Nilikutana na My wife kupitia gazeti la majira...

mimi nilipewa namba ya simu na rafiki angu an stil nko naee
nkamua proach...
akazingua
nkarudia tena after month.....weweeeeee mtoto akilaini mwenyewe then tukafanya meeting ya 1.
 
Najua watu wanakutana wa wenza wa maisha yao katika mazingira tofauti. Kwa mimi ilikuwa hivi;

Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa nasoma kwenye gazeti la majira majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo kikuu fulani hapa Tz, nikiwa mmoja wao. Baada ya furaha ya kuchaguliwa, nikiwa na rafiki yangu, kama utani tulianza kupitia majina ya wadada ambao wangekuwa ma-class mates wangu. Kulikuwa na wadada 9 tu kati ya watu 54 hivyo haikuwa kazi kubwa kuwachambua.

Tulijenga imaginations za mdada alivyo kutokana na jina lake. Nakumbuka tulipofika kwenye jina mojawapo, discussion yetu ilikuwa huyu itakuwa sio mzuri, na zaidi ubini wake ulionekana ni wa kabila fuani linalosemekana wadada ni vicheche. Kwa mantiki hiyo, huyu aliwekwa kwenye kundi la 'wasiofaa'. Majina kama matatu hivi niliyachagua nikiamini lazima watakuwa 'wakali' na nitajitahidi nimpate mmoja wao.

Nilipofika chuo darasani nikawa nakaa kiti cha nyuma kabisa huku nikikagua wadada walivyokuwa wanaingia, na kujisemea "huyu lazima atakuwa fulani" (ile list nilikuwa nayo).

Nifanye tu stori kuwa fupi kwa kusema imaginations zangu zilikuwa tofauti sana. Mmoja kati ya wale watatu 'wanted' nilijaribu kumfuatilia, lakini hata hatukuanza baada ya kugundua hafai. Wale wengine wawili ndo kabisaaaa, hata kuanza sikuanza.

Wakati namaliza chuo, yule tuliesema kuwa hafai kwa sababu ya jina lake na kabila kuwa na tabia za 'ukicheche', alikuwa mchumba wangu, na sasa ni miaka mitatu tuko katika ndoa yenye amani na mapenzi tele.

Je, wewe ulikutanaje na wife/husband wako?

Case yako imefanana sana ya yangu banaa...
 
Unashangaza kweli na maswali yako...kwani watu wanaopanda daladala ni wa aina gani?!

Nashangazwa na kuingia kwenye mahusiano bila kufahamiana kabla ya kukutana kwenye daladala. Mshangao wangu haupo kwa aina ya watu wa kwenye daladala.......upo katika sehemu ya kukutania. Bora hata mfahamiane kwanza kupitia kisimani, darasani, kazini, kijijini,
 
Kwahiyo unadhani walishuka kwenye daladala wakafunga ndoa..?, lazima walifahamiana kwa muda..
 
Nashangazwa na kuingia kwenye mahusiano bila kufahamiana kabla ya kukutana kwenye daladala. Mshangao wangu haupo kwa aina ya watu wa kwenye daladala.......upo katika sehemu ya kukutania. Bora hata mfahamiane kwanza kupitia kisimani, darasani, kazini, kijijini,
Kwani hao wanaokutana kisimani,darasani,kazini na kijijini wanakuwa wamefahamiana before? Lazima kuna siku ya kwanza kuonana halafu huko kufahamiana kunafata na kwao mara ya kwanza walikutana kwenye daladala.
 
Nashangazwa na kuingia kwenye mahusiano bila kufahamiana kabla ya kukutana kwenye daladala. Mshangao wangu haupo kwa aina ya watu wa kwenye daladala.......upo katika sehemu ya kukutania. Bora hata mfahamiane kwanza kupitia kisimani, darasani, kazini, kijijini,
Kweli ushamba/ujinga hauna bei!!!Haya endelea kushangaa basi!
 
Back
Top Bottom