Nilipokuwa darasa la pili nilitongoza nikatapeliwa

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
614
Unaweza usiamini ila ndiyo ukweli, nilipokuwa darasa la pili, siku moja nilimbembeleza mtoto mmoja ambaye naye alikuwa darasa la pili ili aniachie ngoma, haikuwa tabu kwani aliniambia kama nitampa senti hamsini haitakuwa shida, kwa kuwa pesa hiyo sikuwa nayo ilibidi niende kuchota kahawa ya mama na kwenda kuiuza dukani ambapo nilipewa kama shilingi moja, hivyo nilimlia timing yule demu na kumkabidhi senti hamsini alizohitaji, aliniahidi kuwa nitangulie kwenye kichaka fulani then atatia timu, nilikaa pale kwa masaa kadhaa mpaka nilipoona usiku unaingia ikabidi nirudi home huku nikiwa siamini kilichotokea, kesho kwa bahati nilimuona na kumuuliza mbona hakuja? aliruka kimanga na kuniambia hela niliyompa haitoshi, jambo lililofanya nimuongeze sent 50 nyingine, baada ya kumpa hiyo sikumuuona tena hadi baada ya siku kama 2 ambapo nilipomhoji akaniambia nimkome. Nilimhakikishia kuwa kama ameshindwa lazima atarudisha hela yangu, baada ya juhudi zote za kudai hela yangu kugonga mwamba siku moja usiku nikatia timu kwao, kwa bahati nilimkuta akiwa na mama yake na hapo nilimweleza kuwa naomba anirudishie hela yangu baada ya mzozo aliingia ndani na kunitolea sh. 1 na hapo nikarudi nyumbani kwa amani.
 
Aisee we sio mchezo alikugwaya mbele ya mama yake sijui angeulizwa aliichukua kwasababu gani angesemaje?
 
Da umenikumbusha mbali sana mkuu, mimi nikiwa darasa la sita nilikuwa mara yangu ya kwanza kutongoza, ilikuwa ishu yaani sitakaa ni sahau.
Nilimuelezea rafikia yangu basi tukakaa chini tukaandika barua kwenye daftari, sikuchana lile karatasi ili nikirudi nyumbani niombe pesa ya kalamu halafu nibadilishe ninunue bahasha niiweke ile barua, nilipofika nyumbani mama kaniambia nimletee madaftari akague kufungua akaanza kutoa daftari la hesabu akaanza kukagua kufika katikati akakutana na barua niliomuandika yule demu, na ilikuwa noma siku hiyo, nikakimbia sikula hata lunch nikarudi jioni na majani ya kuku, kuua soo lakini wapi bado nilichezea kichapo.
 
Miaka 11?? Bado hawezi kutongoza kama yeye! Tena enzi za senti 50??? Labda useme alianza akiwa na miaka 15!! Wengine senti 50 tumezionea kwenye vitabu vya Hisabati. Class 1 anatongoza??? Labda kweli.
Inaelekea ulianza Class 1 ukiwa na miaka kumi na moja baada ya mkono wa kulia kuweza kugusa bega la kushoto kupitia juu ya kichwa.
 
Duh! Nimecheka mpaka nimepaliwa! We jamaa ni kiwembe. Mbona ulianza mapema sana mkuu?
 
Du.. umekomaa mpaka pesa yako karudisha, lakini saizi najua umeshatapeliwa sana lakini uwezi kukomaa tena:hurt:
 
Back
Top Bottom