Oluwa ni
JF-Expert Member
- May 24, 2015
- 717
- 445
Habari zenu wakuu,
Nadhani wengi mtakuwa mnakifahamu chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).
.
Binafsi jana nilikuwa nimempeleka dogo wangu akasajiriwe maana pale usajiri umeaanza tarehe 28/11 na hivyo nikaona sio mbaya nikienda na dogo wangu wa kiume ili tukiwa wawili tuweze kukabiliana na changamoto za usajiri kama ilivyo usumbufu hata kwa vyuo vingne vikubwa Tanzania.
Cha kushangaza nimekutana na mambo tofauti ambayo yamenifanya nifungue uzi huu na mengine yamenifurahisha.
Kwanza usajiri wao wako fasta na kuna njia mbili, moja ni online ambayo mwanachuo unatumiwa link, username na password na unajisajr na kuattach vyeti vyako ikiwemo slip ya bank.
Baada ya hapo unasubmitt taarifa online kisha unaanza kuzunguka meza za wasajir na unaanzia kwa mhakiki wa bank slip, kisha kwa mhasibu baada ya hapo unaenda sehemu ya kozi yako huska alafu unaenda kukusanya slip yako ili upewe risiti ya malipo ukitoka hapo unaenda kuwekewa taarifa zako kwenye file na unapewa admission number..
Hapo ni kama dakika 20 au 30 kuwazungukia hao wote baada ya hapo unaenda na file lako sehemu ya kupiga picha kwa ajiri ya kupewa kitambulisho cha chuo na hapo unatumia kama dakika 2 tu tayari unapewa kitambulisho chako..
Yaani mizunguko yote unaweza kutumia kama saa 1 tu unakuwa umekamilisha kila kitu..
Sasa nilikuwa najiuliza vyuo vingine ambavyo usajiri mtu anatumia mpaka wiki nzima inakuaje?? Kama watu ni wengi mbona na pale NIT ni wengi mwaka huu ila wako fasta kusajili.
CHANGAMOTO: Kuna watu wanakuja pale hawana fomu hata moja hata admission form hawana. Kuna wale wengine kwa bahati mbaya hawakutumiwa link yenye username na password hvyo inakuwa ni tabu mpaka kumaliza usajili.
Wengine pia hawako serious na mambo yao mtu anakuja kwa ajili ya kuangalia tu mazingira na kuondoka hajali kuhusu usajiri hvyo anakurupuka siku za mwisho.
MAMBO YALIYONICHEKESHA:
Yaani unakuta kipofu anamuelekeza kipofu mwenzie njia hapo utacheka kweli, mtu hajasajiriwa na hana idea yoyote kwamba usajiri unaenda vipi hapo hapo anakuja mtu mwingne wa hvyo hvyo anahitaji msaada kwa hasiyejua.
Kuna mdada fulani jana katoa machozi adharani baada ya kukosea kuandika majina yake kwa usahihi wakati anafanya online registration na alikuwa tayari amesubmitt taarifa hvyo hakujua namna ya kuedit mpaka alipoelekezwa kwa IT ambaye alimfungulia system tena ndipo akaedit..
Furaha baada ya usajiri.. Mtu anatoka chumba wanachotoa vitambulisho akiwa amefanikiwa kupata kitambulisho huku akiwa na furaha mpaka unaweza kuhisi labda amelogwa mpaka watu wanamshangaa..
Jana nimeenjoy siku yangu ntamwambia dogo wangu hata kwny welcome 1st year niende maana ntapata burudani japo sihusiki..
Cc buzi lisilochunika
[HASHTAG]#BeSerious[/HASHTAG]
[HASHTAG]#StepByStep[/HASHTAG]