nilichokiona leo kwa house girl wetu

kaburu mdogo

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
567
400
binafsi napenda sana kuwaheshimu hawa wasaidizi wa ndani maana ndo wanaobeba majukumu yote ya familia kuanzia asubuhi hadi usiku,kiusalama na kila kitu ndani na nje ya familia.nilichokiona leo hapa nyumbani kwetu kimeniskiktisha sana na sikujua kama mzazi wangu anaweza kufanya hivyo;miezi miwili iliyopita alichua msichana kutoka mkoa wa arusha (meru) na kuja nae huku kwa ajili ya kumsaidi kazi za ndani maana wa awali aliondoka na hakurudi,sababu sizijui.baada ya wiki kadhaa nikanza kusikia msichana wetu anaanza kulalamika kuwa bora angerudi na mwisho wa mwezi huu angemwambia bosi wake kuwa anataka likizo fupi maana nyumbani kwao kuna tatizo na ameitwa ghafla na wazee wake!wiki moja baadae mama akapata hizo taarifa na kuniuliza kama nimemsikia akisema nami nikamjibu kuwa binanfsi ahajanambia ila naskia akiwaambia wenzake juu ya swala hilo.wiki iliyopita mama alitafuta msichana kisiri na kumficha kwa jirani na kuanza kumtahutia mdada wa watu sababu lukuki ikiwemo hujui usafi,hujui kupika na mengine mengi ,mdada wa watu akawa anavumilia na mwisho alinambia anahisi mama amemchoka na anamtafutia sababu ili amfukuze.
jana asubuhi bi mkubwa anampa msichana taarifa kuwa anatakiwa kujiandaa aende kwao leo na kunituma nikamkatie tiketi ya basi,jana hiyo hiyo nilimkatia ticket,huku nyuma kumbe bi mkubwa alikua anafuatilia hatua kwa ahatua kila kitua alichokuwa anakifanya huyo mdada kwenye maandalizi yake ya kufungusha mizigo,jioni ndo mzozo ulipokua mkali sana maana msichana wa watu alikua amefungasha vitu vyake vizuri kwa ajili ya safari lahuala bi mkubwa anaanza kuulizia kitu kimoja baada ya kingine alichokua mempa na kuanza kumnyang'anya.nilikereka na iliniuma sana mdada wa watu anabaki kutazamatu asijue la kufanya na alichofanay ni kwenda kununua mfuko wa kirba kwa mangi muuza duka na kufungasha upya mizigo yake,inauma kwa kwel,wazai wetu wana roho nzuri pindi wawa chukuapo wadada ila pindi wawachukiapo ni kiama kikubwa kwao.tujirekebishe maana hizi ni laana kwetu na kwa wajukuu zetu kutoka kwa hawa wadada jamani
 
Afadhali umeliona hilo ila kwanini hukulikemea? We ndo unampa mama yako kichwa na nakuhakikishia akimalizana na wasaidizi atahamia kwa mkeo.
 
Kama wewe muanzisha thread ni mtoto wa huyo mama, ina maana unamuogopa mama yako mzazi au??kama uliumia why ulikaa na kuangalia??ina maana huna sauti kwa mama yako??ulipaswa kumwambia bimkubwa amwachie kila kitu aondoke zake sasa wewe ulikaa tu na kumuangalia??Hata kamaa ni mzazi wako endapo unamuonaa mahali yupo wrong then inabidi uongee na sio kukaa kimya na kuangalia tu....
 
Afadhali umeliona hilo ila kwanini hukulikemea? We ndo unampa mama yako kichwa na nakuhakikishia akimalizana na wasaidizi atahamia kwa mkeo.

Kabisa kwa jinsi nilivyoona maelezo ya huyu jamaa huyo mama atahamia tu kwa mke wake na kumtesa na yeye ataangalia tu na kukaa kimya.....lazima mtoto wa kiume uwe na msimamo ndani ya nyumba hata kwa mzazi wako.....
 
Pole mwana ndo maisha hayo ila bidae ongea na bi mkubwa umwambiea sio vizuri anavyofanya cz bidae wengine watapewa hizo habari matokeo yake ntawekewa sumu c unajua binadamu tupo tofauti
 
Kama kawaida yako full kukurupuka na mineno kama hamnazo.
Unaujua umri wa muanzisha mada?
Kuna sehemu yeyote hapa ameandika kuwa ameoa?
Ulishapima consequences za mtoto (may be) wa umri fulani kumkosoa mama ambaye tabia zake ndio kama hizo?
 
Sio full kukurupuka umeona comment yangu kuna mahali nimesema ameoa??Hata kama hajaowa doesn't matter as long kama mdogo anapoona mzazi wake yupo wrong amwambie na sio kukaa kimya tu...fikiria zaidi then ndio ujibu comment...Hamna umri wa kumkosoa mzazi wako as long upo matured enough unajuwa kizuri na kibaya hapo unaweza kumwambia mzazi no hapo upo wrong....

N.B Najaribu bado kukusoma ni mtu wa aina gani na comment zako zilivyo too low alafu hupendi kuumiza kichwa kwa kufikiria zaidi
 
Bahati nzuri hakuhesabiwa vitu alivyovunja. Kuna nyumba siku hgeli anaondolewa ni mtiti. Glass unevunja nilinunua 10$ per pc SA, shuka lilichujia rangi nilinunua 100$ flea market china. Sasa na kitopu aliletewa ataambiwa ni cha 58$ na gauni la krismas alishoneshewa eve collection 250,000. Ilimradi dada wa watu hajalipwa mshahara kwa miaka 3 na hela yote ni makato. Kuna watu wan roho za kutu acha tu!
 
