Nilimpenda sana JK bila sababu, Sasa Namchukia sana bila sababu!

Usihofu, hauko peke yako. Hata vijana wengi wanaoikimbilia chadema hawana sababu na kuna siku wataichukia bila sababu pia...

Nahisi una mtindio wa ubongo maana chadema si ya vijana tu bali hata sie wazee wenye busara zetu tupo.
Maneno yako ni matusi kwetu wazee wa chadema.
 
Nilimshitukia sana huyu jamaa na rafiki zangu wengi niliwaonya lakini hawakutaka kunisikiliza na wote wanajuta sana.
Bila shaka 2015 hawatafanya kosa hili tena.
 
ww ni moja kati ya watu waliolisababishia taifa hili janga 2005, nakumbuka mwaka 2005 nilivyogombana na watu wengi sana kipindi cha kampeni na leo wanakubali ww.
 
ww ni moja kati ya watu waliolisababishia taifa hili janga 2005, nakumbuka mwaka 2005 nilivyogombana na watu wengi sana kipindi cha kampeni na leo wanakubali ww.
Lakini ukweli 2005 alionekana mwana mapinduzi pamoja na kauli za matumaini, huwezi kumlaumu mtu aliyempigia kura ila ubovu wake umekuja kuonekana baadae.
 
mi ni mmojawapo aisee 2005 nilikuwa mstari wa mbele kumshabikia nilikesha kwenye kwenye kampeni za ccm nilikuwa nakaa na mjomba wangu alikuwa ananikinya sana kurudi usiku kisa kampeni siku moja nilirudi saa nane usiku nilimkuta mjomba wangu sebuleni aliiniuliza kwa upole sana "hivi unaweza kunipa sababu ya muhimu sana ya kumpenda jk?" ukweli sikuwa na jibu lolote la kumpa nikabaki nikawa namjibu atatuletea maendeleo akasema haya utakuja kuniambia, haya maneno nayakumbuka sana maana mjomba wangu leo angekuwa hai bado ningemuambia nimejionea mwenyewe mambo yanavyoenda na mwisho wa siku alifia hosptalini kwa kum overdose na madkari uchwara niliumia sana sasa hivi nikimuona jk najisikia vibaya ila amalize tu kipindi chake aondoke
 
Hiyo inaitwa chuki binafsi,kumchukia mtu bila sababu,na ni tabia ya kishetani hiyo.mtu hajakukosea unamchukia tu.kweli wewe ni bange
 
Hivi yule jamaa aliyetaka kumshusha jk mwanza yupo wapi, mi nahisi yule tupaswa kumhoji vizuri
 
kikwete hana tatizo wenye tatizo ni mimi nawewe wenye chuki binafsi na vijiba vya roho
 
Nilimshitukia sana huyu jamaa na rafiki zangu wengi niliwaonya lakini hawakutaka kunisikiliza na wote wanajuta sana.
Bila shaka 2015 hawatafanya kosa hili tena.

kosa lake nini???au nawe ni chuki binafsi kama mwenzako
 
Mwaka 2005 nilimshabikia sana JK hadi nikaona nchi mpya imezaliwa ila sikuwa na sababu za msingi maana alikuwa hana record yeyote ya kufanya mambo makubwa kwa nchi. Ilikuwa sio mimi tu maana wengi hawakuwa na sababu za kumpenda sana 2005. Mwaka 2010 nilimchukia sana hadi sasa hata picha yake nikiiona inanikera sana. Nikiwasha TV nikimkuta anazungumza nabadilisha haraka. Hanivutii tena hata kidogo. Sio mimi tu watu wengi sana wamchukia JK ila ukiwauliza hawana sababu za msingi.

Swali ni je, kuna ukweli kuwa umaarufu wake ulikuwa cosmetic na nguvu yake inapungua? Siamini mambo hayo ila inawezekana kuna ukweli. Enjoy your weekend guys!

inabidi uende kanisani kama mkristo ukaombewe kama mwislam wende msikitini,una jini chuki binafsi wewe na kwa style hiyo huwezi kupata maendeleo hadi kufa kwako
 
There are a million reasons to hate this lazy noncompetent failure state house hacker, just pick one
 
Mkuu no pun intended,kama ulimpenda na sasa unamchukia,basi inawezekana wewe ni mfuata mkumbo kama ilivyo kwa wengi wetu watanzania.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom