Niko dillema, mchumba wangu ni mchawi!!!

wasalaam MMU!

kama ni kuchanganyikiwa ndo nahisi nachanganyikiwa!!
Katika pitapita zangu na kujituma kwangu kumsaka mchumba ambae ni mzuri nilibahatisha kumpata mtoto wa makabila mmojawa maarufu sana ktk mkoa wetu wa Arusha.
Mtoto mwenyewe si haba, mtoto mweupeee!!
Mtoto wezereee!!
Mtoto unywele!!
Mtoto smile!!
Mtoto meno meupeee!!
Mtoto mguu!!
Dahhhh!!

na kiukweli nilikuwa nikipita nae kila mahali masela nilihisi kama kuna ka uhasama mfali, kina dada walininunia bila sababu kisa kuwaambia ukweli kuwa my hny yre(wayre nilipenda kumwita hivo) kauteka moyo wangu na naahidi kumpenda kwa dhati!!!

Looo! Kuna taarifa ambazo nimeanza kuzipa kutoka kwa marafiki zangu wa mtaani kwao kwamba ile familia ni issue, mama wao aliwahi kumuua mumewe na 7bu zingine kibao zikiwa ni pamoja na kutokuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume majirani zao!!

Sasa mi nitafanyeje? Kama hizi taarifa ni kweli nikijifanya naendelea nae nitaishia wapi?

Naombeni ushauri wenu wapenzi wenzangu wa jf hasa MMU.

ahsanteni.


1. Hujaeleza huyo mama alimuuaje mumewe ili tutafakari hayo mazingira ya uchawi
2. Na je, angekuwa amemaliza wanaume mtaa mzima(wakiwemo hao rafikizo), ndio ungekuwa na amani naye?
3. Pengine ulowauliza wana visa na familia husika,si wapo mtaa mmoja.?
4. Pengine huyo jamaa yako alikataliwa na huyo binti?

Ushauri wangu
1. Jifunze kufanya maamuzi kwa kutumia ushahidi ie data kamili
2. Usiwe na papara,fuatilia na kuuliza kwa watu wengine zaidi ya huyo rafikiyo.
3. Kunywa soda hata maduka ya jirani na kwao huku ukidodosa taarifa za binti na familia yake
4. Tafuta hata mtu mzima wa jirani na kwao(ambaye si rafiki na familia yao,ila pia si adui),tumia busara na akili kuhoji taarifa unazohitaji kujua
 
1. Hujaeleza huyo mama alimuuaje mumewe ili tutafakari hayo mazingira ya uchawi2. Na je, angekuwa amemaliza wanaume mtaa mzima(wakiwemo hao rafikizo), ndio ungekuwa na amani naye?3. Pengine ulowauliza wana visa na familia husika,si wapo mtaa mmoja.?4. Pengine huyo jamaa yako alikataliwa na huyo binti? Ushauri wangu1. Jifunze kufanya maamuzi kwa kutumia ushahidi ie data kamili2. Usiwe na papara,fuatilia na kuuliza kwa watu wengine zaidi ya huyo rafikiyo.3. Kunywa soda hata maduka ya jirani na kwao huku ukidodosa taarifa za binti na familia yake4. Tafuta hata mtu mzima wa jirani na kwao(ambaye si rafiki na familia yao,ila pia si adui),tumia busara na akili kuhoji taarifa unazohitaji kujua
Asante sana, nimekupata na nitajaribu kuufuatilia na kuufuata ushauri wako.ila kwa kukujibu swali lako la kutaka uthibitisho, si mtu mmoja au wawili, so kama binadamu mwenye kuogopa kifo lazima nishtuke.
 
Looo! Kuna taarifa ambazo nimeanza kuzipa kutoka kwa marafiki zangu wa mtaani kwao kwamba ile familia ni issue, mama wao aliwahi kumuua mumewe na 7bu zingine kibao zikiwa ni pamoja na kutokuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume majirani zao!!

Sasa mi nitafanyeje? Kama hizi taarifa ni kweli nikijifanya naendelea nae nitaishia wapi?

