Niletee CV yako haraka!!!! nikafurahi

msani

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
1,801
1,191
katika harakati za kutafuta kazi nilikutana na rafiki yangu ambaye tulisoma naye shule moja olevel,akaamua kunipigia pande kwa jamaa mmoja benki!!
nikaambiwa nipelekee cv haraka,kweli siku ya j3 30/4/2012 mchana huku mvua ikininyeshea nilijikuta maeneo ya posta nikitafuta hiyo benki niweze kumpa jamaa cv yangu,mie nina degree ya finance and investment!!!
jioni yake nilipigiwa simu na rafiki yangu kuwa sijakidhi vigezo vyao kwa kuwa nina D ya english ya olevel,eti nilitakiwa kuwa na angalau C ingawa kwenye kigezo cha hesabu nimefaulu kwani nina B ya olevel na kufanya vizuri kwenye kozi za hesabu za chuo,na pia uwezo wa kufanya kazi ninao kwakweli,ila sbb ya D ya english nimekosa kupewa nafasi!!!!yaani nimeshangaa sana na kuona kuwa wapo wengi wanakosa kazi kwa sbb tu hawa ma-hr ni mbumbumbu wa kutosha!!!!!!sijielewi mpaka sasa maana nikikumbuka nacheka mwenyewe!!!
 
Afadhali kumbe kama unacheka! Mi nilijua utakuwa umehuzunika kwa kukosa job opp.
 
msani usicheke mwenyewe; kama mpo kumi kwenye nafasi moja na degree moja njia ya kuwapunguza ndiyo hiyo
 
Last edited by a moderator:
We hujui tuu hata kama ungekuwa na hiyo c ungeambiwa inatakiwa b yaani ni full maumivu labda alishindwa kukuomba rushwa hapo.
 
Huna vigezo, ndio bottom line wakati wenzako wako class wakula kingredha wewe unazungukia mademu na kuvuta bange..sasa huu ndio wakati wa mavuno.
 
Afadhali kumbe kama unacheka! Mi nilijua utakuwa umehuzunika kwa kukosa job opp.

siwezi kuhuzunika ndg yangu,ila nimecheka kwa sbb zilizotolewa utadhani nilikuwa nimetuma maombi ya kujiunga na chuo,kazi nitapata tu hata kama sio leo basi kesho,sioni sbb ya kuhuzunika kwani kuhuzunika hakunipi kazi mkuu
 
Huna vigezo, ndio bottom line wakati wenzako wako class wakula kingredha wewe unazungukia mademu na kuvuta bange..sasa huu ndio wakati wa mavuno.

dah mkuu umenimaliza kabisa,hahahahaahah yaani hiyo kitu siijui kabisa na sijawahi,sait kayumba labda!!!!
acha kuua namna hiyo bana mie ishakosa kazi kwa hiyo kiigeresaaaa
 
We hujui tuu hata kama ungekuwa na hiyo c ungeambiwa inatakiwa b yaani ni full maumivu labda alishindwa kukuomba rushwa hapo.
siwezi kutoa rushwa kaka,labda hapo ndio pagumu,nitaendelea na shughuli zangu za kitaa mpaka nitakapopata kazi halali ambayo nitaridhika nayo na kuifanya kwa amani
TOKOMEZA RUSHWA KUIJENGA TANZANIA SAFI
 
Huna vigezo, ndio bottom line wakati wenzako wako class wakula kingredha wewe unazungukia mademu na kuvuta bange..sasa huu ndio wakati wa mavuno.

Pamoja na kutoukubaliana na "lugha" uliyotumia hapo kwenye bold, kumfikishia ujumbe huyu mwenzetu, nimefurahi kuwa umegusa penyewe haswa! HANA SIFA/VIGEZO full stop!
Aache kulalamika kama vile ana haki kupanga vigezo vya mwajiri!
Asome zaidi hapa:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-kupata-kazi-partly-tunajitakia-wenyewe.html
 
da comrade nami nina D ya english nimeshtuka sana lakini usijali comrade wataisha wenye c tutabaki wenye D na tutapata kazi tu
 
Unaongea kiingeresa mbofu mbofu pole mpwa

hii engeresa yangu ipo mbovu mkuu,mpaka nikapata D,hii noma ila nshukuru ardhi university walinikubali na kumaliza huku nikijibu mitihani yao yote ndani ya miaka mi4 kwa hii engeresa yangu mbovu....hahahahah pamoja ila ndo changamoto
 
Pamoja na kutoukubaliana na "lugha" uliyotumia hapo kwenye bold, kumfikishia ujumbe huyu mwenzetu, nimefurahi kuwa umegusa penyewe haswa! HANA SIFA/VIGEZO full stop!
Aache kulalamika kama vile ana haki kupanga vigezo vya mwajiri!
Asome zaidi hapa:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-kupata-kazi-partly-tunajitakia-wenyewe.html

Tausi,

Nilikuwa namtania tu huyu mleta uzi, hata yeye mwenyewe ameelewa kuwa ni utani.
Kwa jinsi nilivyomuelewa huyu mtu aliyechukua vyeti na CV ya jamaa ni another msanii tu. Nimeshakutana nao wengi sana kipindi kile nasota kitaa na mavyeti yangu. Kuna watu wanapenda waonekane wanaouezo wa kufukuza na kuajiri ili wapate sifa za kijinga kwa mashori, etc, wakati they don't call shots, ni vidampa tu. Nimeshapotezewa muda na pesa na watu kama hao mara kibao, wengine tena ni ndugu na marafiki. Ndo bongo darisalama, mdau ashukuru tu hakutolewa upepo au hakutapeliwa chochote.
 
hapo alimaanisha tafuta fungu la kusafisha kiingereza uingie kazini mkono mtupu hailambwi
 
Back
Top Bottom