Niliasisi CHADEMA si kwa lengo la kutafuta vyeo - Edwin Mtei

Kitu kikubwa kilichonifanya nimdharau kabisa Zito ni hii ya kauli ya kuonesha anavyohangaika na kuutaka Urais. Mtu ambaye hawezi kupima anachozungumza kina madhara gani, japo si kosa kutamka, lazima awe na upungufu mkubwa wa hekima. Zito hana hekima ndiyo maana hana uwezo wa kujua kauli za kumjenga na kumbomoa. Asiye na hekima hafai kuwa kiongozi mkuu.

Hapo kwenye wekundu:

Kwani wanaotangaza kwamba watagombea urais kupitia CDM (Kama Zitto) wamesema kwamba watajiteua? Namsikia kila siku Zitto akisema "...kama nitapata ridhaa ya chama changu...." Hii inadhihirisha kwamba atatafuta ridhaa ya chama chake (CDM).
 
Wana CCM mnafurahia sana hili saga likiendelea maana ni advantage kwenu, bahati mbaya Zitto hajalitambua hili, hebu apitie humu jukwaani aone vijana wa CCM wanavyoshabikia kisha apate funzo ni siasa za aina gani anafanya!!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu uzee ni dawa.Mzee Mtei ni Jabali la kisiasa na kapitia mambo mengi.Mungu amlinde mzee huyu.

tunataka wazee kama hawa !!!! well articulated in his speeches.
The dry bones shall rise again.May God almighty grant him relief and breakthrough in his elderly age!!!
 
Mtei+Padri+ chadema= udini
Zitto hata ukichaguliwa na cdm kugombea urais kura za waislam hupati tunajua kilicho nyuma ya chadema
 
Umtumwa, umeziba milango ya kuelewa alichokisema mzee Mtei. Nimshakugundua uko upande gani?

Sa ukishanigundua niko upande gani unafanya nini? au ugunduzi wako unakusaidia nini?! Tukiwa na hulka ya kumuona kila mtu anayekosana kimtazamo na wanaChadema wenzie basi si mmoja wao..na yuko upande mwingine, tunajitofautishaje na CCM ambao kutwa-kuchwa wanachimbia mikwara wanachama wao walio na mtazamo tofauti?!
 
Kutangaza nia ya kuwania uraisi huku ukitambua huna sifa ya umri kwa mujibu wa katiba ya sasa na wakati ambapo si kipaumbele cha chama ni sawa na kutangaza nia ya kukibomoa.

Demokrasia si kufanya kitu chochote unachojisikia wakati wowote pasipo kuzingatia maslahi ya chama. Tukikubali kufanya demokrasia ya aina hiyo tutakuwa tunaendekeza ubinafsi badala ya maslahi mapana ya umma.

Mkuu na ndiyo maana sakata hili tu lilipoanza nilisema maneno yafuatayo....DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO.
 
Mzee Mtei hana lolote hakuna kinachomsukuma kufanya hivyo icpokuwa udini 2 aliokuwa nao ww hukumbuki alichokisema kuhusu 2me ya ukusanyaji wa maoni ya katiba eti waislamu ni wengi ktk 2me ukilinganisha na wakristo. Sasa povu linamtoka kisa 2 Zitto(muislam) kutangaza nia ya kugombea urais. Think great guys acheni upuuzi.

Ukiwa na haya mawazo usitegemee kama utaweza kuleta ukombozi wa nchi yetu. Hata mkuu wa kaya alikuwa na mawazo kama yako angalia sasa anavyopata shida katika kufanya maamuzi na jinsi kila mtu anavyojuchukulia sheria mkononi bila kuchukuliwa hatua. Natamani ungebadilika uvae uzalendo zaidi na siyo ushabiki kama unavyoonyesha hapa.
 
Mtei+Padri+Chadema=Udini

Na ndiyo maana tunasema wote wanaoshabikia ujinga huu ni wafuasi wa Magamba.Poleni na nawaambia Mzee Mtei akiwa anapumua kamwe hatakubali kuona chama chake kikivurugwa na vibaraka.
 
Mtei+Padri+ chadema= udini
Zitto hata ukichaguliwa na cdm kugombea urais kura za waislam hupati tunajua kilicho nyuma ya chadema

Kama ni kweli jibu lako linaana kubwa zaidi yaani akili.


..
Sasa angalia kinyumeche.....Ponda X Ubwabwa X Magamba = Ujuha







..










..
 
Kama ni kweli jibu lako linaana kubwa zaidi yaani akili.


..
Sasa angalia kinyumeche.....Ponda X Ubwabwa X Magamba = Ujuha







..










..
Mkuu wangu hawa watu ni wa ajabu sana ndiyo maana nasema,
Mtu yeyote anayeleta udini kwenye masuala ya msingi namchukulia kama Punguani.
 
Mzee kaongea ukweli mtupu kuwa huu siyo muda wa kuitafuta ikulu, kama wewe ni wa ikulu utakuwa wa ikulu tu, chama bado hakijajengwa vijijini kabisa, kwanini hawajamaa wapenda/mpenda IKULU hawashiriki kwenye M4C mara kwa mara?? Nendeni vijijini mkajenge chama siyo kukaa tu kutafuta taarifa na kuandika magazetini.
 
Mwasisi wa CHADEMA Edwin Mtei amesema anaamini chama chake kitaingia madarakani mwaka 2015 lakini hilo haliwezi kutokea kama viongozi wake wataanza malumbano na kuwagawa wanachama kwa lengo la kutafuta uungwaji mkono wa Urais.

Amebainisha kuwa CHADEMA kwa sasa hivi ndiyo mkombozi wa wananchi waliochoshwa na utawala wa CCM hivyo ni vema viongozi wake wakatumia muda mwingi kukijenga chama hapa nchini.

Mzee Mtei amesema CHADEMA kina utaratibu mzuri wa kumpata mgombea wa Urais lakini kama viongozi wake wataanza kutoa kauli za kuwania vyeo hivyo kuna kila dalili ya kuzaliwa makundi yatakayokimega chama.

Mzee Mtei amesema yeye aliasisi CHADEMA si kwa lengo la kutafuta vyeo bali alishirikiana na wenzake ili kiwe kimbilio la wanyonge na kiwasaidie kuboresha maisha yao.

Mzee Mtei kwa kauli yake amesema ''Nimemsihi Zitto kuwa kauli yake ya kutaka kuwania urais inabomoa timu yetu kuliko kuijenga na nimemtaka asubiri mpaka chama kitakapoanza mchakato wa wa kumsaka yule atakayepeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu ujao''

Mzee Mtei amesema kuwa Dk Slaa aliteuliwa na vikao vya chama kugombea urais 2010 na ndiyo maana umoja na mshikamano ndani ya chama ulikuwa mkubwa kiasi cha kukifanya Chadema kipate idadi kubwa ya wabunge katika uchaguzi mkuu uliopita.

Mzee Mtei amesema pia alishauriana na viongozi wakuu wa Chama hicho Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa kwamba wakati huu si wa kuwaza Urais bali wa kukifikisha Chadema vijijini na mijini ambako wananchi wanahitaji ukombozi.

Mzee Mtei alimalizia kwa kusema..''Unaweza kutangaza nia ya kuwania Urais lakini tujiulize kwanini sasa? Kwanini tusiutumie muda mwingi kujenga timu ya kuiunganisha Chadema badala ya kuisambaratisha?

Source: DIRA ya Mtanzania.
Kila mmoja akitangaza nia itakuwa vurugu,kambi zitaundwa na tutaachana na malengo ya chama tutajikita kwenye narrow interests.Hiki ndicho CCM wanachotaka na hata maadui wa Chadema.Hapa sasa tuwe makini,kama mtu alishatangaza haina haja ya kuzua headlines kila siku na kuwafanya watu waachane na ajenda nzito
Kama kweli alilolisema Mzee mtei lina heri basi wamuunge mkono ZITTO apeperushe bendera ya CDM mwaka 2015 kwa vile tayari yeye ameonesha nia, na kama ni unafiki wa kutaka kumpalilia njia mkwe wake hakika patachimbika.

Demokrasia ya kuonyesha nia,inatosha?
 
Mkuu Molemo palilieni demokrasia ndani ya Chama. Watu wajitokeze mapema watangaze nia zao tuwajue kwa matendo yao.
kwa maneno yako wewe ni sawa kwako mtu kubanwa haja kubwa wakati chakula kiko mezani na akaamua kwenda chooni kwanza then akarudi kuja kula, sidhani kama ni uamuzi mzuri kwa mtu mwenye akili timamu, kila kitu na wakati wake, kutangaza kugombea urais wakati chama kina shughuli nyingine za maana si sahihi, suppose kila mwanachama aanze kutangaza kugombea si urais tu hata nafasi zingine za kuchaguliwa kitakuwa chama hiki kweli? acha ushabiki reja reja wa kijinga!
 
Kila mmoja akitangaza nia itakuwa vurugu,kambi zitaundwa na tutaachana na malengo ya chama tutajikita kwenye narrow interests.Hiki ndicho CCM wanachotaka na hata maadui wa Chadema.Hapa sasa tuwe makini,kama mtu alishatangaza haina haja ya kuzua headlines kila siku na kuwafanya watu waachane na ajenda nzito


Demokrasia ya kuonyesha nia,inatosha?

Mkuu Ben,
I have nothing to Add here...
 
Back
Top Bottom