Nilipomtafuta alikuwa bize nimekata kamba anataka tuonane

Fmewa

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
292
81
Ndugu zangu habari zenu. Poleni na majukumu ya hapa na pale.
Leo ninaona niwafahamishe jambo lililonitokea.

Katika harakati za kutafuta mwenza wa maisha (mke) nilikutana na binti fulani ambae nilimpenda na nilitaka kumwoa nilifanya taratibu za kumweleza na alikubali tukaendelea ktk uchumba. Miezi sita baadae mawasiliano yakawa magumu nilikuwa nikipiga simu haipatikani na ikipatikana inaita bila kupokelewa kwa muda kama wa siku tatu. Baadae ya muda huo alinipigia simu kwa namba nyingine na kunijulisha kuwa ile namba aliyokuwa anaitumia hapo mwanzo haikuwa yake bali ni ya kaka yake (wa hiari) ambae anaishi nae, huyo kaka yake ameoa na anaishi na mkewe pia. So kuanzia hapo nikawa natumia namba simu mpya niliyopewa na huyo binti lakini baada ya miezi miwili hali ilijirudia tena, kila nikipiga simu inaita bila kupokelewa hata kwa siku nzima akipokea simu nikimuuliza anasema aliiacha nyumbani kwa vile kazini yuko bize. Nikimuuliza kuhusu mpango wetu wa kuoana anasema tutapanga muda tukutane na tukipanga appointment haji na simu inaita tu bila kupokelewa au haipatikani.

Nilipoona mwenzangu yuko bize nikaona isiwe tabu nikawa naenda hadi kazini ili tuongelee huko huko nikifika naambiwa kuna kazi. Nikaona isiwe tabu nikawa namwambia kuwa ni vizuri tukaweka mipango kwa ajili ya posa baadae kutoa mahari coz kwa kipindi hicho vijisent vya mahari nilikuwa nimevikusanya vipo tayari na nilikuwa naogopa kuvitumia. Kwa sababu tulishindwa kuonana physically nikamwambia tuongee kwenye simu akakataa na kusema hatuwezi kuongelea kwenye simu jambo hilo, yaani kila nililojaribu kulifanya ili tuongee nilishindwa... nakumbuka jumapili moja tulipanga tukutane ili tuongee yule binti alikuja na wadogo zake watatu akasema asingeweza kuwaacha nyumbani pekee yao kwa hiyo siku hiyo ikashindika

Baada ya juhudi kushindwa nilimwambia mama mmoja ambae ndio alituunganisha, nikamwambia hali halisi na nikamwomba akutane na binti ili aongee nae lakini yule binti alishindwa kuonana na huyo mama. walipanga appointment mara tatu bila mafanikio binti yuko bize sana. Nilikuwa nikiongea nae kwa njia simu lakini hataki kuongelea issue kwenye simu.

Kwa kweli uzlendo ulinishinda nikaamua kujivua gamba. siku ya valentines (2012) niliona niitumie kumwambia kuwa sitaweza kuendelea nae tena. nilimpigia simu tangu asubuhi hadi saa nne usiku bila kupokelewa ndipo nilipoamua kuandika ujumbe wa kuvunja uchumba wetu.

Jambo linalonishangaza ni kwamba binti amerudi kwa kasi sana. Anamsumbua yule mama kuwa mimi sikumpa yeye nafasi ya kujitetea ila niliamua kuvunja uchumba bila kumsikiliza yeye ana tatizo gani, nazidi kushangaa kwa sababu mimi hanipigii simu bali anampigia yule mama simu akimuuliza tumefikia wapi kuhusu suala hili... ni wiki mbili sasa anamsumbua huyu mama ili atukutanishe pamoja, sasa najiuliza kwa nini hanipigii wakati namba yangu anayo? mie nikimpigia kwa nini hapokei?

Duh kweli nimeshindwa kumwelewa kipindi kile nilichokuwa namtafuta alikuwa kweli yuko bize au alikuwa anatikisa kiberiti aone kama kuna njiti?

Naombeni maoni yenu katika hili
 
Kaka inaelekea uko desparate na ndoa sana. Haraka haraka hizi ndo huwa zinawaponza watu. Kaa utulie utafute mwanamke aliyetulia na mwenye moyo na wewe. Otherwise utajilaumu baada ya ndoa.

Kwa story nilivyoo-ielewa ni kwamba unaharaka sana na ndoa. Kaka hizo ni pingu za maisha. So tulia kwanza. Huyo mwanamke amewapanga kama nyie wengi. Ndo maana yuko busy hivyo
 
Ndugu zangu habari zenu. Poleni na majukumu ya hapa na pale.
Leo ninaona niwafahamishe jambo lililonitokea.

Katika harakati za kutafuta mwenza wa maisha (mke) nilikutana na binti fulani ambae nilimpenda na nilitaka kumwoa nilifanya taratibu za kumweleza na alikubali tukaendelea ktk uchumba. Miezi sita baadae mawasiliano yakawa magumu nilikuwa nikipiga simu haipatikani na ikipatikana inaita bila kupokelewa kwa muda kama wa siku tatu. Baadae ya muda huo alinipigia simu kwa namba nyingine na kunijulisha kuwa ile namba aliyokuwa anaitumia hapo mwanzo haikuwa yake bali ni ya kaka yake (wa hiari) ambae anaishi nae, huyo kaka yake ameoa na anaishi na mkewe pia. So kuanzia hapo nikawa natumia namba simu mpya niliyopewa na huyo binti lakini baada ya miezi miwili hali ilijirudia tena, kila nikipiga simu inaita bila kupokelewa hata kwa siku nzima akipokea simu nikimuuliza anasema aliiacha nyumbani kwa vile kazini yuko bize. Nikimuuliza kuhusu mpango wetu wa kuoana anasema tutapanga muda tukutane na tukipanga appointment haji na simu inaita tu bila kupokelewa au haipatikani.

