Niliasisi CHADEMA si kwa lengo la kutafuta vyeo - Edwin Mtei

Molemo umesema kweli kabisa,kabla ya kufanya tathimin ya nini mafanikio ya kukieneza chama vijijini kupitia M4C,mwingine anahangaika na kugombea urais maana yake nini?Kipindi ni cha kukieneza chama zaidi vijijini bila ya hivyo hamna kitu.
 
Amenena vyema mzee Mtei maana hakika kwa sasa ni kulivuka daraka kabla hata ya kulifikia. Subira na hekima ni muhimu sana kwenye kuweka nia, hata kuku hachinjwi wakati wa kutotoa bali huachwa kwanza mpaka amalize kutotoa! Mchakato wa katiba mpya ungeachwa kwanza uendelee ili kama umri utashushwa vijana wenye nia iwe mujarabu kwao. Sio uko Tanga halafu useme "nataka kwenda pemba kwa gari wakati hata daraja hakuna"

Lakini lingine kubwa ni busara ya kuongeza juhudi za kukijenga chama badala ya kujenga nyufa za kushinda kwenye media na kutangaza nia ya uraisi. Huu ni wakati wa kukieneza chama vijijini ili kuja kupata wapiga kura wengi wa vijijini ambao hawaja fikiwa, mimi nashangaa wengine hata ala za kuhifadhia kisu hawana lakini wanaamkia jf na ku ng'ang'ania kuweka kisu kiunoni huku wakichutama!

Well said mzee Mtei!
 
Ni vema zitto awe na subira mda ukifika akakane ndani ya chama.
 
Hekima za Mzee Mtei ni lulu, pengine Mzee Mtei asingeongea hivi endapo John Shibuda angetangaza nia ya kugombea uraisi kupitia Chadema, bila shaka kuna masuala ambayo Mzee Mtei anayajua na sisi hatuyajui ndio maana anarudia hii kauli yake kwa mara ya pili, wakati mwingine waandishi wawaulize hawa wazee sababu zinazowasukuma kubomoa kabati zao za ushauri na kuongea falsafa za maana kama hivi.

Mzee Mtei hana lolote hakuna kinachomsukuma kufanya hivyo icpokuwa udini 2 aliokuwa nao ww hukumbuki alichokisema kuhusu 2me ya ukusanyaji wa maoni ya katiba eti waislamu ni wengi ktk 2me ukilinganisha na wakristo. Sasa povu linamtoka kisa 2 Zitto(muislam) kutangaza nia ya kugombea urais. Think great guys acheni upuuzi.
 
Mzee wewe ni Lulu kwa sababu isingekuwa wazo lako tusingekuwa na CHADEMA ambayo sasa ni mkombozi hawa ccm & co wanaothubuti kukunyooshea kidole wakati wewe ndiyo umeasisi kile wanacokipigiania leo. HONGERA Mzee
 
Tuangalie na upande wa pili wa shilingi...kwa nini kutangaza nia kwa Zitto kuchukuliwe kama njia ya kutaka 'kuisambaratisha' Chadema? Hivi kila kiongozi, mwanachama, shabiki/mpenzi wa Chadema angeichukulia kama kauli ya kawaida labda kumpongeza Zitto kwa kutangaza nia then tukasahau tukisubiri wakati muafaka mchakato utakapoanza..kungekuwa na malumbano yanayotishia 'kusambaratisha' Chadema?
Tatizo tunampa Zitto uzito mkubwa (overrate) hasiostahili...zikipigwa kura za maoni nani awe candidate wa uRais Chadema Zitto hatatokea kama favourite...hizi kura zinazoendelea hapa JF kati ya Dr Slaa na Zitto zinaonyesha jinsi Dr alivyomuacha kwa mbali. Kwa nini wanaChadema tuchachawe na kudhani Zitto anatishia kusambaratika kwa Chadema?

Mkuu kuiondoa CCM madarakani si kazi ndogo hasa kwa siasa za Kiafrika tena Tanzania! CDM kinakazi kubwa kufika vijijini na mijini kwa kutengeneza mtandao mkubwa na wa uhakika.Kimuundo CDM bado kina kazi ya kujenga timu level za mitaani itakayoweza kuitikisa vilivyo CCM.