Hivi unaweza kumhukumu mtu kwa kusikiliza majungu...................................hadi sasa unategemea ya kuwa taarifa hizo ni za kweli....................mama yake kama kweli kamwua baba yake bado haimaanishi na uzao wao umekithiri kwa uchawi............................
na kutokuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume majirani zao

Hivi hii nilifikiri ni sifa ya kuwa kumbe umepata kijiwe cha kuzamia nacho moja kwa moja........................hivi ulikuwa wataka mwandani ambaye amekithir kwa mahusiano na wanaumme?....................au una maana tofauti ya hiyo.........................
 
1. Hujaeleza huyo mama alimuuaje mumewe ili tutafakari hayo mazingira ya uchawi
2. Na je, angekuwa amemaliza wanaume mtaa mzima(wakiwemo hao rafikizo), ndio ungekuwa na amani naye?
3. Pengine ulowauliza wana visa na familia husika,si wapo mtaa mmoja.?
4. Pengine huyo jamaa yako alikataliwa na huyo binti?

Ushauri wangu
1. Jifunze kufanya maamuzi kwa kutumia ushahidi ie data kamili
2. Usiwe na papara,fuatilia na kuuliza kwa watu wengine zaidi ya huyo rafikiyo.
3. Kunywa soda hata maduka ya jirani na kwao huku ukidodosa taarifa za binti na familia yake
4. Tafuta hata mtu mzima wa jirani na kwao(ambaye si rafiki na familia yao,ila pia si adui),tumia busara na akili kuhoji taarifa unazohitaji kujua

Hizi hoja zafanana na zile za Asha Dii.............sijui kabughudhiwa na nini hadi katukimbia humu jamvini....................I truly miss her......................na Pauline.......................................labda wametuwekea kamgomo baridi.................lol
 
pole sana! nakushauri ufanye utafiti wa kina juu ya hilo swala, na usipopata ukweli wa jambo ni heri kuachana naye sababu hata kama utataka kuishi naye kwa kupotezea maneno ya watu bado utajikuta unakuwa katika wakati mgumu maisha yako yate kwa hisia za kuw mchumba wako ni mchawi zitaendelea kukutesa siku hadi siku.
 
Asante sana, nimekupata na nitajaribu kuufuatilia na kuufuata ushauri wako.ila kwa kukujibu swali lako la kutaka uthibitisho, si mtu mmoja au wawili, so kama binadamu mwenye kuogopa kifo lazima nishtuke.

Nina ushahidi wa mume aliyefariki kwa ugonjwa wa ukimwi hivyo alikuwa anatumia dose za waathirika(aliyekuwa anajua kuwa kaathirika ni mama,watoto wake na mama mmoja wa jirani).

Huyu mume na mkewe walikuwa na mali nyingi sana,tena walianza kwa maisha ya tabu na mkewe, baadae Mungu akawajalia mali.
Kumbuka hakuwa na dalili yoyote inayoonyesha ya kuwa ni mwathirika.

Ndugu wa mume walikuwa hawaishi kumiminika kwa ndugu yao(si tatizo) ila walikuwa wanamnyanyasa sana huyo mkewe kwa maneno ya hapa na pale yanayohusiana na mali (RED LIGHT)

Wapo waliotaka mitaji,wakipewa pesa wanakula na kurudi kuomba tena(bado walipewa),wapo waliosomeshewa watoto wao n.k

Inasemekana huyu baba alibadili dose,sijui ni kosa gani la kiutaalam lilifanyika, baba akafa ghafla!

Yaliyotokea;
1. Ndugu walidai huyo mama kamuua ndugu yao(yaani mumewe),ie kamloga ili arithi mali.
2. Eneo lote waliloishi uvumi huu ulienezwa hivyo majira wakaitenga familia nzima.
3. Rafiki pekee wa jirani aliyebaki nao alikuwa yule mama anayejua historia nzima ya afya ya yule baba

Jifunze jambo hapa.
 