Kabisa kwa jinsi nilivyoona maelezo ya huyu jamaa huyo mama atahamia tu kwa mke wake na kumtesa na yeye ataangalia tu na kukaa kimya.....lazima mtoto wa kiume uwe na msimamo ndani ya nyumba hata kwa mzazi wako.....

unaleta ukiume wakati unakula ugali wa shkamoo? Umelelewa na familia wewe ama umekulia ghetto?
 
Pole mwana ndo maisha hayo ila bidae ongea na bi mkubwa umwambiea sio vizuri anavyofanya cz bidae wengine watapewa hizo habari matokeo yake ntawekewa sumu c unajua binadamu tupo tofauti

OMBI: Kikaragosi tafadhali badilisha 'avatar' yako...nimejiskia vibaya sasa hivi wakati nasoma hii thread, ahalafu amekuja colleague mMarekani hajui kiswahili..lakini hiyo avatar imemfanya ahdani kuwa tunadiscuss mambo ya kifuska kwenye hii forum. Bahati nzuri amekuwa mstaarabu kiasi cha kuniauliza na nikamuelewesha!

Sikulazimishi...lakini mara nyingine vitu kama hivi vinatuvinjia heshima! Hasa watu ambao tuko JF muda wote wa kazi!
 
unaleta ukiume wakati unakula ugali wa shkamoo? Umelelewa na familia wewe ama umekulia ghetto?

Kwa vile unakula ugali wa shikamoo ndio ukae kimya na kuangalia nini bimkubwa anamfanyia mfanyakazi hata kama ni wrong?nadhani kila mtu amekulia mazingira tofauti so wala sishangai sana.....
 
Hadithi inavutia, yule aliyefichwa kwa jirani ikaishiaje? Au jirani yuko mbali hakushuhudia yaliyompata mwenzake?
 
Pole sana mkuu, mshukuru mungu pia kwa kuwa na moyo wa huruma kwani wengine wana join na wazazi wao kuwanyanyasa hawa watoto wa watu!

Muda mwingine wazazi wetu huwa chanzo cha hawa wasichana kufanya matendo ya ajabu kwani hawana huruma nao!

Kwakweli ni bora ukae na mama yako muongee kwani sidhani kama ataweza kukaa na wasichana wa kazi kwa namna hiyo!

Lakini hii ilifaa sana kule MMU
 
hii sio hadithi kaka,ni ukweliukweli mtupu,hili limetokea nyumbani kwetu na msichana ameondika leo kwa kumpakia kwenye gari la ngorika la saa kumi na mbili kwa safari ya arushak,yule wa jirani mbona ndo anaendelea na majukumu yake hapa ndani!yupo amejaa tele toka saa nne asubuhi.
Hadithi inavutia, yule aliyefichwa kwa jirani ikaishiaje? Au jirani yuko mbali hakushuhudia yaliyompata mwenzake?
 
kwa bahati mbaya sina mazoea ya kukaa na mama kuongea nae juu ya wasicha wa kazi labda pale msichana huyo anapokaribia kuondoka maana wao wenyewe ndo huniambia kuwa siku fulani naondoka,na siwezi kumwambia pia maana mtaa mzima utajua mimi na watetea wasichana wa kazi na kumsaliti kama mwanafamilia,japo huwa nawaambia rafiki zake waongee nae kama rafiki yao na kumwambia.
Afadhali umeliona hilo ila kwanini hukulikemea? We ndo unampa mama yako kichwa na nakuhakikishia akimalizana na wasaidizi atahamia kwa mkeo.
 
hivi nyie mnadhani ni rahisi kwa mtoto kukaa na mama yake na kuanza kuongea juu ya mambo ya msichana wa kazi ni rahisi kiasi hicho kwenye kila familia? midomo ya wanawake waachieni wenyewe maana bi mkubwa wangu atakuchamba mpaka mtaa wa saba wajue na kusema unaisaliti familia kisa house girl
Kama wewe muanzisha thread ni mtoto wa huyo mama, ina maana unamuogopa mama yako mzazi au??kama uliumia why ulikaa na kuangalia??ina maana huna sauti kwa mama yako??ulipaswa kumwambia bimkubwa amwachie kila kitu aondoke zake sasa wewe ulikaa tu na kumuangalia??Hata kamaa ni mzazi wako endapo unamuonaa mahali yupo wrong then inabidi uongee na sio kukaa kimya na kuangalia tu....
 
jamani huyo mama kiboko ila na ww umenikata kinoma why hukumuambia bi mkubwa kua anachofanya sio fresh hata kidogo jamani kha! au ni mkali mpaka na nyie mnamuogopa sana humo ndani( i mean yeye ndio final say)...
 
hivi nyie mnadhani ni rahisi kwa mtoto kukaa na mama yake na kuanza kuongea juu ya mambo ya msichana wa kazi ni rahisi kiasi hicho kwenye kila familia? midomo ya wanawake waachieni wenyewe maana bi mkubwa wangu atakuchamba mpaka mtaa wa saba wajue na kusema unaisaliti familia kisa house girl
duh! bi mkubwa sio kabisa ila mtu wa ivi ukimjulia unakua unakaa mbali na anga zake basi
 
Back
Top Bottom