Tuna lengo kuu la kuitoa CCM madarakani na unahitajika mshikamano mzito haswa,Kiongozi mkubwa kabisa ndani ya Chama tena kibaya zaidi akiwa records zilizowahi kuwachanganya wanachama na wananchi kwa kwenda kinyume na collective responsibility iliyoamuliwa na chama akiwemo yeye kuamua sasa tena kwa nguvu kubwa kutangaza nia za kugombea Urais inabomoa zaidi kuliko kujenga na hilo ndilo linalotokea sasa hadi tunatofautiana!

Kutangaza nia inaambatana na matayarisho binafsi kugombea,je unafikiri kutakuwa na mshikamano na wengine wenye nia hiyo pia? Tusijifanye hatuoni mgawanyiko unaoweza kutokea kwa kila mwanachama kusimama na yule anayeamini ndiye kiongozi mzuri.

Haya mambo ya Urais ndiyo yaliyoifikisha CCM hapa ilipo toka 1995 na level za mgawanyiko umeshamshinda hata Rais.Hatuwezi kuishinda CCM tukiwa na akili mbili na ukomavu wa siasa (hasa kwa sisi wanachama iwe CDM au CCM) bado ni mdogo sana(haijalishi elimu yako) hivyo ku handle wanachama tena waliolelewa na misingi ya Ki CCM inataka umakini mkubwa na si kufikiri wote wanauelewa sawa ndio maana wanaokuja na hoja ya faida ya kumjua mgombea mapema wanafikiri kwa level za uelewa wao bila kujua uelewa wetu wanachama na wananchi kwa ujumla hasa democrasia ya vyama vingi na uchaguzi huru ukiwa ndio kwanza unapata mwamko wa wananchi.

Bila majemadari wetu wanaoongoza mapambano kuing'oa CCM madarakani kuwa wamoja ki malengo bila hila wala unafiki CCM itaongoza miaka 50 mingine!
 
Hapo kwenye wekundu:

Kwani wanaotangaza kwamba watagombea urais kupitia CDM (Kama Zitto) wamesema kwamba watajiteua? Namsikia kila siku Zitto akisema "...kama nitapata ridhaa ya chama changu...." Hii inadhihirisha kwamba atatafuta ridhaa ya chama chake (CDM).

Mbona unaandika kama wewe ni msemaji wa Zitto ??
Zitto kasema kuhusu chama chake, ila wewe unafafanua zaidi kwa niaba ya Zitto kuwa chama chake ni Chadema !!
Sasa Zitto kakwambia kuwa chama chake ni Chadema ??
attachment.php
 

Attachments

  • zitto-na-jk1.jpg
    zitto-na-jk1.jpg
    62.7 KB · Views: 139
right message from an old man on the right time for the right things.
It iz an objective truth from an outstanding figure who sees beyond limit and horizon where others fail!!!!
 
right message from an old man on the right time for the right things.
It iz an objective truth from an outstanding figure who sees beyond limit and horizon where others fail!!!!

Mkuu wangu uzee ni dawa.Mzee Mtei ni Jabali la kisiasa na kapitia mambo mengi.Mungu amlinde mzee huyu.
 
TAFAKARI

Katiba Ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Sehemu ya Uongozi na kazi zao Ngazi ya Taifa

