Niliasisi CHADEMA si kwa lengo la kutafuta vyeo - Edwin Mtei

matamko yanazidi kuongezeka kutoka kwa huyu mzee kisa zitto ametangaza kugombea urais.yeye kama mzee hapaswi kuonyesha mapenzi kwa mkwe wake,yeye ni mzee wa chama.
 
huku ni kukandamiza demokrasia.acha vijana waonyeshe uwezo wao sio kila siku kututangazia kuwa uliasisi chama. Au ndio yale yale ya hii ni kampuni ya watu wa kaskazini
 
Tatizo lake ni kwamba historia imekua ikionyesha kwamba tangu wakati wa mchakato wa uchaguzi 2010 Zitto amekua akitumia kila nafasi aipatayo kujinadi kutaka urais 2015, bila kujali muda wala wakati wa kufanya hivyo.Kwa mfano kile hakikuwa kipindi cha kuwaaminisha wananchi hasa wa North Kgm alikokuwa akipiga kampeni za ubunge kwamba Dr. Slaa hafai kuiongoza nchi hii kwa miaka 10 endapo atachaguliwa , lakini yeye badala ya kumpigia kampeni mgombea urais wa chama chake alijikita zaidi kujinadi kwa hilo..Kwa hiyo ni sahihi tu kumnyamazisha ingawa kwa ninavyomfahamu mimi hawezi kunyamaza kwa sababu hapa imeshaonekana lengo lake si Urais bali kuna kitu nyuma yake, na kuna ushahidi kwamba kuna wakati aliwahi kufanya mawasiliano yenye sura ya kuisaliti Chadema.Anajua kwamba hawezi kupata kura za kutosha kumfikisha huko kwani Dr. Slaa bado anakubalika zaidi na anazidi kukubalika kuanzia ndani hadi nje ya chama,Zitto analijua hilo, Chadema ianguke kiska wakose wote CCM ipite, haya mambo hutokea sana kwenye vyama vyetu, hata CCM iliwatokea Igunga ambapo kada mmoja aliwahi kutamka kwamba "ngoja tushindwe uchaguzi ili tuheshimiane", ya CCM Arumeru siyazungumzii sana kila mtu anajua, na ya Zitto pia ni hayahaya..Mtei yuko sawa kabisa.
 
Mzee umeongea vyema,maana timu yayote ile lazima iwe na mshikamano ndipo itashinda.
Huwezi kuwa unawaza kumaliza mpira wakati ushindi hujapata.ZITTO kuwa na subira,Tanzania ni yetu sote.Pia kumbuka ndugu yangu ZITTO sio kila makaofi wanayokupigia ni ya sifa bali mengine yamejaa kejeli.
 
Tatizo lake ni kwamba historia imekua ikionyesha kwamba tangu wakati wa mchakato wa uchaguzi 2010 Zitto amekua akitumia kila nafasi aipatayo kujinadi kutaka urais 2015, bila kujali muda wala wakati wa kufanya hivyo.Kwa mfano kile hakikuwa kipindi cha kuwaaminisha wananchi hasa wa North Kgm alikokuwa akipiga kampeni za ubunge kwamba Dr. Slaa hafai kuiongoza nchi hii kwa miaka 10 endapo atachaguliwa , lakini yeye badala ya kumpigia kampeni mgombea urais wa chama chake alijikita zaidi kujinadi kwa hilo..Kwa hiyo ni sahihi tu kumnyamazisha ingawa kwa ninavyomfahamu mimi hawezi kunyamaza kwa sababu hapa imeshaonekana lengo lake si Urais bali kuna kitu nyuma yake, na kuna ushahidi kwamba kuna wakati aliwahi kufanya mawasiliano yenye sura ya kuisaliti Chadema.Anajua kwamba hawezi kupata kura za kutosha kumfikisha huko kwani Dr. Slaa bado anakubalika zaidi na anazidi kukubalika kuanzia ndani hadi nje ya chama,Zitto analijua hilo, Chadema ianguke kiska wakose wote CCM ipite, haya mambo hutokea sana kwenye vyama vyetu, hata CCM iliwatokea Igunga ambapo kada mmoja aliwahi kutamka kwamba "ngoja tushindwe uchaguzi ili tuheshimiane", ya CCM Arumeru siyazungumzii sana kila mtu anajua, na ya Zitto pia ni hayahaya..Mtei yuko sawa kabisa.
Hili GUGU ZZK napendekeza ling'olewe mapema ili machungu yawe yametulia ifikapo 2015!!
 
Tangu Mnyika atangaze kuwa maneno ya Mtei hayana uhusiano na misimamo ya CHADEMA, mzee Mtei akisema jambo huwa linaonekana kama hdithi za vijiweni tu. Leo ameongea mambo ya busara sana, ila sasa hatujui kama ni msimamo wa chama au ni maoni yake kama jinsi Wema Sepetu pia anavyoweza kuwa na maoni yake!!!
 
Kama kweli alilolisema Mzee mtei lina heri basi wamuunge mkono ZITTO apeperushe bendera ya CDM mwaka 2015 kwa vile tayari yeye ameonesha nia, na kama ni unafiki wa kutaka kumpalilia njia mkwe wake hakika patachimbika.
Issue si Zito bali ni matokeo yake kwa chama. kama watajitokeza msururu wa watangazania wengine kutatokea makundi madogomadogo kila moja likimuunga mkono mmoja wao. hali hii itaathiri umoja wa chama na hata kukiweka chama pabaya wakati wa kuja kumpata mgombea. nadhani ni vema tukakubaliana kuhusu utaratibu na huo uwe ni utamaduni wetu. inawezekana pia Zito akajakuwa mgombea kufuatia maoni ya mzee mtei. hakuna haja ya haraka
 
msee mtei amempenda mkwe wake mbowe sawa na binti yake alivompenda mume wake
 
huu ni wakati wa wetu vijana tuachwe tuwe huru ki mind tuamue kile tunachokitaka sio mtei anachokitaka.
 
naushauri uongozi wa chadema na wanachedema kwa ujumla kuanzia sasa hivi waanze kuwatambua wapiga kura wake mwaka 2012. ni lazima kwahamasisha watu wako tayari kukipigia kura kwa kukomesha imani za baadhi ya watu kuwa kura yake moja haina athari. kuna watu wanasema hata ufanye nini ccm lazima ishinde kwa hivi wanaacha kupiga kura. huu ni usaliti wa demokrasia.
wanachadema wapiganaji wajifunze sera za chama na taratibu waelimishe watu kuhusu hizo sera. acheni kushutumu muda mwingi bali muda mrefu toeni elimu. pia epukeni makosa madogomadogo kwani yanakipunguzia chama heshima na kuaminika kwa wanachi. kila mtu apambane kwa nafasi aliyonayo. kila mtu aamini katika mabadiliko yenye kuleta ukombozi
 
Kutangaza nia ya kuwania uraisi huku ukitambua huna sifa ya umri kwa mujibu wa katiba ya sasa na wakati ambapo si kipaumbele cha chama ni sawa na kutangaza nia ya kukibomoa.

Demokrasia si kufanya kitu chochote unachojisikia wakati wowote pasipo kuzingatia maslahi ya chama. Tukikubali kufanya demokrasia ya aina hiyo tutakuwa tunaendekeza ubinafsi badala ya maslahi mapana ya umma.

Mkuu Mwita Maranya hivi kama hana sifa na akawa anapita huku na huku akitangaza nia si mnampuuuza tu? Mbona kila akitangaza manakuja juu kuwa anakibomoa chama? Unakumbuka wakati ule Mrema anabebwa na gari lake kusukumwa? Mwalimu alisemaje?

Mimi nadhani Zitto amewasaidia sana kwa kuweka nia yake hadharani kuliko ambao wanafanya mambo chini ya kapeti. Hao ndio wabaya zaidi kwa sababu siku wakiibuka mtakuwa hamkutegemea na watakuwa walishajijenga vya kutosha kimya kimya na hapo ndipo kutakuwa na sintofahamu.
 
Last edited by a moderator:
Mzee huyu ana busara balaa, wanaotaka uteuzi CDM waache malumbano yasiyo na tija maana cyo muda mwafaka.
 
huu ni wakati wa wetu vijana tuachwe tuwe huru ki mind tuamue kile tunachokitaka sio mtei anachokitaka.
Hili suala la vijana na wazee limejitokeza sana siku hizi. na linaanza kuwa tatizo. tujue kuwa hakuna vijana bila kuwepo wazee na hakuna wazee bila kuwepo vijana. it is becoming a typical discrimination. we need the minds of our elders just as we need the energy of the youths. both have to work jointly for development of humankind. both have to be listened. maendeleoya dunia hii ni matokeo ya constructive ideas mbalimbali za watu. kila wazo halipaswi kupuuzwa bali kutafakariwa. LET'S THINK OVER AGAIN OF OUR STATUS OF BEING GREAT THINKERS?
 
Hapo kwenye wekundu:

Kwani wanaotangaza kwamba watagombea urais kupitia CDM (Kama Zitto) wamesema kwamba watajiteua? Namsikia kila siku Zitto akisema "...kama nitapata ridhaa ya chama changu...." Hii inadhihirisha kwamba atatafuta ridhaa ya chama chake (CDM).

Nikweli atatafuta ridhaa ya chama chake na anajua hatapewa, ndiyo maana tunasema anachokifanya sicho anachomaanisha, Zitto hana shida na uraisi annataka kuvuruga chama na kikishavurugika yeye anakuwa tajiri tayari na anaacha mambo ya siasa na kuendelea na na mambo mengine. Ataacha siasa baada ya kazi yake hiyo kwakuwa anajua atakuwa ameshaharibu CV kwenye ulingo wa siasa.
 
Mkuu Mwita Maranya hivi kama hana sifa na akawa anapita huku na huku akitangaza nia si mnampuuuza tu? Mbona kila akitangaza manakuja juu kuwa anakibomoa chama? Unakumbuka wakati ule Mrema anabebwa na gari lake kusukumwa? Mwalimu alisemaje?

Mimi nadhani Zitto amewasaidia sana kwa kuweka nia yake hadharani kuliko ambao wanafanya mambo chini ya kapeti. Hao ndio wabaya zaidi kwa sababu siku wakiibuka mtakuwa hamkutegemea na watakuwa walishajijenga vya kutosha kimya kimya na hapo ndipo kutakuwa na sintofahamu.

Mkuu hizo sio tabia za CDM.Mwita amefafanua vizuri sana nadhani mtu yeyote makini atakuwa ameelewa.Utamaduni wa CDM hauko hivyo na nadhani kama kuna mtu haridhiki na utamaduni huu milango iko wazi anaweza kwenda popote kunakofanania.Ndani ya CDM hakuna aliye maarufu bali chama ndiyo maarufu.
 
Last edited by a moderator:
Mwasisi wa CHADEMA Edwin Mtei amesema anaamini chama chake kitaingia madarakani mwaka 2015 lakini hilo haliwezi kutokea kama viongozi wake wataanza malumbano na kuwagawa wanachama kwa lengo la kutafuta uungwaji mkono wa Urais.

Amebainisha kuwa CHADEMA kwa sasa hivi ndiyo mkombozi wa wananchi waliochoshwa na utawala wa CCM hivyo ni vema viongozi wake wakatumia muda mwingi kukijenga chama hapa nchini.

Mzee Mtei amesema CHADEMA kina utaratibu mzuri wa kumpata mgombea wa Urais lakini kama viongozi wake wataanza kutoa kauli za kuwania vyeo hivyo kuna kila dalili ya kuzaliwa makundi yatakayokimega chama.

Mzee Mtei amesema yeye aliasisi CHADEMA si kwa lengo la kutafuta vyeo bali alishirikiana na wenzake ili kiwe kimbilio la wanyonge na kiwasaidie kuboresha maisha yao.

Mzee Mtei kwa kauli yake amesema ''Nimemsihi Zitto kuwa kauli yake ya kutaka kuwania urais inabomoa timu yetu kuliko kuijenga na nimemtaka asubiri mpaka chama kitakapoanza mchakato wa wa kumsaka yule atakayepeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu ujao''

Mzee Mtei amesema kuwa Dk Slaa aliteuliwa na vikao vya chama kugombea urais 2010 na ndiyo maana umoja na mshikamano ndani ya chama ulikuwa mkubwa kiasi cha kukifanya Chadema kipate idadi kubwa ya wabunge katika uchaguzi mkuu uliopita.

Mzee Mtei amesema pia alishauriana na viongozi wakuu wa Chama hicho Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa kwamba wakati huu si wa kuwaza Urais bali wa kukifikisha Chadema vijijini na mijini ambako wananchi wanahitaji ukombozi.

Mzee Mtei alimalizia kwa kusema..''Unaweza kutangaza nia ya kuwania Urais lakini tujiulize kwanini sasa? Kwanini tusiutumie muda mwingi kujenga timu ya kuiunganisha Chadema badala ya kuisambaratisha?

Source: DIRA ya Mtanzania.

Hateuliwi huko amabae hana ujamaa wa karibu na Mtei au Kanisa, labda mpaaka huyo Mzee akiuaga.
 
Mkuu hizo sio tabia za CDM.Mwita amefafanua vizuri sana nadhani mtu yeyote makini atakuwa ameelewa.Utamaduni wa CDM hauko hivyo na nadhani kama kuna mtu haridhiki na utamaduni huu milango iko wazi anaweza kwenda popote kunakofanania.Ndani ya CDM hakuna aliye maarufu bali chama ndiyo maarufu.

Zitto anasema ameingia chamani akiwa na miaka 14! Amekijenga chama. Nadhani anataka ale matunda!
 
Back
Top Bottom