona wazazi wake kwa sababu amewa-miss sana.
Nilikuwa nimepanga aende mwishoni mwa mwaka huu kwa sababu alilazimika kufunga biashara kwa takriban miezi miwili akiniuguza, na tangu afungue hajakaa hata miezi miwili na sasa anataka kufunga tena asafiri. Swala hilo limekuwa likizua manunguniko na sasa imekuwa nongwa kila nikirudi nyumbani jioni hakuna maelewano na anachotaka ni kusafiri ili akawaone wazazi wake.
Sasa nimeona bora yeshe, nimruhusu aende kuwaona wazazi wake akae huko kwa mwezi mmoja mpaka hamu yake iishe ndipo arejee, lakini kakataa anataka akakae wiki moja tu ndipo arudi kwani hayupo tayari kuniacha peke yangu kwa muda wote huo ikizingatiwa bado sijapona vizuri na ninahitaji ukaribu wake. Nimeona isiwe tabu tumeafikiana na sasa anajiandaa kwa safari wiki ijayo Mwenye enzi Mungu akipenda atasafiri, na mimi nitabaki nyumbani na wanangu Ngina, Ngano na Ngadu. Muombeeni mama yenu, wifi yenu au shemeji yenu safari njema .LOL