Hapo penye red pamenipa wasiwasi kidogo, kuishi na kaka wa hiari, hivi hivi tu? Anyway, jaribu kumpa muda huku ukiendelea na uchunguzi inaweza kukusaidia kuupata ukweli wa kuwa alikuwa anatikisa kiberiti au la!
 
Kaka mkubwa kwa jinsi hali ilivyo inaonyesha wazi vitu muhimu utakavyovihitaji kufanya maamuzi kuhusu huyo dada hunavyo
(What I mean is there is a lot more going on than what you see there)
a) Fuata ushauri wa mdau m1 hapo juu. Tuliza haraka za ndoa isije ikakucost(hela za mahari weka hata kwenye fixed account bank).
b) Mchunguze huyo dada kwa hali ya juu sanaaa! coz nnaamini kuna vitu anakuficha kuhusu anapokaa, kama yuko kwenye uhusiano na wewe tu ama kuna mwingine?, kama yuko tayari kwa ndoa? na kama yuko tayari, Je ni yeye mwenyewe anaweza kujiamulia au ana wasiwasi kuna watu hawatakubali?

Yani kwa kifupi hapo kuna mambo mengi usiyoyajua kuhusu huyo mdada....
 
Mkuu huyo sio wako. Amini ninachokuambia, nyota njema huonekana asubui. Tafuta wife materially, sio huyo kaka. Kwenye swala la mapenzi ya ukweli hakunaga ubize kiasi kwamba mtakosa nafasi ya kupanga mambo yenu!. Afu acha wenge la ndoa! We unampenda bint na kumtangazia ndoa right on the spot!! Hujawahi kuwa na mahusiano tena kabla Mkuu??
 
ndo matatizo ya wapenzi wa 'kuunganishiwa'
ila inaelekea una haraka ya kuoa, je huyo binti unampenda kwa dhati? Unamjua kiundani? Unajua udhaifu wake na umeukubali? Anakujua vyema? Maana inaonekana kama hamjuani kivile.......

Take tame kwanza.......
Tuliza kichwa...
Jipe muda......
 
Maneno mengi yanapoteza muda,kwa sentensi moja tu,achana na huko,tulia then anza kutafuta taratiiibu utapata tu amini usiamini...usimwazie sana kwani atakufanya akili yako ishindwe kurudi fresh na kujipanga vizuri upya

For ur information,hata mie binafsi natafuta ila tunatakiwa kutulia huku ukitenga mda mrefu wa kutosha hadi umpate,slow but sure!
 
Wanawake siku hizi ni wajanja sana.Anakua na wanaume kama saba hivi then anachagua.kigezo chao cha kwanza kwenye kuchagua hua ni uwezo wa mtu kifedha.Akiona yule mwenye hela kama haeleweki eleweki hivi hamuachii, anaendelea kula pesa yake huku anashikilia upande mwingine ambao unaonekana kua na nia ya kuchukua jumla.Kwa ufupi wanashindwa kua wakweli kwa kuogopa kukosa vyote.

Mi nakushauri uachane na huyo binti na tafuta ambaye yuko serious.Utakayempenda na mtakayependana.Huyo atakuja kukusumbua sana baadae, believe me.
 
Mmmh kaka nadhani wengi wamekupa ushauri unaofaa, huyo dada atakupasua kichwa kama ukimuoa, maana sahizi tu kichwa kinakuuma je ukioa? Temana nae mkuu, kisa cha kujitaftia presha na vidonda vyatumbo ni nini??
 
Kwa maelezo yako hamkua pamoja.

Na hukuwa na utaratibu mzuri wa kumtambua mwenzio

Sasa hapo pameharibika ,

Sema na moyo wako juu ya huyo dada ukishapata majibu uyasimamie
 
Asee wewe ni m/ume wa tofauti sana!pamoja na vimbwanga vyote hivyo bado unamuwaza??ndo mpenz wako wa kwanza au??inakuaje unataka kumtolea posa m2 ambae hufaham hata kwao?ubusy gani huo wa kutopokea simu cku 3?kwani yeye mkuu wa nchi?kwa nini asikutafute wewe ampigie huyo mam?amka ucngizini kaka huyo dada HAKUFAI!! Huitaji degree kulijua hilo
 
usimuache endelea kumega huku unatafuta mwingine. mtumie kama anavyokutumia kuumiza kichwa chako.
 
Acha ushamba mapenzi ya kizamani hayo, unamhangaikia demu kama unatafuta kazi vile, kwa nini?
Piga chini au vipi akijichanganya mpige pumbu kiujanjaujanja (asikushike tena masikio, utajuta!) huku ukitafuta mke wa ukweli, huyo sio mke ni mwanamke
 
Huyo alikuwa na mpango wa kando sasa kaona jamaa haeleweki ndo amekukumbuka wewe.Kama angekuwa anakupenda sms yako ya kuvunja uchumba ingemuuma na kukutafuta kwa hali na mali muyazungumze.Huyo hana msimamo atakusumbua yamemchachia huko anataka ayapozee kwako.TUPA KULE KWANI NIN BWANA?
 
Kwa kifupi na straight huyo binti hakufai kabisa. Hata ukifanikiwa kumuoa jua basi ndoa yako haitadumu maana ni kama binti alikuwa hakuhitaji.

Halafu ndoa so kama ukiwa na hela ya kununua gari basi unakuwa na kasi kihivyo utaambulia koroma.
 
Aisay una speed kali sana, yani wewe unataka kuoa mwanamke hata humjui vizuri.

Aisay wewe umeshinda, congrats.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom