- Thread starter
- #121
KATIKA hili huwa sitafuni maneno! Dr. Slaa hakushinda urais mwaka 2010 na wale wanaoamini hivyo ni ama tu wanaamua kueneza propaganda au hawafanyi tafakuri za kina! Kwanini naamini hakushinda:
Huu ni ukweli ulio wazi ingawaje wafuasi na mashabiki wa CHADEMA wasioifahamu vizuri CHADEMA wanataka kuukataa na kuishia kulalamika eti kulikuwa na wizi wa kura!!!! Hata kama palikuwa na wizi wa kura, bado hata kama ingefanyika ON and OFF, still kura zisingetosha kuipa CHADEMA ushindi!!
- Hadi General Election 2010 ( nap engine hadi sasa), nguvu ya CHADEMA nchini ilikuwa unevenly distributed. CHADEMA hawakuwa na ufuasi wa kutosha mikoa ya Lindi, Mtwara, Dodoma, Singida, Pwani, Morogoro, Tanga, Ruvuma, Rukwa, Tabora, Iringa Pamoja na Zanzibar. Hadi wanaingia kwenye uchaguzi (nna pengine hadi sasa), zaidi ya nusu ya nchi ilikuwa haijafikiwa na CHADEMA na wala hawakuwa na japo na ofisi huko!! Huwezi kushinda nafasi ya urais wakati zaidi ya nusu ya nchi hauna ufuasi wa kutosha!
- Hata ile mikoa ambayo ilikuwa na ufuasi wa kutosha, bado ufuasi huo ulikuwepo kwenye baadhi tu ya wilaya/majimbo na sio mikoa mizima! Hii ilikuwepo Kilimanjaro, Arusha, Kagera, Manyara na hata Mwanza.
- Mikoa ambayo CHADEMA ilikuwa na nguvu (Namba 2 bove), CCM pia ilikuwa na ufuasi wa kutosha....hivyo CCM ilitoa changamoto kubwa huko kuliko changamoto ya CHADEMA dhidi ya CCM kwenye mikoa ambako CCM ilikuwa na nguvu.
- Mikoa ambayo ilikuwa ni ngome ya CCM, CHADEMA ilikuwa ni mahututi kabisa lakini hii ni kinyume kwa sehemu ambako ilikuwa ni ngome ya CHADEMA .huko CCM haikuwa mahututi!
- Ilikuwa ukisikia sehemu Fulani CCM wana nguvu, basi ushindi wao huko unakuwa wa kishindo ..na hii ilitokea kwenye maeneo mbalimbali ya nchi! Kinyume chake, ilikuwa hata ukisikia sehemu fulani CHADEMA wana nguvu, basi ushindi wao ungekuwa wa kawaida (Less than 65%) kwavile CCM nako walikuwa na wafuasi wa kutosha kuzuia massive winning!
Dr. Slaa na wenzake wanalifahamu hili, lakini katika kuendeleza propaganda za kisiasa ndipo wanawahadaa wafuasi wao kwamba waliibiwa kura!!! Na hakika CHADEMA haitakuja kushinda uchaguzi hadi watakapobaini na kukubali kwamba maeneo mengi ya nchi hawajafika huko!!! Kukubali peke yake haitoshi, ni hadi pale watakapofanya jitihada za makusudi kukieneza chama sehemu mbalimbali za nchi; hususani kwenye mikoa niliyoitaja in (1) above!!
CHADEMA hawatakuja kushinda uchaguzi (kwa nafasi ya urais) hadi watakapoondokana na dhana ya kwamba Watanzania watawachagua tu wasipowafikia! Tutake tusitake, hadi General Election inafanyika 2010, vijiji vingi walikuwa wanazikana, wanafanya sherehe, wanachanganyikana na makada wa CCM ambao wameenea from the grassroot!
Punguza jazba mkuu.Hata ukitumia hekima kidogo tu watu watakuelewa.