Niliyoyafanya tangu niwe Mbunge-Shukrani kwa WanaJF

Status
Not open for further replies.
Tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupa kwa hizo takwimu ni za kisiasa tu, nikiweka takwimu za Magufuli humu mambo aliofanya tutajaza server ya JF
 
hongera sana Mh Mbunge,angalau umeosha machache,sidhani kqma huyo Papaa Mteketa ana chochote alichofanya,mara nyingi anaweza kusum up yako na wadau wengine wa maendeleo kamakafanya yeye.

Mie sitaki kujua how,when etc, naombi jingine,nimeshapita njia mpaka Mlimba,nilishangaa sana pale Chita kambi ya jeshi iliyo karibu na Kihansi haina umeme,ni aibu sana kwa nchi,watendaji wa wilaya,jeshi na TANESCO kuamua kuuchuna eti kisa wajeshi huwa hawalalamiki,wanakufa kisabuni. Ni miaka zaidi ya kumi na sita tangu waanze kuzalisha umeme pale kihansi,kwa akili ya kawaida tungetegemea mipango iwe imefanyika kuhakikisha wajeshi wanapata umeme. Mie sio mjeshi lakini nawashangaa pia viongozi wa jeshi ambao wamekosa uwezo wa kudai umeme,au wanafurahia kuchakachua diseli ya jenereta?
 
Pia tusisahau kuwa Kiranga lazima atakuwa na maswali, nadhani atakuwa amechelewa kidogo tu, ila takuja hapa, tafadhali msimvunje moyo akija na maswali yake kwasababu tu ya ushabiki wa mbunge husika, so far as haitakuwa mashambulizi ambayo yanaweza kuwa classified as personal, basi mambo safi tu...ndo JF hii...
 
Tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupi kwa hizo takwimu ni za kisiasa tu, nikiweka takwimu za Magufuli mambo aliofanya tutajaza server ya JF

Kila mtu ana haki na wajibu wa kujivunia kile alichotekeleza kwa nafasi yake.

Kama una mengi ya kusema juu ya magufuli, unaweza kuanzisha thread ya accomplishment za magufuli kwa 2011.

Hii habari ya kujaza server ya JF ni kukosa hoja, we unafahamu uwezo wa server ya JF?
 
Wakuu habari!

Ni matumani yangu kuwa tumejiandaa kumaliza mwaka vizuri na kuplan vizuri for next year.

Tukiwa tunafunga mwaka nimeona niandike kwa kifupi yale niliyoyafanya kwa kipindi Cha mwaka mmoja tangu kuapishwa kuwa Mbunge wa Vitimaalum Nov 12,2010.

Taarifa hii inaonyesha utekelezaji wa Kazi za Ubunge,Kazi za chama Wilayani Kilombero na Kazi za Chama Kitaifa.

