Niliyoyafanya tangu niwe Mbunge-Shukrani kwa WanaJF

Status
Not open for further replies.
hongera mama. usihofie changamoto na moto wa jf, dhahabu safi inahitaji moto haswaa kwa ajili ya kuwa refined. so, go mamaa, show them what u are made of!
all the best for 2012
 
Hongera sana Mungu akupe nguvu na afya tele .Kama umeweza kuweka kwa maandishi uliyowaongoza wananchi na kufanyika basi ni kumbukumbu nzuri na mwanzo mzuri .Naamini utafanya mengi zaidi na sisi tupo nyuma yako
 
mie avatar yako tu, lol!
afu hiyo request, kumbe Mtema ndo mbunge wako, hongera!:poa:focus:

Hongera mbunge wa viti maaalum. vipi kuhusu mkataba wa MOU uliwahi kuuliza swala hili bungeni? maana jamii ya kiislam huwa wanaulalamikia sana kwa kipindi kirefu. 2012 unaweza kumuuliza Mh waziri mKUU pINDA ktk maswala ya papo kwa papo?
 
Hongera sana dada. Natamani na rais wetu JK naye angejitathmini kama ulivyofanya wewe ili angalau tujue anasimama wapi kwa mwaka huu wa kwanza wa awamu yake ya pili kwenye ahadi zake tele alizotuahidi kwenye uchaguzi.
 
kwanza hongera kwa kazi zakon
imekuona ukiongea bungeni unajitahidi na unawatia moyo wengi hasa walemavu...
hongera saana kwa yote unayoyafanya...

but kazi za chama kitaifa ni kushiriki maandamano????????please.......
 
vipi mh. Hapo morogoro kuna mchango wa Tv IMANI. jee wewe kama mzaliwa na mBUNGE wa Mkoa wa Morogoro umechangia chochote kufanikisha? kwani huwa tunakuona ukichangia ktk kwaya mbali mbali.
naomba jibu mH mBUNGE


Eibara libi lita nyinaryo! ww kweli ni Malaria Sugu! tinkumanya enjae oligilekela maki!
 
Wakuu habari!

Ni matumani yangu kuwa tumejiandaa kumaliza mwaka vizuri na kuplan vizuri for next year.

Tukiwa tunafunga mwaka nimeona niandike kwa kifupi yale niliyoyafanya kwa kipindi Cha mwaka mmoja tangu kuapishwa kuwa Mbunge wa Vitimaalum Nov 12,2010.

Taarifa hii inaonyesha utekelezaji wa Kazi za Ubunge,Kazi za chama Wilayani Kilombero na Kazi za Chama Kitaifa.

A. KAZI ZA KIBUNGE
Tangu nimeapishwa nimefanikiwa kufanya Kazi mbalimbali za Kibunge Wilayani Kilombero,Jimbo ambalo niligombea na kupata Kura 38,550 sawa na asilimia 45 ya kura zote zilizopigwa. utekelezaji wa awamu hii ulikuwa ni QUICK WINS. Quick zifuatazo zimefanyika;
1. Nimepigania bei ya Sukari ishuke -Kuna maeneo Bei imeshuka lakini maeneo mengine hali bado ni mbaya. Kilombero ni Wilaya inayozalisha Sukari, Kiwanda Cha Illovo hivyo bei ya Sukari unapaswa kuwa chini kuliko maeneo yasiyodhalisha Sukari.
2. Nimepigania kituo Cha Polisi Cha Wilaya kiboreshwe-kimeboreshwa
3. Nimepigania kituo Cha afya Cha Mlimba kipatiwe Maji na Ambulance lirudishwe hivi vyote vimefanyika.Ambulance ilikuwa gereji zaidi ya miezi Sita mwaka 2010.
4. Nimepigania utekelezaji wa huduma bure kwa Wajawazito,Watoto chini ya Miaka Mitano,Wazee na Wenye Ulemavu-Kuna maeneo imefanikiwa maeneo mengi bado.
5. Nimetetea haki za Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Na KPL-Baadhi ya Kero zimetekelezwa lakini nyingine bado-Suala la Maslahi bado ni tete,suala la Usalama Kazini bado ni tete.
6. Nimetetea na kusimamia kero ya Wakulima na Wafanyabiashara ya kuongezeka kwa Ushuru bila kushirikishwa katika hatua zote muhimu.
7. Nimepigania haki ya Umeme kwa Wananchi wa Kilombero kwani tunavyanzo viwili ya umeme,Kihansi na Kidatu.REA imeenda kule ila inasua sua sana lakini Wizara imetuhakikishia kuwa inatekeleza azma yake ya kupeleka umeme maeneo yote ya karibu na vyanzo vya umeme.
8. Nimepigania barabara ya Kidatu-Ifakara kwa kiwango Cha lami-imeshindikana kwa mwaka wa fedha 2011-2012.
9. Nimesomesha Wanafunzi 86 Sekondari,13 Vyuo Vikuu hawa wa Vyuo Vikuu walihitaji kutoa advance ili waweze kusajiliwa then wapate Mkopo
10. Nimeezeka madarasa mawili(2) ya shule ya Msingi Mkula
11. Nimegharamia Visima viwili vya maji
12. Nimehudumia Baba aliyekuwa kipofu kwa miaka 8 akaweza kuona tena kupitia hospitali ya CCBRT
13. Nimesaidia wagonjwa wengine zaidi ya 42 wakapata huduma za afya na kupona
14. Nimesaidia Jezi kwa Vijana katika Kata 12 Kati ya 23 za Wilaya ya Kilombero
15. Nimefanikisha ligi Mbili katika Kata Mbili-Ligi za Mpira wa Miguu na Netboli
16. Nimeshiriki kwenye fundraising katika Misikiti 3 na Makanisa 4
17. Nimekuwa sehemu ya kufanikisha Uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishirki Cha Mt Fransisco
18. Nimeshiriki kuwasaidia Wahanga wa Mafuriko Wilayani Kilombero
19. Nimefanikisha Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kushirki Umitashumta ngazi ya Wilaya,Mkoa na Taifa
20. Nimefanikisha Vikundi Viwili vya kina Mama Wajane kuweza Kujiajiri na kuendesha maisha yao wenyewe.
21. Nimefanikisha Vikundi 5 vya kina mama kuweza Kujiajiri.
22. Nimefanikisha Vikundi 3 vya wenye ulemavu Kujiajiri wenyewe.
23. Nimefanya Mikutano ya Hadhara ya Elimu ya Uraia pamoja na Shukrani zaidi ya 20.

Na mengine madogo madogo mengi.

B. KAZI ZA CHAMA WILAYANI KILOMBERO

Katika kukuza chama Wilayani Kilombero nimefanikiwa kufanya yafuatayo;
1. Nimelipia na kufungua Ofisi za CHADEMA katika Kata 5
2. Nimefungua na Kuzindua Matawi 13 yaliyojengewa na yenye Uongozi wa Kudumu
3. Nimeingiza Wanachama zaidi ya 8,000

C. KAZI ZA CHAMA ZA KITAIFA
1. Nimeshiriki Maandamano ya CHADEMA Kanda ya Ziwa katika Mikoa yote ya Kanda hiyo katika kupigania haki za watanzania.
2. Nimeshiriki Maandamano ya CHADEMA Nyanda za Juu Kusini kasoro (Mikoa ya Iringa na Ruvuma) katika kupigania haki za watanzania.
3. Nimeshiriki kwenye Kazi za Siasa Arusha - Sakata la Kuvuliwa Uanachama Madiwani kusaka muafaka.
4. Nimeshiriki kwenye Uchaguzi Mdogo wa Igunga
5. Nimeshiriki kutoa Mafunzo ya Mapungufu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2011 katika Mkoa wa Ruvuma
6. Nimeshiriki kwenye Siasa za Vyuo Vikuu, Makongamano, Mikutano ya Hadhara na Uzinduzi wa Matawi
7. Nimeshiriki kwenye Siasa za Dodoma, Singida na Morogoro.

Natambua nilipaswa kuyafanya zaidi ya haya lakini kutokana na sababu mbalimbali hayo ndio niliyofanikiwa kuyafanya. Angalau nimefanikiwa kufanya karibu asilimia 70 ya niliyopanga kuyafanya kwa mwaka huu 2011 kama Mbunge wa Vitimaalum Wilayani Kilombero.

Naomba nichukue fursa hii pia kuwashukuru wanaJF wote kwa support yenu kwangu kwa hakika ninawashukuru sana tena sana.JF imekuwa ni nyumbani, JF imekuwa ni darasa, Vile vile JF imekuwa ni Tanuru la Moto maana wakati mwingine huwa ninaingizwa kwenye moto hasa. Na mwisho nichukue fursa hii kuwaomba radhi wale wote niliowakwaza kwa namna moja ama nyingine, tuanze upya mwaka ujao..

With Love
Regia

Hongera saaana RM, keep it up!! ila hapo kwenye red duh uko siriazi? well next year jitahidi ukimbie kambi ya makapera ndani ya CDM maana siku hazigandi and nobody is getting any younger!! otherwise kazi nzuri na endelea hivyo hivyo. ila umesahu jambo moja la kiungwana saana ulilofanya bungeni. nafikiri unalikumbuka. much respect!
 
mbunge yeyote wa cdm ni mbunge wangu,hongera sana mbunge wangu lini sasa utakuja kutujulia hali huku jimbo la uchaguzi la mwibara .
 
Japo kuwa mie si mzuri sana katiika siasa ila taarifa hii imekaa katika sura ya kujitafutia ujiko zaidi kuliko kuonesha tangible results, kwa mfano M/kiti wa CCM anaweza kusema serikali imejitahidi kwa hali na mali kuwasaidia waathirika wa mafuriko Dsm ili waweze kurejea katika hali yao ya kawaida na bado bado juhudi hizi zinaendelea - tumeona kambi na viwanja vya Mabwe Pande. Hakuna atakaeuliza swali, sasa wewe mh. sana kama ulifanya yote hayo naomba unisaidie yafuatayo:

1. Hapo hakuna mbunge alieshinda?
2. Hakuna baraza la madiwani?
3. Hakuna Mwenyekiti wa hilo baraza?
4. Hakuna Mkurugenzi wa hiyo wilaya?
5. Hakuna Mkuu wa wilaya na mkoa?
6. Hakuna watendaji wengine wa eneo hilo?
Kama wapo basi utueleza wanafanya kazi gani wakati wewe ukichukua ujiko mkubwa namna hii?
 
Japo kuwa mie si mzuri sana katiika siasa ila taarifa hii imekaa katika sura ya kujitafutia ujiko zaidi kuliko kuonesha tangible results, kwa mfano M/kiti wa CCM anaweza kusema serikali imejitahidi kwa hali na mali kuwasaidia waathirika wa mafuriko Dsm ili waweze kurejea katika hali yao ya kawaida na bado bado juhudi hizi zinaendelea - tumeona kambi na viwanja vya Mabwe Pande. Hakuna atakaeuliza swali, sasa wewe mh. sana kama ulifanya yote hayo naomba unisaidie yafuatayo:

1. Hapo hakuna mbunge alieshinda?
2. Hakuna baraza la madiwani?
3. Hakuna Mwenyekiti wa hilo baraza?
4. Hakuna Mkurugenzi wa hiyo wilaya?
5. Hakuna Mkuu wa wilaya na mkoa?
6. Hakuna watendaji wengine wa eneo hilo?
Kama wapo basi utueleza wanafanya kazi gani wakati wewe ukichukua ujiko mkubwa namna hii?

Wakati mwingine hua tunasahau kwamba mafanikio tuliyofikia hatukufanikisha wenyewe, japo tunaweza tukawa tumehusika kwa kiasi kikubwa. Kila mtu yupo kujipamba yeye mwenyewe, wengine nao watajijua wenyewe.
 
Baada ya kupata pongezi nyingi lazima changamoto nazo uwe unazikubali maana mtaaluma mmoja alisema "We learn nothing from success but from failures and challenges" so usilewe na sifa, haya angeandika wa CCM ndo ungeona watu walivo wanafiki. Mi sina chama ila,

- threads za ongezeko la posho na kufutwa kwa viti maalum ili kupunguza matumizi yasiyo na tija mbona huwa uonekani, nini msimamo wako ktk hayo?
 
Regia umeonyesha mfano mzuri given the fact that upo kwenye ubunge for only a year vs wengine ambao wako kwa muda mrefu zaidi ie more than a decade, lakini they never bother to put down what the have achieved during the period...

Pia the fact kwamba wewe ni member wa JF uliyeupata ubunge mara baada ya wengi humu kukubali hoja zako nyingi.

Nimefurahishwa na the fact that bado wewe ni mwana JF damu, kwasababu this is JF's way...Tuonyeshe ulichowafanyia wananchi, keep it up and hopefully kabla ya uchaguzi ujao utafanya mengi zaidi na hivyo kuchakachulliwa iwe shida zaidi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom