Nisaidieni mawazo, niko mpweke sana

Loloo

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
214
54
Jamani wanajamii wenzangu,

Embu nisaidieni mawazo.

Mimi ni binti wa miaka 34 very attractive, nafanya kazi nina elimu yangu na ni mkristu mzuri. Tatizo ni kwamba ninaishi mbali na watu wa familia yangu na mimi sio mtu wa kujichanganya sana, baada ya kuwa na uhusiano na vijana wawili na kukuta ni matapeli nimeamua sitaki tena uhusiano na mwanaume labda awe mchaga mwenzangu ni hi kwa sababu wale matapeli walikuwa wenyeji wa huku ninakoishi.

Tatizo kubwa sasa hivi nimekuwa mpweke sana yani ninataka kuwa mwenyewe muda wote nimepanga nyumba nzima sikai hata na house girl, siendi kwa mtu wala sikaribishi tena mtu kwangu nikitoka kazini sa nane sitoki ndani hadi kesho yake, hata rafiki akiniita out natoa excuse ya uongo, weekend natoka kuosha gari na kusali tu,bat list JamiiForums is my near friend and Jesus whom i talk to everytime.

Je, hii hali ni ya kawaida, nifanye nini?
 
Sweet Baby punguza haraka omba MOD waedit title. BTW. Nitarudi kwa ushauri
 
jamani wana jamii wenzangu embu nisaidieni mawazo.mie ni bint wa miaka 34 very attractive,nafanya kazi nina elimu yangu na ni mkristu mzuri.tatizo ni kwamba ninaishi mbali na watu wa familia yangu,na mie sio mtu wa kujichanganya sana,baada ya kuwa na uhusiano na vijana wawili na kukuta ni matapeli nimeamua sitaki tena uhusiano na mwanaume labda awe mchaga mwenzangu ni hi kwa sababu wale matapeli walikuwa wenyeji wa huku ninakoishi.tatizo kubwa sasa hivi nimekuwa mpweke sana yani ninataka kuwa mwenyewe muda wote nimepanga nyumba nzima sikai hata na house girl,siendi kwa mtu wala sikaribishi tena mtu kwangu nikitoka kazini sa nane sitoki ndani hadi kesho yake,hata rafiki akiniita out natoa excuse ya uongo wkend natoka kuosha gari na kusali tu,at list jamii forum is my near friend and Jesus whom i talk to everytime..je hi hali ni ya kawaida.?nifanye nini?

Oh dear....well....let me PM you
 
Pole sana..! Unahitaji kufikiria upya uhusiano wako na Mungu.. Sidhani kama Yesu ni mbaguzi kiasi hiko..Mie nakushauri ujitahidi kuimarisha uhusiano upya na Yesu, ninaamini unajua kuwa yeye ndo anapanga na kupangua..

Pia kama wewe umeshindwa kujua kama ni kawaida au sio kawaida, sisi wengine itatuwia vigumu, kwa sababu huenda hayo maisha ndo umeyachagua..

Kila mtu anaumizwa katika maisha. Hakuna aliye salama. Kuna wengine wamejiua kabisa, na wengine kuwa vichaa. Umshukuru Mungu uko hai na unafanya kazi vizuri pamoja na mambo mengine..Amua kutokuathiriwa na matatizo uliyoyapata. Yafanye kama ndo ngazi ya kupandia kwenda kwenye maisha bora zaidi..Pia miaka 34 kwa mwanamke nadhani kama una mpango wa kuolewa, labda ungekuwa unajichanganya kiasi, hasa hasa huko kanisani.
 
Sweetlady i can only imagine what you are going through. Lakini vipi huko job,unainteract na watu au pia ni m2 wa buyu?na church je?
 
kanisani kwenyewe naenda english mass coz watu sio wengi,waafrica wachache tena watoto, it is as if sitaki kukutana na watu ingawa nature ya kazi yangu ni kukutana na watu wa kila aina.am thinking of finding a transfer nikakae karibu na kwetu
Sounds like una phobia flani sijui ya binadamu?! vipi kuhusu animals,do have pets at home? Don worry u've already taken a step to a big change.hapa hapa jf utapata mwanga
 
jaribu kumuona psychiatric, haupo kawaida kabisa na hiyo ni dalili ya ugonjwa wa akili. ukichelewa sitashangaa umejinyonga kwa upweke.
 
he someone aliniambia kama wewe itnojec lakini namshukuru Mungu hilo wazo halijawahi kunipata na huyo man nilijua anataka kutake advantage sikumpa nafasi huwa nasali sana ,sanasana kuna wakati natamani kuacha kazi niende kukaa kwetu hilo ndo wazo linalojia kila mara ndo mana nafikiria nihamie karibu na kwetu kama itawezekana

ndugu,
umwa magonjwa yote lakini sio upweke...basi jaribu kujichanganya maeneo kama kwenye sports events au kwaya..
 
wewe ni binti miaka 34??acha utani!!wewe ni mwanamke acha mambo ya ajabuuu
 
kwa hiyo kibibi kinaanzia miaka 21 sio?

wee ina maana miaka 34 unajiita binti??mbona mnapenda kuchanganya watu!!!wewee una watoto??kama huna tafuta mtu mapema,akupe mimba uzae mwanao wa kucheza nae!!acha mambo ya ajabu
 
the fact that kuwa kibibi sio dhambi basi i truly admit me kibibi i hope you are content.sure?
 
sina mtoto na sitafuti mtu wa kunipa mimba kwani wew hapo ulipo ushajua Mungu atakupa pumzi ya miaka mingapi kumuhudumia HUYO mtoto wa mkeo?Sara aliza na miaka tisini why should i be wory?USIJALI KAKA YANGU ME NI BINTI MWENYE SURA NA NAJIHESHIMU SANA NINGETAKA KUOLEWA HATA KESHO BUT I HAVE MY BELEIF AND MALENGO MBONA WANAOTAKA KUNIOA HATA KESHO NI WENGI TU ILA CJAPATA WA KUFANAN NAE.
 
sina mtoto na sitafuti mtu wa kunipa mimba kwani wew hapo ulipo ushajua Mungu atakupa pumzi ya miaka mingapi kumuhudumia HUYO mtoto wa mkeo?Sara aliza na miaka tisini why should i be wory?USIJALI KAKA YANGU ME NI BINTI MWENYE SURA NA NAJIHESHIMU SANA NINGETAKA KUOLEWA HATA KESHO BUT I HAVE MY BELEIF AND MALENGO MBONA WANAOTAKA KUNIOA HATA KESHO NI WENGI TU ILA CJAPATA WA KUFANAN NAE.

kufanana naye nini??sura au nini??mbona mna mambo ya ajabu sana nyie?
 
Pole mpenzi, sote tunatendwa kwenye maisha...lakini tunassamehe na kuzidi kupenda na kutenda mema. Usiwaogope binadamu,yapaswa uwe karibu na watu walau wachache unaowaamini na kuwapenda. Inachosha akili na kuzeesha kuwa mpweke hivyo.ushauri wangu, tafuta marafiki wachache mnaoheshimiana na wanaompenda Mungu kama wewe,zungumza nao,shiriki kwenye activities kama lunch,dinner,movie au hata shopping na wao.Utajifunza mengi,utajiona mwenye thamani zaidi na wao pia wataona u rafiki mzuri. Mungu akutunze na akupe ushindi na akuondolee hofu zozote zile na zaidi akupe mwenza anayestahili mdada wa thamani yako.AMEN!
 
Back
Top Bottom