Nina ushahidi wa mume aliyefariki kwa ugonjwa wa ukimwi hivyo alikuwa anatumia dose za waathirika(aliyekuwa anajua kuwa kaathirika ni mama,watoto wake na mama mmoja wa jirani).Huyu mume na mkewe walikuwa na mali nyingi sana,tena walianza kwa maisha ya tabu na mkewe, baadae Mungu akawajalia mali.Kumbuka hakuwa na dalili yoyote inayoonyesha ya kuwa ni mwathirika.Ndugu wa mume walikuwa hawaishi kumiminika kwa ndugu yao(si tatizo) ila walikuwa wanamnyanyasa sana huyo mkewe kwa maneno ya hapa na pale yanayohusiana na mali (RED LIGHT)Wapo waliotaka mitaji,wakipewa pesa wanakula na kurudi kuomba tena(bado walipewa),wapo waliosomeshewa watoto wao n.kInasemekana huyu baba alibadili dose,sijui ni kosa gani la kiutaalam lilifanyika, baba akafa ghafla!Yaliyotokea;1. Ndugu walidai huyo mama kamuua ndugu yao(yaani mumewe),ie kamloga ili arithi mali.2. Eneo lote waliloishi uvumi huu ulienezwa hivyo majira wakaitenga familia nzima.3. Rafiki pekee wa jirani aliyebaki nao alikuwa yule mama anayejua historia nzima ya afya ya yule babaJifunze jambo hapa.
nakupata vizuri sana, lakini unauamini uchawi? Unaamini kama kuna kitu kinaitwa uchawi na huwa watu wanakufa?
 
Hizi hoja zafanana na zile za Asha Dii.............sijui kabughudhiwa na nini hadi katukimbia humu jamvini....................I truly miss her......................na Pauline.......................................labda wametuwekea kamgomo baridi.................lol

Ngoja nifikishe salaam mkuu,hasa hapo kwenye bold!
 
nakupata vizuri sana, lakini unauamini uchawi? Unaamini kama kuna kitu kinaitwa uchawi na huwa watu wanakufa?

Hiyo ilitakiwa iwe thread ya kujitegemea.ILA,vitabu vya dini vimeainisha kuwa uchawi upo japokuwa hauzidi nguvu za Mungu wa Kweli,aliyetuumba.ie Ukiwa na imani thabiti hasa kwa YESU,hulogeki!

Hili la kufa huwa linanipa kizunguzungu kidogo.niwahi kuona kwenye ile Spora Show ya star tv,mchungaji(ambaye alikuwa mchawi mkuu) akitoa maelezo hivi;


Wachawi wanakuuwa kichawi kwa kuchukua nyayo(unyayo wa mahali ulipokanyaga)
Alisema nyayo ni kivuli chako hivyo ule mchanga unachanganywa na vitu vingine vya kichawi,sijui wanakoroga vipi,halafu muhusika popote alipo anakufa,kwa sababu yoyote ile ya ghafla.

ILA hapo anakuwa AMEKUFA KICHAWI TU,japo ndugu wataona kafa kweli na watazika lakini wanazika vitu vingine,mawe,migomba n.k

Wao wachawi wanamchukua muhusika kichawi,na wataishi naye na kumfanyia watakavyo


Ikifika muda wake wa KUFA KWELI(Kifo tulichoandikiwa binadamu wote),atakufa,na watamzika.Kifo hiki hata wao hawawezi kukikwepa.

PIA alisema wakati akiwa mchawi hakuna walichokuwa wanakiogopa kama JINA LA YESU,watu waliokuwa wanataka kuwaaloga ambao walikuwa na imani thabiti ilikuwa ni changamoto kwao na mara nyingi walishindwa.
 
