Nimeamua kujiunga na jeshi la m4c

Mbalinga

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
1,714
1,370
Nimechoka kuwa mpiga debe wa M4C sasa nataka nijiunge na jeshi la M4C (CDM). Ninaishi Kijitonyama, Je ufisi za karibu za CDM ziko wapi, nahitaji kuchukua kadi yangu rasmi. Na natoa wito kwa wengine wote wapiga debe sasa tufanye kwa vitendo zaidi. NAOMBA WADAU MNIFAHAMISHE OFISI YA CDM ILIYO KARIBU NA KIJITONYAMA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Karibu sana,jamani mwelekezeni ofisi ndugu yetu, mlio maeneo ya huko
 
Hongera kwa kutambua maendeo na mabadiliko ya taifa hili yanamuhitaji kila mmoja wetu hasa kwa vijana ambao ni chachu ya maendeleo
 
Nzi na Nyuki hufa kwa kulazimisha kupenya kwenye kioo angavu.

Ndivyo watakavyo angamia wasomi, wafanyakazi na wakulima wanaolazimisha kutimiza ndoto zao kupitia ccm.

Sasa tuko kwenye kampeni maalam dhidi ya ccm 2015, waliingia kwa mbinu na watatoka kwa mbinu, watenda hutendwa
KARIBU SANA KWA PAMOJA TUISAPORT CHADEMA, Tanzania bila ccm inawezekana!

Wape ujumbe huu wenzako na waale wote waliochoshwa na ccm hasa;
WAKULIMA, WALIMU, NMB, TRL, WAZEE WA EAC na WANAFUNZI VYUONI.

MUNGU IBARIKI CHADEMA NA WANACHAMA WAKE.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Wewe unga tu hadi makao makuu kinondoni utapokelewa na kuelekezwa vizuri zaidi. Nenda mpaka american chips ulizia ofisi za gari la ukombozi utaonyeshwa mkuu.
Well done.
 
Nenda Kinondoni karibu na makaburi (yale ya mwanzo) utaelekezwa Makao Makuu. Nenda na picha passport size mbili na shilingi elfu mbili tu. Hapo jirani utapima gwanda kwa kamanda Fundi Hoza; bei ni sh.70,000 tu. Ukitaka safari buti ya Bata nenda pale Kinondoni Manyanya; then utatoka full kamanda.

Hongera sana kwa uamuzi.
 
Karibu sana huku hakuna bagia wala chapati wala tisheti, kikubwa kwetu ni ukombozi KARIBU
 
Nenda Kinondoni karibu na makaburi (yale ya mwanzo) utaelekezwa Makao Makuu. Nenda na picha passport size mbili na shilingi elfu mbili tu. Hapo jirani utapima gwanda kwa kamanda Fundi Hoza; bei ni sh.70,000 tu. Ukitaka safari buti ya Bata nenda pale Kinondoni Manyanya; then utatoka full kamanda.

Hongera sana kwa uamuzi.

full maelezo. thanx mkuu. huyu kamanda nina uhakika kayapata vizuri. saafi sana.

Tuendeleeni kuwaelimisha watanzania, waelimike ili waliondoe madarakani hili li serikali la ccm magamba/mafisadi/majambazi/wauaji.
 
Ila huwa hatupeani posho huku',jiandae kujitolea kamanda.2po chimbo dhidi ya CHAMA CHA UKOO.
 
Nenda Kinondoni karibu na makaburi (yale ya mwanzo) utaelekezwa Makao Makuu. Nenda na picha passport size mbili na shilingi elfu mbili tu. Hapo jirani utapima gwanda kwa kamanda Fundi Hoza; bei ni sh.70,000 tu. Ukitaka safari buti ya Bata nenda pale Kinondoni Manyanya; then utatoka full kamanda.

Hongera sana kwa uamuzi.

Hii kali kijiunga na jeshi la ukombozi mpaka ulipe?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Njoo sinza kijiweni Opposite na sheli inayopakana na BOA (Bank of Africa). Fuata barabara ndogo inayopita katikati ya maduka. Ofisi ya kata iko hatua 30 hivi toka barabarani. Kuna bendera kubwa na viongozi wapo muda wote!.. Pia utawakuta mafundi wanashona kombati nzuri bei ikiwa 50,000 -70,000 kulingana na ubora wa kitambaa. Kadi zetu ni sh. 1500/= (kiingilio -500 na ada ya mwaka mmoja 1000). Passport size moja ni muhimu sana. Unaweza kulipa ada hata ya miaka sita mpaka 15. Kama una kadi au Tshirt za magamba au bi mkubwa uje nazo!.. KARIBU SANA TUMNG'OE NDULI!....
 
unadhani ni magamba ambapo mtu kujiunga anapewa ubwabwa na vitumbua..

Sijawahi kujisikia ukiingia jeshi la ukombozi inabidi ulipe vinginevyo kina Garang na Savimbi wasingekuwa na askari; mtaliwa sana safari hii.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Wewe umetoka ukanda upi na Kabila gani na dini gani ndo Unaweza ukajiunga Ukijibu hayo.Hatutaki wakuja
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom