Nilitegemea Mawaziri hawa kufikishwa Mahakamani!

Mjomba wa taifa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
231
161
Ikumbukwe hivi karibuni, Rais Kikwete alipangua baraza la Mawaziri kufuatia shinikizo la wabunge kutokana na ubadhilifu wa mali ya umma. Miongoni mwa Mawaziri/Naibu waliopoteza nafasi zao ni pamoja na Mustafa Mkulo, William Ngeleja, Omar Nundu, Ezekieli Maige, Cyril Chami, Haji Mponda na Lucy Nkya.

Mawaziri hawa hawakuondolewa madarakani kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao bali Kutumia madaraka yao kuiba rasilimali za nchi. Ikiwemo kuuza Twiga (Wizara ya Maliasili), Kuuza viwanja vya umma (Wizara ya fedha) n.k.

Hivi ni kwanini mpaka leo watu hawa hawajafikishwa Mahakamani either wasafishwe kwa tuhuma hizo ama wapewe adhabu stahili. Licha ya kuwepo kwa mashaka ya kesi za viongozi wanapofikishwa mahakamani kuchukua muda mrefu kutolewa hukumu lakini bado wananchi wangerudisha imani iliyopotea kwa serikali hata kwa kuona viongozi wabadhilifu hawaishii tu kuondolewa madarakani bali kufikishwa mahakamani.
 
umenena mkuu, tusubiri tuone coz majuzi itv hosea alisema kuna watu wanawachunguza, may b hao ni miongoni
 
Kikwete ndo mwisho wake wa kufikiri hapo,huwa wanafanya mambo kwa kuogopa hasira za wananchi,hawawezi kuchukuliana hatua,lao moja,na wabunge wetu nao wamefumbwa macho!
 
labda wapate shinikizo kama lile la kutaka waondoleo kinyume na hapo mchezo umeishia hapo. hakuna cha kuchunguzwa wala mahakamani full kulindwa.
 
Ikumbukwe hivi karibuni, Rais Kikwete alipangua baraza la Mawaziri kufuatia shinikizo la wabunge kutokana na ubadhilifu wa mali ya umma. Miongoni mwa Mawaziri/Naibu waliopoteza nafasi zao ni pamoja na Mustafa Mkulo, William Ngeleja, Omar Nundu, Ezekieli Maige, Cyril Chami, Haji Mponda na Lucy Nkya.

Mawaziri hawa hawakuondolewa madarakani kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao bali Kutumia madaraka yao kuiba rasilimali za nchi. Ikiwemo kuuza Twiga (Wizara ya Maliasili), Kuuza viwanja vya umma (Wizara ya fedha) n.k.

Hivi ni kwanini mpaka leo watu hawa hawajafikishwa Mahakamani either wasafishwe kwa tuhuma hizo ama wapewe adhabu stahili. Licha ya kuwepo kwa mashaka ya kesi za viongozi wanapofikishwa mahakamani kuchukua muda mrefu kutolewa hukumu lakini bado wananchi wangerudisha imani iliyopotea kwa serikali hata kwa kuona viongozi wabadhilifu hawaishii tu kuondolewa madarakani bali kufikishwa mahakamani.

Hao wawili sidhani kama wana tuhuma kama hizo.
 
umenena mkuu, tusubiri tuone coz majuzi itv hosea alisema kuna watu wanawachunguza, may b hao ni miongoni
mambo ya kupeleka mahakamani watu wakubwa yanatoka wapi???. hii siyo sera ya chama. kama wana makosa tutawaonya kwenye vikao vya ndani vya chama. wengine hayawahusu kunani kyawafuatilia hayo? s
 
umenena mkuu, tusubiri tuone coz majuzi itv hosea alisema kuna watu wanawachunguza, may b hao ni miongoni
hosea alikwisha poteza moral authority tangu aisafishe richmond!, binafsi simwamini kabsaaaa!
 
umenena mkuu, tusubiri tuone coz majuzi itv hosea alisema kuna watu wanawachunguza, may b hao ni miongoni
Hiyo ni lugha iliyozoeleka hapa kwetu..........serikali ipo ktk mchakato.............upembuzi yakinifu unafanywa....., serikali sikivu inaliaangalia jambo hili..........., CHADEMA wanataka nchi isitawalike..........., tume maalumu imeundwa kufuatilia jambo hili............., waziri mwenye mamlaka...............!!!!!!!!!!!!!!1
 
Back
Top Bottom