Hiyo ilitakiwa iwe thread ya kujitegemea.ILA,vitabu vya dini vimeainisha kuwa uchawi upo japokuwa hauzidi nguvu za Mungu wa Kweli,aliyetuumba.ie Ukiwa na imani thabiti hasa kwa YESU,hulogeki!Hili la kufa huwa linanipa kizunguzungu kidogo.niwahi kuona kwenye ile Spora Show ya star tv,mchungaji(ambaye alikuwa mchawi mkuu) akitoa maelezo hivi;Wachawi wanakuuwa kichawi kwa kuchukua nyayo(unyayo wa mahali ulipokanyaga)Alisema nyayo ni kivuli chako hivyo ule mchanga unachanganywa na vitu vingine vya kichawi,sijui wanakoroga vipi,halafu muhusika popote alipo anakufa,kwa sababu yoyote ile ya ghafla.ILA hapo anakuwa AMEKUFA KICHAWI TU,japo ndugu wataona kafa kweli na watazika lakini wanazika vitu vingine,mawe,migomba n.kWao wachawi wanamchukua muhusika kichawi,na wataishi naye na kumfanyia watakavyoIkifika muda wake wa KUFA KWELI(Kifo tulichoandikiwa binadamu wote),atakufa,na watamzika.Kifo hiki hata wao hawawezi kukikwepa. PIA alisema wakati akiwa mchawi hakuna walichokuwa wanakiogopa kama JINA LA YESU,watu waliokuwa wanataka kuwaaloga ambao walikuwa na imani thabiti ilikuwa ni changamoto kwao na mara nyingi walishindwa.
uuuuwi! Kumbe uchawi upo? Sa yre akiwa nao kweli (labda karithishwa na mamaake, ataniacha?
 
uuuuwi! Kumbe uchawi upo? Sa yre akiwa nao kweli (labda karithishwa na mamaake, ataniacha?


Kwa jinsi ulivyojaa hofu..............tayari una IMANI kuwa kweli ni wachawi!Hata ukikuta si kweli baada ya kufanya uchunguzi,maisha yako yatakuwa ya mashaka sana.Homa kidogo,utahisi kakuloga,mafua kidogo,utahisi uelogwa kwani IMANI YAKO ni haba.Yaani umeshakaa kulogwa logwa tuu,nahisi si mkristo thabiti wewe.....

Nakushauri tafuta njia muafaka ya kusitisha mahusiani hayo na si visa."Mchawi mpe mtoto akulelee"!

Naomba kukuuliza,
Ungezaliwa na mama/baba wachawi,ila wewe usiwe mchawi...........ungeoa mke mchawi au ungetafuta aliye thabiti kiimani na kuoa?
 
ushauri sahihi ni muache now..
hisia hujenga jambo ambalo hata kama halipo,we utaliona lipo

uliamini kwao ni wachawi,basi lazima mtakuja kugombana..
chochote kitakachokutokea mbele,hisia zako zitakuwa wana kuroga hata kama sio kweli
so bora umuache now
The boss kwa nini aamini mambo ya kuambiwa? atajuaje kama wamemzushia ili amteme then amchukue yeye?
yote yanawezekana, kama ni mkristo au muislam safi afunge siku saba kwa sala ili apate majibu
 
Kwa jinsi ulivyojaa hofu..............tayari una IMANI kuwa kweli ni wachawi!Hata ukikuta si kweli baada ya kufanya uchunguzi,maisha yako yatakuwa ya mashaka sana.Homa kidogo,utahisi kakuloga,mafua kidogo,utahisi uelogwa kwani IMANI YAKO ni haba.Yaani umeshakaa kulogwa logwa tuu,nahisi si mkristo thabiti wewe.....Nakushauri tafuta njia muafaka ya kusitisha mahusiani hayo na si visa."Mchawi mpe mtoto akulelee"!Naomba kukuuliza,Ungezaliwa na mama/baba wachawi,ila wewe usiwe mchawi...........ungeoa mke mchawi au ungetafuta aliye thabiti kiimani na kuoa?
Dah! Suali gumu. So we unataka niendelee nae kisa yeye asije akakosa mpenz au?
 
Dah! Suali gumu. So we unataka niendelee nae kisa yeye asije akakosa mpenz au?
Hivi wewe unajua uchawi??? angekuroga hata hapa usingekuja kuuliza swali kama hili, na kama kweli mchawi basi sasa hivi keshapata alarm fulani unamteta humu, na ole wako ukutane nae leo utakoma......hahahahaha hakuna kitu kama hicho
 
Fanya utafiti wa kina kuhusiana na taarifa ulizozipokea baada ya kuzithibitisha achana naye lkni kwa muda huu usioneshe ishara zozote mbaya kwa huyo dada kwani huna hakika kwa shut uma ulizozisikia
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom