Nilichojifunza Bandarini Dublin Kuhamia Dar - PINDA

Mkuu,
Pinda alijibu nini kuhusu hospitali ya Mara?Ni hospitali gani inaongelewa ni ile ya Kwangwa au ni ya pale mjini iliyoachwa na mkoloni?Kuna wakati nilisikia hospitali ya Kwangwa ianataka kuchukuliwa na Kanisa Katoliki.

Mkuu Lageneral salam,
Katika taarifa niliyopewa inasema ni Hospitali ya Mkoa na kufuatilia kwangu nimepata jibu kuwa hiyo ya Kwangwa ndio ya mkoa napia ndio Kanisa Katoliki wanayotaka kuiendeleza.Habari zaidi zinasema Mheshimiwa Pinda anamualiko Mkoani Mara kwa madhumuni ya kuhamasisha uchangiaji wa Hospitali hiyo. Jibu la mh Pinda alikubali kuwa huo mradi umesahauliwa au kutupwa kwa muda mrefu na sasa ni wakati wakuushughulikia.
 
Last edited:
Kwanza nasikitika kumis kikao hicho. Pili naomba kuuliza watanzania wenzangu mlioshiriki kikao na kumpigia makofi YES WE CAN kama inavyoripotiwa, mnafahamu mchakato ya policy intervention katika nchi zinazo endelea na mkaona applicability yake TZ kisha kumpigia makofi bila hata yaufafanuzi itafanyikaje? Mambo ya kitaalamu tusiruhusu wanasiasa watupige politic na kuwashangilia, they should tell us how they gonna put things into practice. Swali dogo tu mngemuuliza Dublin kuna makampuni tisa ya kutoa Mizigo badalini je na TZ tunahitaji kampuni tisa or what is feasible number of firms we need for the purpose? Mipango mingi inafeli bongo kwa kuwa wanasiaja wanaiga bila hata kujua empirical and conventional basis ya hivyo wanavyo taka kucopy. Nashauri tuache kushangilia mpaka tuelezwe mikakati husika sio politic za kuwafanya politician watoke roho zao zikiwa zimesuuzika kwa kudanganya umma.

bm21 salam mkuu,
Inaelekea kuwa upo Uk na ikawaje ukakosa hicho kikao?hata hivyo kwa mujibu wa taarifa niliyonayo waliitwa viongozi wa Jumuia za Watanzania. Kwa maoni uliyotoa ni hakika maswali hayo yangepaswa kubainishwa. Jaribu kuwatafuta jamaa wa Tanzania Association ili future events zisikupite nimedokolewa kua Raisi huenda akaelekea huko punde.
 
Kufananisha bandari ya daresalama na bandari ya Dublin mmmmhhh. Kidogo naona bwana pinda amejikwaaa. Kwanini asiifananishe na ya msumbiji?.
 
Nitamshauri Pinda kufikiria upya mawazo yake kwani Tatizo sio wingi wa Wakandarasi isipokuwa sheria na taratibu zinazoambatana na WATU na MAZINGIRA yetu. Tanzania na hasa Dar sio Dublin wala Ulaya kwa sababu kwanza tuna Handle discipline problems na effective workplace management ni kama vile uko mnadani, miaka nenda miaka rudi..
Ushindani kwetu sisi ni DEAL na unakaribisha zaidi wizi, magendo na pengine hata kupotea kwa mizigo kwani mizigo itakuwa inatolewa na mikono mingi yenye majukumu sawa.. Access ya bandarini itakuwa wazi kwa mashirika tofauti na watu wasiojulikana wataweza kupenya kirahisi..Naifahamu Bandari yetu na matatizo ya wananchi wake mbali kabisa na mkandarasi mhusika ambaye pia ni part of the problem. Kwa hiyo, kwetu sisi siku zote imekuwa sio swala la namba za mashirika ila NANI anayeshika madaraka hayo!..

Kinachotakiwa Tanzania kwanza ni kuhamisha bandari nzima ya mizigo toka hapo ilipo, kisha ni kuwapa M/wakandarasi wenye experience, uwezo toka vifaa hadi kifedha kuweka mitambo ya kisasa inayolenga mbali (longterm)..
Kwa sasa hivi Uongozi mzima wa Bandari unatakiwa kutazamwa upya kwani tatizo sio Mkandarasi peke yake ila ni mfumo mzima wa kutoa mizigo.. Kuna MIKONO mingi sana yenye mamlaka na sauti tofauti kisha kuna watu waliokabidhiwa madaraka wanajiuona MIUNGU WATU..wanafanya kazi wanavyopenda wao..
 
watu wenye hisa bandarani wanatoa michango kwa chama tawala
kwa hiyo yote ni porojo tuu
 
Muhehimiwa Waziri mkuu wa Tanzania Bw Mizingo Pinda alitamka hayo alipokua akijibu maswali ya viongozi wa jumuia mbalimbali za Watanzania waishio Uingereza. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za ubalozi wa Tanzania jijini London pia ulihudhuriwa na Mh Balozi mama Mwanaidi Maajar na Maafisa wa ubalozi.baada ya viongozi wa jumuia hizo kujitamulisha wakiongozwa na mwenyekiti wa Tanzania association,Waziri mkuu alitoa fursa ya kujibu maswali badala ya kutoa hutuba,akichelea kuwbowesha wasikilizaji wake.Maswali yaliyojitokeza yalihusu 1,uraia wa nchi mbili 2,hali ya ufisadi nchini TZ 3,mizigo bandarini 4,hospitali mkoa wa mara 5,rushwa(bandari,TRA,(EPA)).6,hospitali ya muhimbili na 7,kitabu ;bunge lenye meno.Katika kujibu maswali hayo waziri mkuu alielezea hali ya bandari ya dar kama ni ya kusikitsha mno na ana hakika ubovu mkubwa uliopo na uzorotaji unasababishwa na MKATABA MBOVU ambao umemkabidhi Mkandarasi mmoja kumiliki shughuli zote. kutokana na kukosa mshindani imemfanya aendeshe kama apendavyo alisema waziri Pinda.Hiyo ni tofauti kabisa na hali niliyoikuta Dublin,Bandari ya Dublin kuna Wakandarasi Tisa wanaoopareti hivyoni wazi kutakua na ushindani wa kutrak Meli in. Hivyo nimeondoka na funzo kuwa mkataba tulionao Dar hautufai na hauwafai Wananchi na sidhani kama itakuwa kazi kuwashawish wenzangu kuvunja mkataba huo na tuige mfano wa Dublin.I think we can alisisitiza Pinda na Wasikilizaji walijibu YES WE CAN huku wakipiga makofi.Chanzo changu kiliniarifu kuwa kikao hicho kilichelewa kuanza lakini kwa mtazamo wake kilikua cha mafanikio kwa pande zote. kikao kilifanyika jana 02 03 2009.
Takriban mwaka na miezi miwili sasa toka waziri mkuu Mh. Mizingo Pinda atoe ahadi ya kurekebisha matatizo yaliopo katika bandari ya DAR ifanane na aliyoyaona katika bandari ya Dublin. Kesho 26/05/2010 anakutana na Wadau wale wa mwaka jana jijini London, mh Waziri mkuu, swali la nyongeaza: Ni mabadiliko gani yamefikiwa katika Bandari ya Dar es salaam toka ulipotupa ahadi ya kupeleka mfano wa Bandari ya Dublin zaidi ya mwaka mmoja uliopita?
 
Takriban mwaka na miezi miwili sasa toka waziri mkuu Mh. Mizingo Pinda atoe ahadi ya kurekebisha matatizo yaliopo katika bandari ya DAR ifanane na aliyoyaona katika bandari ya Dublin. Kesho 26/05/2010 anakutana na Wadau wale wa mwaka jana jijini London, mh Waziri mkuu, swali la nyongeaza: Ni mabadiliko gani yamefikiwa katika Bandari ya Dar es salaam toka ulipotupa ahadi ya kupeleka mfano wa Bandari ya Dublin zaidi ya mwaka mmoja uliopita?

Sitegemei kuna jibu loote atakloweza kuto kuhusu Bandari yetu ilyooza...Mhe Kagame alilamika kwa JK lakini wakaona mpuuzi.Sasa hivi nchi ambazo waluwa wakitumia bandari yetu wametuhama.
Leo tungekuwa tumeizatiti bandari yetu angalau kama Mombasa na sio Dublin ambayo ni ndoto ya kusadikika tungeweza angalau kuziba tundu katika bajeti yetu.
Lakini wako wapi waziri Kawambwa?...inasikitisha sana kuona hata wabongo wanaogopa kuitumia bandari yetu na inasikitisha zaidi kuona viongozi wetu hawajali wala haiwasumbui kabisa. I CRY FOR YOU TANZANIA....
 
Topic kama hizi tungekuwa tunawaprintia na kuwatumia kabla hawajaja kwenye kuomba kura (kula) tena
 
Back
Top Bottom