Nimeamini, CHADEMA ni Wasikivu…….Soma Hii Hotuba Uone!

English Learner

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
355
355
Jumamosi ya Tarehe 7, Mwezi Aprili, Mwaka 2012, siku ambayo CDM walikuwa wanaandaa mkutano Arusha kueleza hatua itakazochukua kufuatia kutenguliwa kwa Ubunge wa Mh. Lema, nilitoa pendekezo la kipande cha kuwemo kwenye Hotuba ya Mwenyekiti wa CHADEMA (Kipande chote kimenukuliwa hapo chini). Leo katika tathmini yangu nimebaini kuwa Mwenyekiti na CDM kwa ujumla waliitika, waliikubali na wanaitekeleza hotuba yangu. Kwa moyo wa dhati uliyojaa furaha nawapongeza sana CDM kwenye kufanyia kazi ushauri mzuri.

Ebu nikuonyeshe sehemu walizofanyia kazi:

“….Makamanda, tuwaambieni ccm, kwa mara nyingine tena imekula kwao! …..na sasa tunasema na hili la Mh. Lema ishakula kwao! ……

……….. .Tunaishukuru mahakama ya ccm kwa kutoa kibali kinachompa Mh. Lema muda wa kutosha kukiimarisha chama nje ya Arusha. Mh. Lema tutakuomba likizo yako ikiisha upelekee Taarifa ya Kazi kwa Mzee Mkama na Nakala kwa M/Kiti Kikwete. Mh. Lema, chama kitakupa jukumu jipya. Toka sasa Jimbo lako la Utumishi litakuwa Tanzania nzima. ……

……….. Kwa kadri Allah atakavyokuwezesha, utakwenda kila mkoa, kila wilaya, kijiji na kila tarafa. Ukaamshe, uanzishe, uimarishe na kukomaza fikra za ukombozi.

Hii kampeni yako itaitwa “Operation Ukombozi”….”

Hii wamebadilisha kidogo kuendana na maeneo wayokwenda. Kwa mfano sasa uko Mtwara na Lindi, inaitwa Operesheni Okoa Kusini=UKOMBOZI


KIPANDE CHA HOTUBA KILICHOPENDEKEZWA


……….. …………

“Ndg. Wananchi, sisi viongozi wa Chadema tunaishukuru sana ccm, serikali yake na vyombo vyake vyoote vya dola. Tunawashukuru kwa jinsi wanavyotusaidia kuujulisha umma kwa vitendo kuwa dhamira ya chama cha mapinduzi:


  • Si kulinda mali na rasilimali za nchi hii bali kuzitelekeza na kuziteketeza!

  • Si kumkomboa Mwananchi bali kumkomoa!

  • Na wala hawapo kwa ajili ya kulinda na kutetea haki zako wewe Mwananchi, bali wapo kuhakikisha hautambui haki zako, na kama haujaelimika ubaki mjinga ili wakutawale milele bila kelele!

Awali tulipowaambieni hayo ndo malengo na undani wa ccm, wachache walituelewa haraka na wengi polepole wanaendelea kutuelewa. Kumbukeni jinsi Dr. Slaa alivyodhihakiwa baada ya kutoa orodha ya Mafisadi pale Mwembeyanga, kumbukeni jinsi Mh. Zitto Kabwe alivyoadhibiwa na Bunge kwa kufichua Uchafu wa Mawaziri wa ccm, kumbukeni jinsi wananchi wa Zanzibar, Mbeya, Tabora na hapa Arusha walivyokutana na dhahama katika kutetea maamuzi yao na kuutumia uhuru wao wa kikatiba wa kuchagua viongozi wawapendao.

CHADEMA tungekuwa waongo, ccm hata isingekiri baada ya uchaguzi Mkuu kuwa ndani yake si kama kuna mafisadi tu, bali kuna yale yaliyokubuhu, yenye MAGAMBA mazito yaliyoshindikana hata kuvuliwa. Msingesikia kesi (japo gheresha) za EPA. Hata hiyo dharau ya majambazi kurudisha pesa na yasijulikane wala kuchukuliwa hatua za kisheria isingetokea. Viongozi wa CHADEMA wangekuwa waongo, leo hii Dr. Slaa angekuwa gerezani akiwa anatumikia vifungo vya kesi zaidi ya 100, Badala ya Nazir Karamaghi kupotea kabisa kisiasa Mh. Zitto ndiye angepotea, Mbowe naye sijui angekuwa wapi? Lakini kubwa zaidi vijana kama Lema, aliyethibitisha uongo wa Waziri Mkuu tena mbele ya Bunge, kijana kama Lema aliyesimama upande mmoja na wanyonge katika kutetea haki, kijana ambaye sasa kila Mtanzania anamfahamu kama mtu hasiyetishwa na maji ya pilipili, mabomu ya machozi, gereza, kisu, risasi na wala haongeki kwa pesa au cheo! eti serikali-ccm kwa kutumia Mahakama inaamua kumuondoa katika siasa na harakati za ukombozi kwa kipindi wakitakacho wao! Thubutu…haiwezekani na kamwe haitawezekana! Peoplesssss…………

Makamanda, tuwaambieni ccm, kwa mara nyingine tena imekula kwao! Ilikula kwao na inazidi kula kwao kwa kumbeza Dr. Slaa mara zote, ilikula kwao kwa kumsimamisha Mh. Zitto ubunge, ikala kwao kwa kuwapeleka Wanafunzi wa Elimu ya juu likizo ili wasishirikia uchaguzi Mkuu, inazidi kula kwao kwa kudandia hoja ya Ufisadi huku MAGAMBA magumu yakiwa yamewakwama, mchakato wa Katiba Mpya utakaa sawa na kula kwao, na sasa tunasema na hili la Mh. Lema ishakula kwao! Tunao ujasiri wa kusema kwa hakika kuwa imeishakula kwao kwa sababu CHADEMA daima inasimama na matakwa ya Haki za Wananchi. Na kwa sababu hiyo, ndo maana nanyi daima mnatupa nguvu kwa kutambua kuonewa kwetu na kutupa moyo kwa hali na mali. Vivyo hivyo nasi tunapigana juu ya kuonewa kwenu, kudhulumiwa kwenu na ubadhilifu wa rasilimali za nchi yetu.

CHADEMA inao na bado inawahitaji sana vijana jasiri kama Mh. Lema. Hasa katika kipindi hiki ambacho tayari Wananchi mmetuhakikishia kutwaa dola hapo mwaka 2015, CDM inahitaji sana nguvu kazi ya watu wanaojituma kama Mh. Lema. Tunaishukuru mahakama ya ccm kwa kutoa kibali kinachompa Mh. Lema muda wa kutosha kukiimarisha chama nje ya Arusha. Mh. Lema tutakuomba likizo yako ikiisha upelekee Taarifa ya Kazi kwa Mzee Mkama na Nakala kwa M/Kiti Kikwete. Mh. Lema, chama kitakupa jukumu jipya. Toka sasa Jimbo lako la Utumishi litakuwa Tanzania nzima. Kwa kadri Allah atakavyokuwezesha, utakwenda kila mkoa, kila wilaya, kijiji na kila tarafa. Ukaamshe, uanzishe, uimarishe na kukomaza fikra za ukombozi. Hii kampeni yako itaitwa “Operation Ukombozi” ………………………………….”
 
mbona mengi tuu CDm wanafanya kwa ujumla si wabishi as long as yanaleta sense.Ni chama cha wananchi,na hivyo kinafanya unayotaka.It speople power.
 
Back
Top Bottom