A. KAZI ZA KIBUNGE
Tangu nimeapishwa nimefanikiwa kufanya Kazi mbalimbali za Kibunge Wilayani Kilombero,Jimbo ambalo niligombea na kupata Kura 38,550 sawa na asilimia 45 ya kura zote zilizopigwa. utekelezaji wa awamu hii ulikuwa ni QUICK WINS. Quick zifuatazo zimefanyika;
1. Nimepigania bei ya Sukari ishuke -Kuna maeneo Bei imeshuka lakini maeneo mengine hali bado ni mbaya. Kilombero ni Wilaya inayozalisha Sukari, Kiwanda Cha Illovo hivyo bei ya Sukari unapaswa kuwa chini kuliko maeneo yasiyodhalisha Sukari.
2. Nimepigania kituo Cha Polisi Cha Wilaya kiboreshwe-kimeboreshwa
3. Nimepigania kituo Cha afya Cha Mlimba kipatiwe Maji na Ambulance lirudishwe hivi vyote vimefanyika.Ambulance ilikuwa gereji zaidi ya miezi Sita mwaka 2010.
4. Nimepigania utekelezaji wa huduma bure kwa Wajawazito,Watoto chini ya Miaka Mitano,Wazee na Wenye Ulemavu-Kuna maeneo imefanikiwa maeneo mengi bado.
5. Nimetetea haki za Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Na KPL-Baadhi ya Kero zimetekelezwa lakini nyingine bado-Suala la Maslahi bado ni tete,suala la Usalama Kazini bado ni tete.
6. Nimetetea na kusimamia kero ya Wakulima na Wafanyabiashara ya kuongezeka kwa Ushuru bila kushirikishwa katika hatua zote muhimu.
7. Nimepigania haki ya Umeme kwa Wananchi wa Kilombero kwani tunavyanzo viwili ya umeme,Kihansi na Kidatu.REA imeenda kule ila inasua sua sana lakini Wizara imetuhakikishia kuwa inatekeleza azma yake ya kupeleka umeme maeneo yote ya karibu na vyanzo vya umeme.
8. Nimepigania barabara ya Kidatu-Ifakara kwa kiwango Cha lami-imeshindikana kwa mwaka wa fedha 2011-2012.
9. Nimesomesha Wanafunzi 86 Sekondari,13 Vyuo Vikuu hawa wa Vyuo Vikuu walihitaji kutoa advance ili waweze kusajiliwa then wapate Mkopo
10. Nimeezeka madarasa mawili(2) ya shule ya Msingi Mkula
11. Nimegharamia Visima viwili vya maji
12. Nimehudumia Baba aliyekuwa kipofu kwa miaka 8 akaweza kuona tena kupitia hospitali ya CCBRT
13. Nimesaidia wagonjwa wengine zaidi ya 42 wakapata huduma za afya na kupona
14. Nimesaidia Jezi kwa Vijana katika Kata 12 Kati ya 23 za Wilaya ya Kilombero
15. Nimefanikisha ligi Mbili katika Kata Mbili-Ligi za Mpira wa Miguu na Netboli
16. Nimeshiriki kwenye fundraising katika Misikiti 3 na Makanisa 4
17. Nimekuwa sehemu ya kufanikisha Uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishirki Cha Mt Fransisco
18. Nimeshiriki kuwasaidia Wahanga wa Mafuriko Wilayani Kilombero
19. Nimefanikisha Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kushirki Umitashumta ngazi ya Wilaya,Mkoa na Taifa
20. Nimefanikisha Vikundi Viwili vya kina Mama Wajane kuweza Kujiajiri na kuendesha maisha yao wenyewe.
21. Nimefanikisha Vikundi 5 vya kina mama kuweza Kujiajiri.
22. Nimefanikisha Vikundi 3 vya wenye ulemavu Kujiajiri wenyewe.
23. Nimefanya Mikutano ya Hadhara ya Elimu ya Uraia pamoja na Shukrani zaidi ya 20.

Na mengine madogo madogo mengi.

B. KAZI ZA CHAMA WILAYANI KILOMBERO

Katika kukuza chama Wilayani Kilombero nimefanikiwa kufanya yafuatayo;
1. Nimelipia na kufungua Ofisi za CHADEMA katika Kata 5
2. Nimefungua na Kuzindua Matawi 13 yaliyojengewa na yenye Uongozi wa Kudumu
3. Nimeingiza Wanachama zaidi ya 8,000

C. KAZI ZA CHAMA ZA KITAIFA
1. Nimeshiriki Maandamano ya CHADEMA Kanda ya Ziwa katika Mikoa yote ya Kanda hiyo katika kupigania haki za watanzania.
2. Nimeshiriki Maandamano ya CHADEMA Nyanda za Juu Kusini kasoro (Mikoa ya Iringa na Ruvuma) katika kupigania haki za watanzania.
3. Nimeshiriki kwenye Kazi za Siasa Arusha - Sakata la Kuvuliwa Uanachama Madiwani kusaka muafaka.
4. Nimeshiriki kwenye Uchaguzi Mdogo wa Igunga
5. Nimeshiriki kutoa Mafunzo ya Mapungufu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2011 katika Mkoa wa Ruvuma
6. Nimeshiriki kwenye Siasa za Vyuo Vikuu, Makongamano, Mikutano ya Hadhara na Uzinduzi wa Matawi
7. Nimeshiriki kwenye Siasa za Dodoma, Singida na Morogoro.

Natambua nilipaswa kuyafanya zaidi ya haya lakini kutokana na sababu mbalimbali hayo ndio niliyofanikiwa kuyafanya. Angalau nimefanikiwa kufanya karibu asilimia 70 ya niliyopanga kuyafanya kwa mwaka huu 2011 kama Mbunge wa Vitimaalum Wilayani Kilombero.

Naomba nichukue fursa hii pia kuwashukuru wanaJF wote kwa support yenu kwangu kwa hakika ninawashukuru sana tena sana.JF imekuwa ni nyumbani, JF imekuwa ni darasa, Vile vile JF imekuwa ni Tanuru la Moto maana wakati mwingine huwa ninaingizwa kwenye moto hasa. Na mwisho nichukue fursa hii kuwaomba radhi wale wote niliowakwaza kwa namna moja ama nyingine, tuanze upya mwaka ujao..

With Love
Regia
Mimi nina kaswali, je ungependelea kubakia kuwa mbunge ama unadhani unaweza majukumu makubwa zaidi?

Je haya uliyoyafanya na kuya mention, ni kwasababu unataka ubakie kuwa mbunge, upate nafasi ya juu zaidi, ama ni moyo yu umekutuma kuonyesha jinsi unavyowatumikia wananchi bila kutegemea kuwa utachaguliwa tena?

Je kama usipochaguliwa tena ni kweli kuwa hutajali licha ya kuwafanyia wananchi hao mambo yote hayo? Would you hold grudges for it happend the second time?

Sitll naamini kama ni kweli hayo uliyomention hapo juu ni kutokana na jitihada zako, basi hii itatufanya pia tuwaulize kina Zitto na wengineo kama they can do the same.

Shida niliyonayo na wanasiasa ni kwamba they do something in order to get something of move value to them...
 
hongera sana!
Ila pigania sana haki za wafanyakazi viwandani sio hapo Kilombero tu bali nchi nzima kwani hawapati haki zao kabisa.
Ukianzia na working condition ni mbaya kupita maelezo, contracts ni za muda mfupi na mafao yao yaani mishaharakwa siku ni midogo mno unaweza kuta kama pale Maguni, Tumbaku Morogoro kwa siku unalipwa 3000 hii inamaana kwa mwezi unalipwa 66000 kwa siku za kazi.
Inasikitisha yaani unafanya kazi mpaka unazeeka hauwezi jenga hata kibanda.
Otherwise nikutakie 2012 yenye mafanikio.
 
hongera Regia, japokuwa mimi siyo mpiga kura wako, lakini nimeona jitihada zako, nakutakia heria ya mwaka mpya, na mafanikio zaidi.
 
Hongera RM Mbunge halali wa kilombero.tathmini binafsi ni nzuri kuliko kusubiri kutathminiwa.unajua ulipotoka na unapoelekea na kama kuna mapungufu watu wanayajua na kuweka inputs zao
keep it up!
 
dada! Kwanza nikupongeze kwa kaz nzur ya maendeleo unazofanya, kaza buti. Ila nnalokwambia ni hyo namba tano [5] kwenye kaz za kbunge, ukpgania hapo kufa na kupona hayo mengne hayatokupa shda sana. Nakutakia mafankio zaid.
 
UMESHIRIKI KWENYE SIASA" nilikuona kweye midahalo quality ya uwanasiasa wako bado iko chini hasa kujenga hoja,jirekebishe soma vitabu vya public speaking ,fanya reseach uwe na data
 
Tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupa kwa hizo takwimu ni za kisiasa tu, nikiweka takwimu za Magufuli humu mambo aliofanya tutajaza server ya JF

magufuri yupi mjomba wa kujaza server kwa mafanikio? Kama ni huyu mzinza wa chato hadi sasa umeme umemshinda pale kwake.
 
Mkuu nakushukuru sana kwa comment yako.Nimefurahi pia kuona ni jinsi gani unavyoifahamu na kutambua Kero za Kilombero.Kifupi baadhi ya Kero nilikuwa ninazifahamu na baadhi ndio nimezisikia kwako,huu ndio utamu wa JF.
Kifupi ndio nimeanza kuandika kero mbalimbali nilizozikusanya then na kuandaa MPANGO KAZI wa mwaka 2012 ambao nadhani nitauweka humu JF pindi utakapokuwa tayari.Mkakati utakuwa nikusemea Bungeni kupitia Maswali na Majibu,Kuingiza kupitia Bajeti za Kambi ya Upinzani,Kusemea kwenye Vikao vya Madiwani,Kusemea kupitia Media na njia nyinginezo za kuandika barua kwa wahusika kupitia Ofisi ya Mbunge RM Wilayani Kilombero.
Thank You once again



Hongera sana Regia kwa kazi nzuri,

Labda ningependa kufahamu umejipanga kiasi gani kukabiliana na changamoto ambazo hukuweza kuzitatua kwa mwaka huu, hasa kwa uchache hizi zifuatazo ambazo nadhani zinahitaji kushughulikiwa haraka.

1. Mgogoro wa uongozi wa chama wilayani kilombero, kuna taarifa kwamba kuna makundi mawili yanavutana hadi kusababisha kuhatarisha ustawi wa chama wilayani kilombero.
2. Maslahi ya wakulima wa miwa kiwandani Illovo, ongezeko la bei ya miwa kutoka sh.60,000 kwa tani moja ya miwa inayolipwa sasa pamoja na ombi la wakulima hao kutaka kuwepo na muwakilishi wao wakati wa upimaji wa miwa ili kuongeza uwazi na kuaminiana.

3.Suala la kiwanda(illovo) kuchelewa kuchukua miwa toka mashamba ya wakulima inapotokea ajali ya moto hivyo wakulima kupata hasara kwa kushindwa kuiuza inapokuwa imepitiliza muda wa kuingia kiwandani.