7.7 NGAZI YA TAIFA
7.7.1 Ngazi hii itaundwa kwa eneo lote la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
7.7.2 Ngazi ya Taifa itaundwa kwa kuzingatia masharti ya Kanuni za Chama zilizotungwa na
Baraza Kuu.
7.7.3 Viongozi Wakuu wa Ngazi ya Taifa watakuwa wafuatao:
(a) Mwenyekiti wa taifa
(b) Makamu Mwenyekiti Bara
(c) Makamu Mwenyekiti Zanzibar
(d) Katibu Mkuu
(e) Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
(f) Naibu Katibu Mkuu (Bara)
7.7.4 Kutakuwa na Kurugenzi za Utendaji Makao Makuu ya Chama zitakazoundwa na Kamati
Kuu kutokana na mahitaji ya Chama.
7.7.5 Kutakuwa na mfumo wa ulinzi na usalama wa mali, viongozi na maslahi ya chama
utakaotambulika kama Brigedi Nyekundu (Red Brigade).
7.7.6 Kamati Kuu inaweza kuongeza au kupunguza idadi ya kurugenzi kadri ya mahitaji
7.7.7 Ngazi ya Taifa itakuwa na vikao vifuatavyo:-
(a) Mkutano mkuu wa Taifa
(b) Baraza Kuu
(c) Kamati Kuu
(d) Sekretarieti ya Kamati Kuu
7.7.8 Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa watakuwa wafuatao:-
(a) Wajumbe wote wa Kamati Kuu
(b) Wajumbe wote wa Baraza Kuu
(c) Wenye viti wa Wilaya/Majimbo
(d) Makatibu wote wa Majimbo/Wilaya
(e) Wajumbe ishirini watakaochaguliwa na Mikutano Mikuu ya kila Baraza la chama
kuingia kwenye Mkutano Mkuu Taifa kwa uwiano ufuatao:-
1 Wajumbe kumi na tano kutoka Tanzania Bara
2 Wajumbe wa tano kutoka Tanzania Zanzibar kwa kila baraza
(f) Mjumbe Mwakilishi wa kila Wilaya
7.7.9 Mkutano Mkuu Taifa utakutana mara moja katika kipindi cha miaka mitano. Mikutano
Mikuu maalum / dharura inaweza kuitishwa wakati wowote ikiwepo ulazima kwa
utaratibu utakaowekwa na Kanuni.
7.7.10 Kazi za Mkutano Mkuu wa Taifa ni:-
(a) Kuchagua Mwenyekiti wa Chama Taifa na Makamu wake wawili
(b) Kujadili taarifa za Baraza Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwa utekelezaji.
(c) Kuteua mgombea wa Uraisi na mgombea wenza wake kwa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na mgombea Urais wa Zanzibar.
(d) Kujadili na kuridhia Itikadi, falsafa na sera za Chama kisha kuweka mikakati na
miongozo ya utekelezaji.
(e) Kujadili na kuridhia programu ya Chama kwa kuzingatia mapendekezo ya Baraza
Kuu.
(f) Kuzingatia na kutoa maamuzi juu ya rufaa na masuala ya kinidhamu
yanayowakilishwa na Baraza kuu.
(g) Kupokea na kujadili taarifa ya Bodi ya wadhamini wa Chama juu ya mali na
rasilimali za Chama
(h) Kuidhinisha Ilani (Manifesto) ya Chama kwa uchaguzi mkuu.
(i) Kuthibitisha mapendekezo ya kuunda tume maalum kama yalivyowalishwa na
Baraza Kuu.
(j) Kujadili na kufanyia maamuzi agenda nyingine yeyote iliyoletwa kwake na Baraza
Kuu.
(k) Kujadili na kuthibitisha mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba ya Chama.
7.7.11 Wajumbe wa Baraza Kuu la Taifa watakuwa:
(a) Wajumbe wote wa Kamati Kuu.
(b) Wenyeviti wa Baraza la Uongozi, Mikoa.
(c) Wajumbe wateule wasiozidi sita watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa kwa
kushauriana na Katibu mkuu na kuidhinishwa na baraza kuu. Wajumbe wateule
hawa watateuliwa kwa uwiano wa wajumbe wanne wanaume wawili na wanawake
wawili.
(d) Wajumbe watano watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa kila Baraza la Chama,
kwa uwiano wa wajumbe wanne toka Bara na mmoja toka Zanzibar kwa kila Baraza.
(e) Wenyeviti wa wilaya za chama
(f) Mwakilishi wa jimbo na chama
7.7.12 Baraza Kuu la Taifa litakutana angalau mara moja kila mwaka. Vikao maalum/dharura
vinaweza kuitishwa kadri itakavyolazimu kwa mujibu wa kanuni za Chama.
7.7.13 Kazi za Baraza Kuu zitakuwa:-
(a) Kupendekeza wagombea wa Urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na kuwasilisha mapendekezo yake katika
mkutano mkuu kwa uamuzi.
(b) Kumchagua Katibu Mkuu miongoni mwa majina mawili yatakayopendekezwa na
Mwenyekiti Taifa.
(c) Kuwachagua manaibu katibu wakuu miongoni mwa majina mawili mawili kwa kila
naibu yatakayopendekezwa na Mwenyekiti Taifa.
(d) Kuchagua wajumbe wa nane kuingia kwenye Kamati Kuu. Kwa uwiano ufuatao:-
• Wanaume watatu na wanawake watatu kutoka Tanzania Bara na angalau mmoja
awe mlemavu
• Mwanaume na Mwanamke mmoja kutoka Tanzania Zanzibar
(e) Kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya rufaa za uchaguzi na za kinidhamu kutoka ngazi
za chini.
(f) Kujadili mikakati ya uendeshaji wa shughuli za Chama kwa kipindi kati ya mkutano
mkuu na mkuu mkutano na kuifanyia maamuzi panapostahili.
(g) Kuthibitisha mikakati na rasilimali za kuendesha kampeni za wagombea wa Chama
katika chaguzi za serikali hususani uchaguzi Mkuu na uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
(h) Kuandaa ratiba na maelekezo ya uchaguzi wa kichama kwa mujibu wa Katiba na
Kanuni za Chama .
(i) Kutunga na kuzifanyia marekebisho kanuni za kuendesha shughuli za Chama.
(j) Kujadili taarifa za Kamati Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwa utekelezaji.
(k) Kusimamia utendaji kazi wa Kamati Kuu.
(l) Kupendekeza kwa Mkutano Mkuu masuala yote ya Katiba ya Chama na mabadiliko
yake.
(m) Kujadili rasimu ya Ilani (Manifesto) ya uchaguzi kwa Uchaguzi Mkuu na uchaguzi
wa Serikali za Mitaa kuwasilisha mapendekezo yake kwa mkutano Mkuu kwa
maamuzi.
(n) Kusimamia chaguzi za Chama ngazi za Jimbo/Wilaya.
(o) Kuteua wadhamini wa Chama.
(p) Kusimamia utekelezaji na uzingatiaji wa maadili ya Chama.
(q) Kuthibitisha kanuni za uendeshaji Chama na miongozo ya Mabaraza ya Vijana,
Wanawake na Wazee.
(r) Kumwachisha ujumbe wa Baraza Kuu mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume na
Katiba, kanuni na maadili ya Chama ama hatakidhi matakwa ya kuteuliwa kwake.
(s) Kuthibitisha wa majimbo ya chama
7.7.14 Wajumbe wa Kamati Kuu watakuwa:-
(a) Mwenyekiti waTaifa
(b) Makamu Mwenyekiti Bara.
(c) Makamu Mwenyekiti Zanzibar
(d) Katibu Mkuu
(e) Naibu Katibu Mkuu Bara
(f) Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
(g) Wawakilishi watano wa Wabunge wa Bunge la Muungano.
(h) Wajumbe watatu toka Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
(i) Wajumbe nane waliochaguliwa na Baraza Kuu kuingia Kamati Kuu kwa uwiano wa
nusu kwa nusu wanaume na wanawake na mjumbe mmoja kutoka kila kundi atoke
Zanzibar.
(j) Wawakilishi watano wa madiwani wa chama, wawili wakiwa madiwani wa kawaida
na watatu wawe Wenyeviti wa Halmashauri zinazoongozwa na Chama. Wajumbe
hawa watachaguliwa na umoja wa madiwani wa Chadema.
(k) Wenyeviti wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee ngazi ya Taifa.
(l) Wajumbe wateule wasiozidi sita watakaoteuliwa na Mwenyekiti Taifa kwa
kushauriana na Katibu Mkuu na kuthibitishwa na Baraza Kuu. Angalau wawili wawe
wanawake.
(m) Wenyeviti Wastaafu wa Chadema.
(n) Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni au Waziri Mkuu atokanaye na Chadema.
(o) Kiongozi wa kambi ya upinzani au Waziri Kiongozi kwenye Baraza la Wawakilishi
atokanaye na Chadema.
(p) Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya Chadema.
(q) Rais wa Zanzibar atokanaye na Chadema
(r) Spika wa Bunge na Spika wa Baraza la Wawakilishi watokanao na Chadema.
(s) Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini atakuwa mjumbe asiye na kura.
(t) Wakurugenzi wa kurugenzi za chama watakuwa wajumbe wasio na kura.
7.7.15 Kamati Kuu itakutana mara nne (4) kwa mwaka. Vikao maalum/dharura vinaweza
kuitishwa kadri itakavyolazimu kwa mujibu wa kanuni za Chama.
7.7.16 Kazi za Kamati Kuu zitakuwa:-
(a) Kufanya utafiti wa wagombea na wa Uraisi na Mgombea Mwenza na kuwasilisha
ripoti zake kwa Baraza kuu kwa ajili ya mapendekezo yake kwa Mkutano Mkuu.
(b) Kuteua Wakurugenzi wa Idara Kuu za Chama Makao Makuu
(c) Kuteua Makatibu wa Wilaya na Mikoa
(d) Kuthibitisha uteuzi wa Sekretarieti za Wilaya.
(e) Kutoa mapendekezo kwa Baraza Kuu juu ya rufaa za uchaguzi na kinidhamu.
(f) Kuandaa na kutoa Mapendekezo kwa Baraza Kuu, Mikakati ya kuendesha shughuli
za Chama kwa kila mwaka na kwa kipindi cha miaka mitano.
(g) Kuandaa na kutoa mapendekezo kwa baraza Kuu , Mikakati ya kupata mahitaji ya
raslimali za kuendesha kampeni za wagombea wa Chama katika chaguzi za kiserikali.
(h) Kuandaa na kutoa mapendekezo kwa Baraza kuu ratiba na maelekezo ya uchaguzi wa
kichama.
(i) Kupitia na kutoa kwa Baraza Kuu mapendekezo ya haja ya kuzifanyia marekebisho
au maboresho Kanuni za Chama ama Katiba ya Chama.
(j) Kujadili taarifa za Sekretarieti ya Kamati Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwa
utekelezaji.
(k) Kusimamia utendaji kazi wa Sekretarieti ya Kamati Kuu
(l) Kufanya mapitio ya Sera za Chama na kutoa mapendekezo kwa Baraza Kuu kwa
kuzingatia matokeo ya Utafiti uliofanywa na Sekretarieti ya Kamati Kuu.
(m) Kusimamia utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Baraza Kuu na Mkutano
Mkuu.
(n) Kuwa kiungo na kudumisha mahusiano mema kati ya Chama na vyama vingine vya
siasa nchini, Afrika Mashariki na nchi nyingine.
(o) Kuthibitisha ajira za watumishi wakuu wa Chama ngazi ya Taifa.
(p) Kuteua kamati au tume za kushughulikia masuala maalum ya kichama kwa muda
maalumu.
(q) Kuteua wakaguzi wa mahesabu ya Chama kwa kila mwaka
(r) Kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge na Baraza la wawakilishi
Zanzibar
(s) Kuandaa agenda za Baraza Kuu na Mapendekezo ya agenda za Mkutano Mkuu.
(t) Kufanya uamuzi juu ya mpendekezo ya kufukuza Mwanachama.
(u) Kuandaa hoja za kupelekwa Bungeni na Wabunge wa Chama
(v) Kumwachisha ujumbe wa Kamati Kuu mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume na
katiba, kanuni na maadili au kushindwa kukidhi matakwa ya kuteuliwa kwake.
(w) Kuratibu utendaji wa ofisi ndogo ya Makao Makuu Zanzibar.
(x) Kusimamia utendaji kazi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee.
(y) Kuteua wajumbe maalum wawili kuingia Kamati ya Utendaji ya Jimbo/Wilaya.
7.7.17 Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu:-
(a) Katibu Mkuu – Mwenyekiti Wa Sekretariat
(b) Naibu Katibu Mkuu Bara
(c) Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
(d) Wakurugenzi wa Idara zote Makao Makuu
(e) Wajumbe watano wataalam watakaoteuliwa na Mwenyekiti kwa kushauriana na
Katibu Mkuu.
(f) Katibu wa Sekretariat atakaeteuliwa na Katibu Mkuu.
(g) Makatibu wa Mabaraza yote ya chama Taifa
7.7.18 Kazi za Sekretariati ya Kamati Kuu
(a) Utekelezaji wa kazi za kila siku za uendeshaji shughuli za chama
(b) Utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Kamati Kuu
(c) Uandaaji wa agenda na nyaraka kwa ajili ya vikao vya Kamati Kuu, Baraza Kuu
na Mkutano Mkuu.
 
Kama kweli alilolisema Mzee mtei lina heri basi wamuunge mkono ZITTO apeperushe bendera ya CDM mwaka 2015 kwa vile tayari yeye ameonesha nia, na kama ni unafiki wa kutaka kumpalilia njia mkwe wake hakika patachimbika.

Watu wa CCM utawajua tu, kazi yenu ni kuchochea udini, ukabila, n.k huku mkiacha nchi ikiporwa mali zake na mafisadi na wawekezaji wa nje.
Chadema hivi sasa iko kwenye zoezi la kupita nchi nzima kuwaelimisha watanzania kuhusu mabadiliko yanayotakiwa hapa Tanzania.
Zitto hashiriki kabisa zoezi hili, yuko busy kusafiri na JK, na kusaka urais wa mwaka 2015 !!!
Sijui urais anaoutaka ataupataje bila ya wananchi nchi nzima kufahamu umuhimu wa kuleta mabadiliko ya kweli !!
Ndio maana anaonekana kuwa ni kibaraka wa CCM ndani ya Chadema, kila siku kazi yake ni kutoa matamko ya kutaka urais !!
Na zaidi kabisa, kuonyesha kuwa Zitto ni kibaraka wa CCM, kila atoapo tamko la kutaka urais, wana-CCM wa JF wataunga mkono sana matamko yake !!
 
