Nikiwaita wanawake wenye tabia hizi kuwa ni vichaa nitakuwa nimekosea kweli?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,395
Kuna wanawake wengi sana ambao wanagombea kupendwa, au wanajipendekeza ili wapendwe. Hawa ni wanawake ambao wana kasoro kubwa kwenye mifumo yao ya kufikiri au ufahamu.

Unaweza kukuta mwanamke anadhalilishwa, anaoneshwa kwamba hatakiwi, amechokwa, ameshachezewa lakini amemng’ang’ania mwanaume huyo kama luba.

Unaweza kukuta anakwenda Baa na mwanaume, na mwanaume huyo anaanza kuwashika wanawake makalio mbele yake, anamtajia hawara zake, anamwonyesha wazi kwamba, hamthamini, bali anamtumia tu kama chombo cha starehe. Lakini manamke huyo amemng’ang’ania mwanaume huyo. Mwenyewe anaita kupenda.


Kwa kawida mwisho wa safari ya mapenzi kama haya ya ‘kichaa’ ni mwanamke kuachwa, tena kuachwa kwa visa na mikasa mingi. Kumbuka unapojipendekeza badala ya kupenda, unamkera unayejipendekeza kwake. Lakini mbaya zaidi ni kwamba, kile tunachoita kupenda sana ni kuhemkwa na wala sio kupenda. Tunapopenda hatupotezi ufahamu wetu, bali tunakuwa na ufahamu zaidi.

Tunapohemkwa huwa hatutumii akili bali tunatumia hisia. Kwa hiyo tunakuwa watumwa wa hisia zetu. Katika hali kama hiyo, mwanamke anachanganya kupenda na kuhemkwa. Anafikia mahali anagundua kwamba, ameumia sana na hakupata alichokuwa anataka kutoka kwa mwanaume, ambaye alisema anampenda sana.

Lakini pia ili kumdhihirishia kwamba anampenda, atajaribu kujiua akikataliwa, atatafuta kila visa ili mwanaume ahisi kushtakiwa na dhamira, aone kuwa yeye ndiye mwenye makosa. Anataka kupendwa, anaomba kupendwa, anashurutisha kupendwa. Kwa nini?

Kama nilivyosema, hayo ni matatizo kwenye kwenye mfumo wa kufikiri. Mwanamke wa aina hiyo ni mgonjwa na ndio maana ana utegemezi.
 
Kuna mengi nyuma ya pazia, kama anahemkwa na mumewe ....anawaza mengi, watoto, aibu, fedheha, kuanza upya, anampenda.. nk

Siwasapoti ila sidhani kama ni vichaa, kuna doctors,judges n other proffesional women travelling that road,

when a woman knows her worth wanaacha, wale wasio na kipato inakuwa ngumu zaidi kutoka ila kuna those who dares na kutoka...

Walaaniwe wanaume wa jinsi hii ya kushika mahawara bar mbele ya wake zao simply bcoz wake zao hawawezi kuwafanya kitu
 
Mkuu kwa upande wa pili ikitokea kwa mwanaume inakuwaje?? wewe unajua kuwa mwanamke wako anatoka na bosi wake na semina haziishi; mtoto wako kafanana na jirani yako mwenye Pajero lakini wewe huambiliki wala usikii... kwa hiyo watu wakuiteje?
 
Acha nikimbie vinginevyo hizi laana ni zaidi ya nuclear missiles
 
Wengine wamezoea tabu, labda hata malezi walio pewa yalikuwa ya manyanyaso. Hawakufanikiwa kufundishwa lipi jema na lipi bovu kimapenzi. Kazoea kutreatiwa kama mbwa au kama punda. Au pengine maisha ya mama yake na baba yake yalikuwa ya misukosuko, ya ugomvi kupigana na kudharirishana, nae anaona ya kawaida tu maana hata wazazi wake waliishi kwa kunyanyasana.

Au kapenda sana ilimladi awe nae tu huyo bwana, ingawa anajua huyo jamaa ni mbwa. Au jamaa anamlidhika sana huyo dada kitandani, na hizo raha hataki wapate wengine tu, hata yeye vile vile anataka, ndio anafight kula kitam.

Au mwanamke anajiskia fahari kuwa na huyo bwana. Au labda huyo dada anapenda wanaume wenye tabia za kiuni. Mie narafiki yangu akipenda wanaume wanao mtreat vibaya, kama wakimbaka, wakimdanganya, akimkuta na mwanamke mwengine watukanae na kugombana na kupigana.


mwanamme akimtreat vizuri anamuona ****, na lijinga. Haya kila mtu na lake ulimwengu huu.

Na kuna wanaume pia wanapenda wanawake vicheche pia, mwanamke mwenye wanaume wengi, mjeuri, hasie na adabu.
 
ulishawahi fanyia mpenzi wako hayo???... usione kobe kainama.. binti anaevumilia huo ujinga siku akikurudi.. Utajuta kuzaliwa
 
Mpendwa ningeomba tafsiri rahisi na nyepesi ya neno kuhemkwa maana na akili yangu hii ya kubandika na mate upepo kidogo tu hiyooooo naiokotea posta sijaelewa kitu. Naomba msaada wako kabla sijachangia
 
Mkuu kwa upande wa pili ikitokea kwa mwanaume inakuwaje?? wewe unajua kuwa mwanamke wako anatoka na bosi wake na semina haziishi; mtoto wako kafanana na jirani yako mwenye Pajero lakini wewe huambiliki wala usikii... kwa hiyo watu wakuiteje?
utakuwa umepigwa limbwata
 
Mkuu kwa upande wa pili ikitokea kwa mwanaume inakuwaje?? wewe unajua kuwa mwanamke wako anatoka na bosi wake na semina haziishi; mtoto wako kafanana na jirani yako mwenye Pajero lakini wewe huambiliki wala usikii... kwa hiyo watu wakuiteje?

Ni kweli uko sahihi, lakini niliangalia upande ambao unaumia zaidi...............
 
Mpendwa ningeomba tafsiri rahisi na nyepesi ya neno kuhemkwa maana na akili yangu hii ya kubandika na mate upepo kidogo tu hiyooooo naiokotea posta sijaelewa kitu. Naomba msaada wako kabla sijachangia

Ngoja nitafute kamusi ya kiswahili, ili nikupe maana sahihi ya neno hilo. Ahsante kwa kuuliza.................
 
Nifafanulie kwenye kuchechezewa,,,,,,,anachezewaje???????swali kwa mtoa mada au yeyote alienielewa na kumuelewa mtoa mada
 
Na wanaume wanaong'ang'ania wanawake ambao anajua kabisa hamtaki lakin utakuta anampigia magoti nusura alie hvi hii ni akili kweli au niite wendawazimu?
 
Back
Top Bottom