4. Maslahi ya wafanyakazi pamoja na mazingira bora ya kazi kwa wafanyakazi wa Illovo na Kilombero plantations. Hapa pia kuna tatizo la management kupandikiza watu wao ndani ya uongozi wa TPAWU ili kuendeleza agenda yao ya kuwalipa ujira mdogo wafanyakazi wengi wa ngazi ya kati na chini na kuwalipa vizuri wazawa wachache ili watumike ku justify dhulma yao na wao wenyewe makaburu wakijilipa mishahara minono, na wengine wakiwa hawana hata taaluma zilizokosa watanzania hadi kuwapa fursa makaburu hao wafanye kazi nchini.

5.Ujenzi wa barabara za Kidatu-Ifakara, Ifakara-Mngeta/Malinyi na Ifakara-Mahenge. Hapa pia kuna haja ya kujenga/kupanua daraja la mto kidatu ili kuruhusu magari makubwa ya mizigo kuvuka kutoka ruaha-ifakara. Daraja lililopo ni finyu kiasi fulani kupitisha magari makubwa.Hii itasaidia kurahisisha usafirishaji wa mazao ya wakulima kama mchele hivyo kuongeza tija kwa wakulima.

6. Ufufuaji wa kiwanda cha mang'ula, ili kuongeza ajira kwa vijana wa kilombero na morogoro kwa ujumla.

7.Uanzishwaji wa kiwanda cha sukari maeneo ya mbingu. Kulikuwepo na proposal miaka michache iliyopita toka kwa kampuni ya AL Hushoom ya kutaka kujenga kiwanda hicho, sijui hili liko katika hatua gani. Niliwahi kusikia kuna mchezo mchafu ulikuwa unachezwa kati ya uongozi wa mkoa kwa kushirikiana na Illovo kuzuia Al Hushoom kuruhusiwa kujenga kiwanda cha sukari.

8.Suala la kilomo ndani ya bonde la mto kilombero ambapo mamlaka ya bonde imegawa sehemu kubwa ya ardhi kwa wawekezaji kutoka nje na kuwasahau wananchi wakulima wadogo wadogo, wazawa wanaolizunguka eneo hilo wamebaki wakitangatanga kutafuta maeneo ya kufanyia kilimo.

Nitashukuru kusikia toka kwako, una mikakati gani juu ya hayo mambo machache niliyotaja na mengine ambayo sikutaja.
 
Mh.Regia unaonekana kuwa na agenda nzuri katika hayo mafanikio uliyoyaorodhesa lakini umeyaeleza kijumlajumla mno
 
Dada Regia kwanza nikupe hongera kwa kuamua kuorodhesha mambo uliyofanya kama mbunge. Wanaoweza ku-prove ukweli wa ulichoandika siyo mimi na baadhi ya wanaJF bali ni wanaKilombero wenyewe. Pamoja na hayo, nikushauri jambo moja kwamba kazi ya mbunge siyo kuwapatia wananchi samaki ingawa njia hiyo inaweza kusaidia kwa muda. Mimi nadhani wewe kama mbunge jitahidi sana kuwawezesha wananchi wako wapate nyavu na kisha wafundishwe namna ya kuvua samaki na namna ya kutunza nyavu na kuzifanyia
matengenezo. Ukienda kwa mwelekeo huo, utawaachia maendeleo endelevu na alama ya kudumu nyuma yako. Daima wananchi watakukumbuka kwa mchango wako. Ukiwapatia samaki (ada ya shule, mbolea, mahindi, n.k.) watawala hao samaki na baada ya muda mfupi wataanza kulia njaa tena na kusahau kabisa msaada wako.
 
Regia,

..according to Johnson Mbwambo wa gazeti la Raia mwema, kuna uharibifu mkubwa sana wa MAZINGIRA ktk maeneo ya bonde la mto KILOMBERO. vipi hili suala la MAZINGIRA umelishughulikia namna gani?

..kuhusu elimu naomba ujielekeze ktk kuhakikisha wanafunzi wa Kilombero wanapata elimu yenye viwango. msiridhike na kuandikisha watoto shule, au kuwalipia ada na karo. elekeza nguvu zako ktk kuhakikisha kwamba wanafunzi ktk jimbo lenu wanajifunza na kufanya vizuri ktk mitihani ya kitaifa.

..you r doing a great job, but I believe there is room for improvement.
 
Hongera sana Mkuu ni wabunge wengine nao waeleze jinsi walivyo fanya kazi majimboni mwao

Ila umesahau moja kuwa umefanikiwa pia kuhudhuria vikao vya bunge na vya chama au huwa huingii
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom