Nilipomtafuta alikuwa bize nimekata kamba anataka tuonane

mambo ya mapenzi bana ......sasa hapo unataka ushauri wa nn au ili ukamwambie jf walinishauri nikuache?
tupa kureee huyo ,au oa ufe kwa stress.
 
Alikua na jamaa, wewe ulikua backup plan, nafikiri main server imecolapse anakutafuta wewe, believe me that hiyo sever itarudi na atakutosa tena HAKUFAI.

Ndugu zangu habari zenu. Poleni na majukumu ya hapa na pale.
Leo ninaona niwafahamishe jambo lililonitokea.

Katika harakati za kutafuta mwenza wa maisha (mke) nilikutana na binti fulani ambae nilimpenda na nilitaka kumwoa nilifanya taratibu za kumweleza na alikubali tukaendelea ktk uchumba. Miezi sita baadae mawasiliano yakawa magumu nilikuwa nikipiga simu haipatikani na ikipatikana inaita bila kupokelewa kwa muda kama wa siku tatu. Baadae ya muda huo alinipigia simu kwa namba nyingine na kunijulisha kuwa ile namba aliyokuwa anaitumia hapo mwanzo haikuwa yake bali ni ya kaka yake (wa hiari) ambae anaishi nae, huyo kaka yake ameoa na anaishi na mkewe pia. So kuanzia hapo nikawa natumia namba simu mpya niliyopewa na huyo binti lakini baada ya miezi miwili hali ilijirudia tena, kila nikipiga simu inaita bila kupokelewa hata kwa siku nzima akipokea simu nikimuuliza anasema aliiacha nyumbani kwa vile kazini yuko bize. Nikimuuliza kuhusu mpango wetu wa kuoana anasema tutapanga muda tukutane na tukipanga appointment haji na simu inaita tu bila kupokelewa au haipatikani.

Nilipoona mwenzangu yuko bize nikaona isiwe tabu nikawa naenda hadi kazini ili tuongelee huko huko nikifika naambiwa kuna kazi. Nikaona isiwe tabu nikawa namwambia kuwa ni vizuri tukaweka mipango kwa ajili ya posa baadae kutoa mahari coz kwa kipindi hicho vijisent vya mahari nilikuwa nimevikusanya vipo tayari na nilikuwa naogopa kuvitumia. Kwa sababu tulishindwa kuonana physically nikamwambia tuongee kwenye simu akakataa na kusema hatuwezi kuongelea kwenye simu jambo hilo, yaani kila nililojaribu kulifanya ili tuongee nilishindwa... nakumbuka jumapili moja tulipanga tukutane ili tuongee yule binti alikuja na wadogo zake watatu akasema asingeweza kuwaacha nyumbani pekee yao kwa hiyo siku hiyo ikashindika

Baada ya juhudi kushindwa nilimwambia mama mmoja ambae ndio alituunganisha, nikamwambia hali halisi na nikamwomba akutane na binti ili aongee nae lakini yule binti alishindwa kuonana na huyo mama. walipanga appointment mara tatu bila mafanikio binti yuko bize sana. Nilikuwa nikiongea nae kwa njia simu lakini hataki kuongelea issue kwenye simu.

Kwa kweli uzlendo ulinishinda nikaamua kujivua gamba. siku ya valentines (2012) niliona niitumie kumwambia kuwa sitaweza kuendelea nae tena. nilimpigia simu tangu asubuhi hadi saa nne usiku bila kupokelewa ndipo nilipoamua kuandika ujumbe wa kuvunja uchumba wetu.

Jambo linalonishangaza ni kwamba binti amerudi kwa kasi sana. Anamsumbua yule mama kuwa mimi sikumpa yeye nafasi ya kujitetea ila niliamua kuvunja uchumba bila kumsikiliza yeye ana tatizo gani, nazidi kushangaa kwa sababu mimi hanipigii simu bali anampigia yule mama simu akimuuliza tumefikia wapi kuhusu suala hili... ni wiki mbili sasa anamsumbua huyu mama ili atukutanishe pamoja, sasa najiuliza kwa nini hanipigii wakati namba yangu anayo? mie nikimpigia kwa nini hapokei?

Duh kweli nimeshindwa kumwelewa kipindi kile nilichokuwa namtafuta alikuwa kweli yuko bize au alikuwa anatikisa kiberiti aone kama kuna njiti?

Naombeni maoni yenu katika hili
 
Na mimi naungana na wengine achana nae huyo.

Mbona mabinti wako wengi tu tena wazuri wazuri na heshima zao, ya nini kushupalia hapo ambapo kwa hii leo panaonyesha hapana manufaa ya baadae?

Mfano, jaribu kupiga simu kwa ile namba ya zamani na ujitambulishe kama rafiki yake na unamtafuta. Halafu sikiliza mshindo utakuwaje? Unaweza ukakuta hiyo namba ni ya husband!
 
Usikute yupo kwenye dozi!
Ushauri:
  1. Kama unampenda kutana naye umsikilize
  2. Kama humpendi basi usipoteze muda, ndoa si kitu cha mzaha. Unaweza kuoa mchawi akakusumbua.
  3. Otherwise usije ukatolewa kafala.
 
ndo matatizo ya wapenzi wa 'kuunganishiwa'
ila inaelekea una haraka ya kuoa, je huyo binti unampenda kwa dhati? Unamjua kiundani? Unajua udhaifu wake na umeukubali? Anakujua vyema? Maana inaonekana kama hamjuani kivile.......

Take tame kwanza.......
Tuliza kichwa...
Jipe muda......

Asante sana ndugu yangu kwa ushauri wako.
Ninaposema kuunganishiwa ninamaanisha kuwa kwa huyo mama ilikuwa ni sehem ambayo tuliamua kuwa tunakutania.. hizo ni taratibu tulizojipangia kuwa tusikutane popote.
Nakuhusu kufahamiana tulikuwa tunafahamiana kwa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kuanzia hiyo safari na hiyo miezi sita baadae ninayoisema ni baada ya kuamua kuwa wachumba. Sio kwamba simfaham bali namfahamu japo sio saaana nae pia ananifahamu kwa sehemu.

Thanks
 
Kaka inaelekea uko desparate na ndoa sana. Haraka haraka hizi ndo huwa zinawaponza watu. Kaa utulie utafute mwanamke aliyetulia na mwenye moyo na wewe. Otherwise utajilaumu baada ya ndoa.

Kwa story nilivyoo-ielewa ni kwamba unaharaka sana na ndoa. Kaka hizo ni pingu za maisha. So tulia kwanza. Huyo mwanamke amewapanga kama nyie wengi. Ndo maana yuko busy hivyo

Asante ndugu
Jambo la kuwekwa kwenye waiting list ndo linaleta taabu. so ntaendelea kuwa kwenye waiting list hadi lini? mie nataka kuwa first eleven.
Thanks
 
mambo ya mapenzi bana ......sasa hapo unataka ushauri wa nn au ili ukamwambie jf walinishauri nikuache?
tupa kureee huyo ,au oa ufe kwa stress.

Ndugu asante...... lakini kwenye mambo kama haya ushauri ni wa muhimu.
Teh teh teh hapo kwenye red umenichekesha kweli coz hata haijui hiyo JF ni kitu gani....
thanks once again
 
Na mimi naungana na wengine achana nae huyo.

Mbona mabinti wako wengi tu tena wazuri wazuri na heshima zao, ya nini kushupalia hapo ambapo kwa hii leo panaonyesha hapana manufaa ya baadae?

Mfano, jaribu kupiga simu kwa ile namba ya zamani na ujitambulishe kama rafiki yake na unamtafuta. Halafu sikiliza mshindo utakuwaje? Unaweza ukakuta hiyo namba ni ya husband!

Kama ulikuwepo.
Kuna mtu mmoja aliwahi kupiga hiyo namba niliyoambiwa kuwa ni ya kaka akatukanwa kwa nini anamfuatilia mke wa mtu, kwa hiyo huyo jamaa mwenye hiyo namba alijitambulisha kuwa yeye ndo mume wa huyo binti.
Nilizipata hizo taarifa nikazifuatilia ila sikupata uhakika kuhusu hilo ila jambo ninalokumbuka ni kwamba kuana watu walikuwa wanawasiliana na huyo binti kwa kupitia namba ambayo mimi niliambiwa ni ya kaka lakini watu wengine wakipiga wanampata huyo msichana na wanaongea nae. Niliwahi kuweka mtego siku moja kuhusu matumizi ya hiyo namba nikamwambia huyo mama ampigie coz yule mama hakujua kama binti amebadilisha namba, tukiwa wote yule mama alipga simu na yule binti akpokea, ni kuanzia hapo nilianza kuhisi vibaya japo sikusema

Nakushukuru kwa ushauri wako
 
Aisay una speed kali sana, yani wewe unataka kuoa mwanamke hata humjui vizuri.

Aisay wewe umeshinda, congrats.

Thanks
Ni jambo la maamuzi tu ndugu yangu mbona watu wanakutanaga for the first time na wanaenda on bed the same day!!!!!
Anyways thanks alot
 
Kwanza umeniumiza kama kaka wa kuzaliwa, ulivyokua unamfuatilia msichana hivyo ingawa dalili zote kua hakutaki zlikua anakuaonyesha.

Kakaangu ndoa sio maigizo, na mapenzi yanatakiwa ya balance sio wewe upende tu halafu yeye hakupendi, ki ukweli huyo dada hutakiwi hata kumpa mda kwani sio wako, na ukimuoa utajuta sana baadae kwani hata kaa akuheshim na ukigombana nae tu kidogo atakua anakwambia kwanza mi sikukupenda ulinilazimishia kuolewa na wewe.

Na kitendo cha kuja na wadogo zake kwenye maongezi yenu ya muhim nitosha kabisa hakuhitaji, pia kua busy kila wakati ni picha kamili kua hakupendi uanamfwatafwata, najinsi waschana tulivyo ukute hata ofisini kwao ilikua ukienda anawambia lile lijinga limekuja tena kunisumbua yani silipendi, wanakuchungulia madilishani wanacheka.

Achana nae kabisa ndugu yangu la sivyo atakuja kukuumiza sana mbeleni, na wala usidhani alikua anatikisa kiberiti hapana, jibu ni kwamba hakupendi tena hakupendi kabisaaa, uamuzi niwako lakini.
 
Nakushukuru dada yangu kwa ushauri huo
 
hata mimi mmenisaidia coz namimi nipo katika harakati hizo najiona namimi nahusika kwenye hili....
Nafikri kwangu na huyo alieanzisha hii hoja tumenufaika vya kutosha yaani mie mmenifungua macho sana nawashukuru asanteni.
Ndugu yangu umeelewa hayo walioyasema wewe ulieleta hoja? chukua ushauri huo utakusaidia
 
Asante tupo pamoja ndugu yangu. hayo ndo maisha
 
Kwanza umeniumiza kama kaka wa kuzaliwa, ulivyokua unamfuatilia msichana hivyo ingawa dalili zote kua hakutaki zlikua anakuaonyesha.

Kakaangu ndoa sio maigizo, na mapenzi yanatakiwa ya balance sio wewe upende tu halafu yeye hakupendi, ki ukweli huyo dada hutakiwi hata kumpa mda kwani sio wako, na ukimuoa utajuta sana baadae kwani hata kaa akuheshim na ukigombana nae tu kidogo atakua anakwambia kwanza mi sikukupenda ulinilazimishia kuolewa na wewe.

Na kitendo cha kuja na wadogo zake kwenye maongezi yenu ya muhim nitosha kabisa hakuhitaji, pia kua busy kila wakati ni picha kamili kua hakupendi uanamfwatafwata, najinsi waschana tulivyo ukute hata ofisini kwao ilikua ukienda anawambia lile lijinga limekuja tena kunisumbua yani silipendi, wanakuchungulia madilishani wanacheka.

Achana nae kabisa ndugu yangu la sivyo atakuja kukuumiza sana mbeleni, na wala usidhani alikua anatikisa kiberiti hapana, jibu ni kwamba hakupendi tena hakupendi kabisaaa, uamuzi niwako lakini.

Ndugu uanjua sisi wengine tupo serious kwenye jambo hili na sipendi kumchezea mtu. Huyu msichana kweli nilimpenda ndo maana usumufu huo mie niliona jambo la kukabiliana nalo kiume kwani lengo langu nilihitaji kuwa nae toka moyoni
Kwangu ndoa ni jambo ambalo nataka nilifanye so nilimfuatilia coz nilimpenda sana sana.
Nakushukuru kwa concern yako

Thanks
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom