Nilichoshuhudia World Trade Centre kubaki ground zero - September 11

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,884
6,885
RTXKQQP_232941.jpg
1339521-large-watermark-comp_232905.jpg
space2_060250.jpg
AP01090105647_232923.jpg

Ilikuwa majira ya asubuhi wakati nipo nahangaika kurekebisha texture halftone dots kwenye computer ili kupata taswira sawia ya letters texture na picha nzuri kabla sija send kwenye image output, nikaona press man akija mbio kwangu na kunishtua kwamba Word Trade Centre New York imegongwa na ndege. "Oh man, come over here to watch live, something crazy happening in New York right now, otherwise you gona miss it." Stop scrolling down your computer screen man." Kwa kuwa nilikuwa bado na uchovu wa usingizi ukitilia maanani narudi toka chuo saa tano usiku na kulala muda mfupi tu na kisha saa moja asubuhi lazima niingie kibaruani maana maisha ya shule ughaibuni tofauti na ya kibongo na huna wa kumlalamikia karo na matumizi, kwani ni nyawigimbye, no dezo.

Kwa vile vijana hawa wa kimarekani tulizoea kutaniana kama kawaida yao nikaona leo wanaanza masikhara mapema hata kazi haijashika kasi. Kabla sijaachana na key board President kaja kwa speed na kuniambia, "they are not kidding you, very serious. Get out once, you never know whats gona happen here." Nikainuka na kutoka nje na kushtukia tower moja linafuka moshi mzito kuanzia theluthi moja ya juu. Na wakati bado tunaendelea kushangaa ilikuwa kama movie vile tukishuhudia bonge la dege jingine likiingia kwa kasi kwenye tower ya pili. Wasiwasi ulitujaa kwani hatujui nini kitaendelea.

Nilichoshuhudia ni ile ndege ya pili ikiingia na jinsi majengo yalivyoporomoka kwa awamu kwa kishindo na moshi uliochanganyika na vumbi la majengo kufunika sehemu kubwa ya Manhattan kitovu cha biashara ya marekani. Masaa macheche baada ya vumbi kusambaa kwenye mitaa na barabara za Manhattan nikakumbuka kumpigia simu mtanzania mmoja aliyekuwa anafanya kazi mitaa michache kutoka pale, na aliponihakikishia yuko salama na amepanda boti kuvuka mto Hudson kurudi NJ nikatulia kigogo ujuavyo damu nzito kuliko maji.

Kama kihoro nilichoshuhudia nilipokuwa nchini humo ni hiki cha tuko la Sptember 11. Ilionekana hakuna pa kushika na kabisa baada ya kuona Pentagon nayo imelipuliwa na ndege iliyotegemea kulipua Makao Makuu ya serikali imeangukia huko Conner stone state (PA) basi palikuwa hapatoshi. Moshi kutoka masalia ya majengo ulifuka kwa takribani miezi miwili. Ama kwa hakika jungu kuu halikosi ukoko.
 
Je kwa mtizamo wako , ukireflect yaliyotokea wakati huo, je bado unaamini ni alqaeda walifanya mashambulizi yale au ni serikali ya george bush ili wapate pretext ya war kwa ajili ya kujitanua mashariki ya mbali, na kuziintimidate serikali za dunia zipitishe sheria fulani fulani za kiulinzi zenye kuinufasha amerika?.

Ni nini maoni yako juu ya kuanguka jengo la world trade centre 7 (wtc 7), maana hilo halikugongwa na ndege yoyote, na lilisimama muda mrefu tu baada ya twin towers kuanguka na then baadae likacollapse vertically?

Ahsante!
 
Kila mmoja anamtazamo wako. Leo maafa yaliyotokea kuzama Meli iliyokuwa ikitokea Zanzibar kuelekea Pemba kila mtu anatoa tafsiri yake, lakini jambo moja tu ninaloweza kukuambia sina hulka ya mambo ya kusadikika, ila kutokana na uchunguzi uliotumika kwa njia inayoeleweka kwa uwazi na kujibiwa na wahusika ndo ninayofahamu mie. Hii ya kujitanuwa wamarekani kwenda middle east sijui cho chote.
 
Hata mie nilishuhudia through TV (CNN) nilikuwa na brother wangu (RIP) tulipoona ndege ya pili napiga tower ya pili alisimama na kusema kwa kisukuma " Utulwa mna Amerika!" he hated Americans
 
Hata mie nilishuhudia through TV (CNN) nilikuwa na brother wangu (RIP) tulipoona ndege ya pili napiga tower ya pili alisimama na kusema kwa kisukuma " Utulwa mna Amerika!" he hated Americans

Wakati narudi home toka kazini hata hamu ya kuingia darasani siku nayo ila tu nilijilazimisha hadi kufika chuoni nikaambiwa no class today. Nikageukia upande wa mto Hudson na kuangalia Manhattan ilivyofuka moshi na kuchafuka kwa jivu na vumbi hakukutamanika kamwe. Kila niliyemtazama bila kusema kitu anaitikia kwa kutikisa kichwa na kutoamini kilichotokea.
 
Back
Top Bottom