Nilikutema kumridhisha mama

arabianfalcon

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
2,285
584
Wapenda wana JF habari za leo,
Rafiki yangu kazini leo kanieleza mkasa wake nimemuonea huruma sana naombeni ushauri wenu wenzangu.
Huyu dada alikua na mpenzi wanapenda sana penzi lao lilidumu miaka mi3,mama wa mtoto wakiume akawa
Anajifanya anampenda sana huyu dada sababu mtoto wake alikua apeche na mdada mambo yake safi

Baada ya mtoto wake kupata muelekeo wa maisha mama anamwambie mwanawe NIKUSIKIE UMUOWE MALAYA YULE
Huna radhi na mimi,mtoto wa kiume alikolea kwa mdada kiukweli siku 2kabla ya ndoa mama wa mtoto akaona hana
Jinsi yakumkataza mwanae mama akaita kikao kukanya mwanae asiowe, mtoto akamwambia mamake kua anasahau
Kama huyo MALAYA ndio alimtoa huko mpaka sasa alipofikia ni huyu malaya ndio alimshika mkono,mama kuona
Kazidiwa na mwanawe akazivua nguo akasema ukiowa mie sio mamako tena harusi ikavunjika,

Mtoto wakiume akatafutiwa mke na mamake aoe akaowa,baada ya miaka mi3 mdada aloitwa malaya alisha jipanga akaolewa
maisha yake mazuri,bwana yule alomsikiza mamake kazi amefukuzwa mke kamkata kisa mume hana pesa na kachoka na kula daga msumari kila siku, jamaa na mamake walivyo kosa haya wanarudi kwenda kuomba msamaha eti shetani aliwapitia,je huyu mama na mwanawe walivyofanya ni haki? au huyo jamaa hakujua umuhimu wa yule dada mpaka akamsikiliza mamake? je unadhani watu kama hawa kwenye jamii tuwa tafautishe vipi? naomba msaada wenu.......

pole sana mwambie huyo dada awasamehe ila asirudiane na huyo kaka....tena asiangalie nyuma kabisaa watampoteza mtu na mamaye hawana haya loh.ila anaweza kumsaidia kibinadamu akampa mtaji ajifanyie biashara.......

so far jamaa hana kosa....
sio rahisi kwa culture yetu ,mama yako akuvulie nguo na wewe ujifanye mbishi..
culture zetu zipo deep mno...

labda mungu ameonesha kuwa hao wawili waliandikiwa wawe pamoja...
sasa bora mdada asamehe,warudiane....
mama huyo kashaumbuka na kujifunza....

Alimtema kwaajili ya mama na sasa anataka ammeze kwaajili ya mama huyo huyo!?

Umeshasema dada ana ndoa yake na mambo yake sio haba hivyo hana shida nao.Mwambie awaambie wachape mwendo...kijana hana msimamo mama nae hana shukurani wala sio mstaarabu.Hana haja ya kuwakaribishia watu wa aina hiyo maishani mwake.Hata akisema awasaidie tu...ipo siku atashangaa hata ndoa aliyonayo wanaivuruga!!

Hovyo kabisa...mimi naweza msamehe mwanaume akifanya kosa alafu asipete sapoti ya wazazi wake (yani nao wamuone mkosaji) ila kama wote wako kwenye boat moja hamna kitu hapo.Maana hata kujirekebisha itakua ngumu iwapo mzazi wake anamsapoti kwahiyo imekula kwao hiyo!!!

Hapo hakuna cha umshauri kitu, huyo dada aendelee na maisha yake, mimama mingine sijui inakuwa kama imepagawa vile, unamvulia nguo mwanao kisa? sasa ndio wajifunze wazazi wengine,..mwmbie huyo dada kama anaweza msaidia huyo kaka apate kazi amsaidie, ila asijihusishe nae na chochote, hata kama alimpenda vipi

pole sana mwambie huyo dada awasamehe ila asirudiane na huyo kaka....tena asiangalie nyuma kabisaa watampoteza mtu na mamaye hawana haya loh.ila anaweza kumsaidia kibinadamu akampa mtaji ajifanyie biashara.......

mmmh,mwenzangu mtaji simshauri,wajipange tuu kwani alipompa mwanawe mke alomtaka yeye hakujua kama maisha yana panda nakushuka,
yani kama mie hata staki kujua wasonge2,mama mtumzima halafu mie nashanga kwanini wazazi wengine wanakua na akili chafu kama hizo sijui wanashau fadhila mapema sana na wanaona huyo mkwe wao atafaidika wakati ni haki yake mke kula cha mumewe,ndio mana staki kuka na mkwe same house aje anione mwezi akimaliza aishie sio kama simpendi no naogopa kuniharibia nyumba yangu.

Speaking of mkwe, kuna dada mtaani juzjuz kamwambia mumewe akalale kwa mama ake, maana mama wanaishi naye, akisikia gari la mwanawe nje keshakurupuka eti kumwekea chakula, maji ya kuoga na maongezi sebuleni, yaani sdada kavumiliaa weeee mwisho kaamua liwalo na liwe kamtolea nguo zake kamwambia ahamie kwa mama, najua dada amevunja heshima, ila kuna wakati maji yanavuka shingo aisee

wamama zetu na wake zetu ni kama simba na yanga au tom na jerry
always visa lol

so far jamaa hana kosa....
sio rahisi kwa culture yetu ,mama yako akuvulie nguo na wewe ujifanye mbishi..
culture zetu zipo deep mno...

labda mungu ameonesha kuwa hao wawili waliandikiwa wawe pamoja...
sasa bora mdada asamehe,warudiane....
mama huyo kashaumbuka na kujifunza....
Hawezi kurejeana nae ameshaolewa na mume mwengine ana twins wake vi shunaaaaa!!!

hawa wanaonekana wanaweza rudiana, hapo sasa ndio mwanzo wa cheating, sababu mdada anaonekana aliolewa tu coz aliachwa mapenzi yako kwa huyo mkaka mwenye mama cha mdomo

Jamaa hapaswi kulaumiwa hata kidogo. Stage ya kuvuliwa nguo na mama si ndogo, na hakuna hata mmoja kati yetu anayeweza mkatalia mama ambaye amekuvulia nguo umuache mwenzio, ni uamuzi hatari sana kuendelea. Mama ndo hana busara. Dada amsamehe mwenzie, na amsaidie kama anaweza, aelewe hali ya mwenzie n nguvu kubwa iliyotumika kuwatenganisha. Hata ingekuwa upande wa dada mama yake afanye hivyo ndoa ingekufa tu.

Ndugu Wananchi Mmesahau ile Methali isemayo ''Mkataa pema''

''Pabaya panamuita''

Wapenda wana JF habari za leo,

Rafiki yangu kazini leo kanieleza mkasa wake nimemuonea huruma sana naombeni ushauri wenu wenzangu.

Huyu dada alikua na mpenzi wanapenda sana penzi lao lilidumu miaka mi3,mama wa mtoto wakiume akawa

Anajifanya anampenda sana huyu dada sababu mtoto wake alikua apeche na mdada mambo yake safi

Baada ya mtoto wake kupata muelekeo wa maisha mama anamwambie mwanawe NIKUSIKIE UMUOWE MALAYA YULE

Huna radhi na mimi,mtoto wa kiume alikolea kwa mdada kiukweli siku 2kabla ya ndoa mama wa mtoto akaona hana

Jinsi yakumkataza mwanae mama akaita kikao kukanya mwanae asiowe, mtoto akamwambia mamake kua anasahau

Kama huyo MALAYA ndio alimtoa huko mpaka sasa alipofikia ni huyu malaya ndio alimshika mkono,mama kuona

Kazidiwa na mwanawe akazivua nguo akasema ukiowa mie sio mamako tena harusi ikavunjika,

Mtoto wakiume akatafutiwa mke na mamake aoe akaowa,baada ya miaka mi3 mdada aloitwa malaya alisha jipanga akaolewa

maisha yake mazuri,bwana yule alomsikiza mamake kazi amefukuzwa mke kamkata kisa mume hana pesa na kachoka na kula daga msumari kila siku, jamaa na mamake walivyo kosa haya wanarudi kwenda kuomba msamaha eti shetani aliwapitia,je huyu mama na mwanawe walivyofanya ni haki? au huyo jamaa hakujua umuhimu wa yule dada mpaka akamsikiliza mamake? je unadhani watu kama hawa kwenye jamii tuwa tafautishe vipi? naomba msaada wenu.......

Dah, hivi kumbe kuna wazaz bado wako traditional mpaka sasa!

Back
Top Bottom