mfianchi
Platinum Member
- Jul 1, 2009
- 11,855
- 8,251
''Nile maharage kwani mi Muha''hii ni kauli ambayo ilipendwa sana kutumiwa miaka ya nyuma na wakazi wa Kunduchi wakati huo njia ya kwenda Bagamoyo ilipita Kawe hadi nyumba za polisi Kunduchi,kauli hiyo ilitokana na wakazi wengi wa Kunduchi wakati huo wakiwa Wazaramo kupendelea kula samaki ambao walikuwepo kwa wingi,hao Waha wanaosemwa walikuwa wanfanya kazi kwenye shamba la mkonge la giriki liliokuwepo kuanzia Tangibovu hadi pale Mbuyuni , vibarua wengi wa hilo shamba walikuwa watu wa kuja kutoka Kigoma ambao ndio walikuwa wengi,na pia ndio walikuwa vibarua kwenye machimbo ya kokoto Kunduchi menu yao kubwa ilikuwa harage na dona.Kwa vijana wa CCM ya Jakaya naona mtashangaa kuwa kuanzia Tangibovu hadi Mbuyuni palikuwa shamba la mkonge,hivi sasa familia ya huyo giriki imebakiwa na kipande cha ardhi kuanzia kona ya Africana hadi Mbuyuni.Hawa Waha ambao walikuwa wanataniwa enzi hizo kwa kula maharage sasa ndio matajiri wa vitongoji vya Tengeta na Kunduchi na wale ambao walikuwa wanajifanya hawali maharage sasa maharage kwao ndio menu kubwa na ndio malofa,ama kweli dunia imebadilika .