Sooth
JF-Expert Member
- Apr 27, 2009
- 3,928
- 5,615
Huu ni unafiki tu, yaani uamuzi wako wa kujiunga na CCM nao ni mada ya kujadiliwa? Kama una mapenzi ya dhati na CCM ungejiunga nao kimya kimya. Unatutangazia ili tuamini kwamba CCM bado inaungwa mkono na Watanzania? Waacheni ambao hawakufanikiwa kuunda serikali waseme, mlio serikalini fanyeni kazi, vitendo vionekane, ndipo wananchi watawakubali. Kama unafanya kazi, wananchi wataona, huhitaji kuwatangazia wananchi kwamba unafanya kazi.