Nilimuamkia mngoni nikakoma .

mtani sooo ulifika mpaka pande za kumpitimbi! hongera sana mtani ukija safari nyingine nitafute nipo kijiji kinachofuta bada ya mpitimbi. utakuta tumekutayarishia pombe inaitwa MYAKAYA brewed using mayau (mihogo). msosi utakuta ugali na namgujulu(mboga ya manyonyoli) utauliza huko huko manyonyoli ndo nini. matunda mtani yapo ya kumwaga kuna masuku, madonga, machungwa mapapai mapwete mpaka hapo mtani nadhani utaridhika na kuomba upewe mdala(mchumba) wa kugega(kuoa) hahahaaaa

Duh! Mkuu umenikumbusha mbali sana! Hivyo vitu tulikuwa tunavipata enzi hizo tukiwa JKT Mlale. Kuna kijiji kimoja kinaitwa Lusonga nilipata 'mdala wa kugega'.
 
Hii imenikumbusha ugomvi mkubwa uliotokea kati ya dreva moja mwenyeji wa mikoa ya bara na mngoni moja. Ni kwamba mngoni alitoka hospitalini yeye mkewe na mtoto mdogo njialikapita lori likiwa na dreva na utingo wake. Kwa kumhurumia mama na mtoto utingo alimpisha sehemu ya mbele yeye akapanda nyuma pamoja na jamaa wa kingoni. Baada ya kuwafikisha sehemu walikuwa wakienda baada ya kuteremka chini yule mngoni kwa nia nzuri kabisa alikwenda kumshukuru dreva kwa msaada aliowapa .Tatizo lilikuwa kwenye matamshi yake ambayo yalitafsiriwa vibaya na dreva. Alisema hivi, nanukuu"bwana dreva asanti sana kwa kuntia nyuma ya gari na mki wangu na mtoto ukawatii mbele ya gari . Asanti sana bwana

Nami, hii imenikumbusha hotuba ya mgeni rasmi kutoka mkoa wa Mara. Alianza kwa kusema ''nashukuru kupata nafasi hii kwani mwaka jana muriniarika nikaharisha, lakini leo nimefurahi sana nimekunya mbere yenu na wote mneniona''
 
Katika pitapita zangu mitaa ya Mpitimbi nilikutana na jamaa yangu Ngonyani nami kwa heshima yangu ya kinyamwezi nikamsalimia shikamoo mjomba,akanijibu "Malihabi mjombi ,hujambi?"Akimaanisha marahaba mjomba hujambo.

Mimi huko huko nilisikia mama mmoja akiulizwa na mzee 'uni uhakika na unichokinena? Nasemi hivii uniuhakika na unichokisimi? Hii ilikuwa ni baada ya kumpa mzee wa kingoni taarifa ambazo alikuwa haziamini.
 
hahaha aaaa wadau mmenichekesha sana Xmass yangu imekuwa nzuri, UNGONINI bana Raha sana!!! Nawa JAMBUSA( salimia) WOTE Heri ya kirisimasii(hatuwezi sena krismas) penyeapa mtima kuvina ati sijaenda kunyumba (Penyewe apa moyo unauma sijaenda nyumbani) CHRISTMASS OYEEEE BONA NE OOOOOOH CHRISTMAS OYEEEEE, TUKACHEZE KAMANYOLA NA MAQUIS OOOH, NAKWENDA WAAAPI!!!! aaaah KING KIKI MJOMBA ULIIMBA JAMANI Mwenye clip ya huu wimbo aniwekee nautafuta youtube siupatii plseeeeeeeeee walongo wangu.
 
Paka Mweusi umenikumbusha Nyumbi hii bombi hii, palepale pamfaranyaki, ukisikia jogoo anawika kokorikoo, ujue ndio hapohapo.

Happy New Year 2011!
 
Mimi huko huko nilisikia mama mmoja akiulizwa na mzee 'uni uhakika na unichokinena? Nasemi hivii uniuhakika na unichokisimi? Hii ilikuwa ni baada ya kumpa mzee wa kingoni taarifa ambazo alikuwa haziamini.

mmhhh hii sasa ni funga kazi langu jicho nafunga mdomo wangu
 
Katika pitapita zangu mitaa ya Mpitimbi nilikutana na jamaa yangu Ngonyani nami kwa heshima yangu ya kinyamwezi nikamsalimia shikamoo mjomba,akanijibu "Malihabi mjombi ,hujambi?"Akimaanisha marahaba mjomba hujambo.

nawe ungemjibu sijambi mana ukikaa kimya si ataona huna adabu ?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom