Mwasisi wa CHADEMA Edwin Mtei amesema anaamini chama chake kitaingia madarakani mwaka 2015 lakini hilo haliwezi kutokea kama viongozi wake wataanza malumbano na kuwagawa wanachama kwa lengo la kutafuta uungwaji mkono wa Urais.
Amebainisha kuwa CHADEMA kwa sasa hivi ndiyo mkombozi wa wananchi waliochoshwa na utawala wa CCM hivyo ni vema viongozi wake wakatumia muda mwingi kukijenga chama hapa nchini.
Mzee Mtei amesema CHADEMA kina utaratibu mzuri wa kumpata mgombea wa Urais lakini kama viongozi wake wataanza kutoa kauli za kuwania vyeo hivyo kuna kila dalili ya kuzaliwa makundi yatakayokimega chama.
Mzee Mtei amesema yeye aliasisi CHADEMA si kwa lengo la kutafuta vyeo bali alishirikiana na wenzake ili kiwe kimbilio la wanyonge na kiwasaidie kuboresha maisha yao.
Mzee Mtei kwa kauli yake amesema ''Nimemsihi Zitto kuwa kauli yake ya kutaka kuwania urais inabomoa timu yetu kuliko kuijenga na nimemtaka asubiri mpaka chama kitakapoanza mchakato wa wa kumsaka yule atakayepeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu ujao''
Mzee Mtei amesema kuwa Dk Slaa aliteuliwa na vikao vya chama kugombea urais 2010 na ndiyo maana umoja na mshikamano ndani ya chama ulikuwa mkubwa kiasi cha kukifanya Chadema kipate idadi kubwa ya wabunge katika uchaguzi mkuu uliopita.
Mzee Mtei amesema pia alishauriana na viongozi wakuu wa Chama hicho Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa kwamba wakati huu si wa kuwaza Urais bali wa kukifikisha Chadema vijijini na mijini ambako wananchi wanahitaji ukombozi.
Mzee Mtei alimalizia kwa kusema..''Unaweza kutangaza nia ya kuwania Urais lakini tujiulize kwanini sasa? Kwanini tusiutumie muda mwingi kujenga timu ya kuiunganisha Chadema badala ya kuisambaratisha?
Source: DIRA ya Mtanzania.