Tuangalie na upande wa pili wa shilingi...kwa nini kutangaza nia kwa Zitto kuchukuliwe kama njia ya kutaka 'kuisambaratisha' Chadema? Hivi kila kiongozi, mwanachama, shabiki/mpenzi wa Chadema angeichukulia kama kauli ya kawaida labda kumpongeza Zitto kwa kutangaza nia then tukasahau tukisubiri wakati muafaka mchakato utakapoanza..kungekuwa na malumbano yanayotishia 'kusambaratisha' Chadema?
Tatizo tunampa Zitto uzito mkubwa (overrate) hasiostahili...zikipigwa kura za maoni nani awe candidate wa uRais Chadema Zitto hatatokea kama favourite...hizi kura zinazoendelea hapa JF kati ya Dr Slaa na Zitto zinaonyesha jinsi Dr alivyomuacha kwa mbali. Kwa nini wanaChadema tuchachawe na kudhani Zitto anatishia kusambaratika kwa Chadema?

Mkuu Riwa, ukishatangaza nia ya kuwania uongozi mathalani Urais, kinachofuata ni nini?
 
Mzeee mtei Mungu akubariki sana kwani umekuwa active sana na mwenye maono ya mbali, nakumbuka ushauri wako kuhusu tume ya katiba mpya na watu walikuponda na kukutukana lakini leo tumeona ni kwanini ulisema vile, pia hata hapa kwa huyu kichwa ngumu Zitto bora umempa live koz jamaa hasikii kitu lakin naamin ukweli ameupata hata kama masikio anajifanya amefunga.
 
Zitto anawafanya wenye chama wasipate usingi.kila chama kinapofika chini ndio malengo ya hawa wakanda yanavyoyayuka bila kujua wenyewe,watajiunga wengi na hawatakubali kupelekwapelekwa.zitto kuwa makini hawa wamesoma na wanapesa lkn wachache.
 
Mzee Mtei hana lolote hakuna kinachomsukuma kufanya hivyo icpokuwa udini 2 aliokuwa nao ww hukumbuki alichokisema kuhusu 2me ya ukusanyaji wa maoni ya katiba eti waislamu ni wengi ktk 2me ukilinganisha na wakristo. Sasa povu linamtoka kisa 2 Zitto(muislam) kutangaza nia ya kugombea urais. Think great guys acheni upuuzi.

wewe acha upumbavu wako wa kuchanganya habari, hapa hakuna sijui Zitto dini yake ni mshia au msuni bali hapa tunaongelea ujinga na uwendawazimu wa Zitto kutaka kukigawa chama na urais wake kifallla.
 
Zitto anawafanya wenye chama wasipate usingi.kila chama kinapofika chini ndio malengo ya hawa wakanda yanavyoyayuka bila kujua wenyewe,watajiunga wengi na hawatakubali kupelekwapelekwa.zitto kuwa makini hawa wamesoma na wanapesa lkn wachache.

Wewe CCM badala ya kujenga chama chenu mnakalia majungu ili CDM isambaratike.Mtangoja sana.
 
Hapa mtasababisha hata sisi tusio washabiki tuanze kuogopa siasa ya Tanzania. Katika hali ya kawaida Zitto amechemka kutangaza nia mapema tena wakati M4C yao ikiwa hot yeye kaja na ajenda ya Urais kupunguza makali ya M4C. For real kumwunga mkono huyu jamaa ni kudhoofisha upinzani.
Sasa utabiri wa Wasira utatimia hata kabla ya 2014 kama CDM hawatakuwa makini and its so bad to see this.
 
Zitto anawafanya wenye chama wasipate usingi.kila chama kinapofika chini ndio malengo ya hawa wakanda yanavyoyayuka bila kujua wenyewe,watajiunga wengi na hawatakubali kupelekwapelekwa.zitto kuwa makini hawa wamesoma na wanapesa lkn wachache.

ujinga mtupu umejaza kichwani, ww peleka huko huko udhaifu wa kufikiri kwenye chama lenu CUF lakini si huku wenye kwa maarifa.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom