nikiwa na 40mil naweza jenga nyumba ya namna gani....

kaka asikudange mtu kwahiyo pesa utajenga nyumba ambayo siyo kamili au kwamaneno mengine sio ya kisasa..nyumba ya vyumba vitatu yenye sebule ya kutosha, dinning, vyoo viwili na parking ya gari..ikiwa imefanyiwa finnishing ya kisasa inaenda mpaka millioni 80 reasonable one.
 
Kama unataka kujenga to completion/finishing Tshs 40m za kitanzania, unaweza ukajenga vyumba viwili vya kulala plus sitting room, dining room na kitchem. Lakini tahadhari, usimamizi wako ndiyo utakaokuokoa, namaanisha uwe na muda wa kwenda mwenyewe kunununa vifaa vya ujenzi na kusimamia kuhakikisha vinatumika ipasavyo, vingine mafundi watakuchakachua hata kwenye lenta hautafika.
 
Jaamani jaamani mbona watu mnaexaggerate mambo hivyo? kwanza mngemuliza je anajenga kwa material gani matofali yapi kuchoma, hydraform, au cement bricks? siku hizi kuna pre- fabricated houses. je kwa material tofauti bado tuu gharama ni ileile? Mimi nimegundua watu wengi waliojenga wanapenda kutoa gharama kubwa sana za ujenzi walizotumia.
 
Wasikukatishe tamaa bana unaweza kujenga room tatu, sebule, choo, jiko bila hofu kama tu una kiwanja tayari. Mambo ya finishing mapema mapema mbwembwe tu, uwaweza kufanya finishing ndani tu ukahamia, halafu hayo mengine taratibu yatajipa.

Sisi wengine tulifanya hivyo, tukamalizia kwa kutumia pesa ya kodi ya pango ambayo iliokolewa kutokana na kuishi kwangu, leo hii nyumba yangu haina tofauti na mfanyabiashara mkubwa, na geti juu.
 
Mkuu nakushauri usijenge nyumba kulingana na kiasi cha fedha ulizonazo, bali jenga nyumba kulingana na eneo unalipoata kiwanja, mazingira, upatikanaji wa vifaa, matakwa, interest zako, mambo unayopenda, idadi ya watu wanaotegemea kuishi katika nyumba hiyo, tabia zao na mambo mengine yanayokuhusu walenga watakaokaa katika nyumba hiyo kisha fanya building economy ya nyumba yako kujua kwa mahitaji ya nyumba yako itakughalimu kiasi gani na kwa muda gani hadi kumalizika.

Kumbuka unaweza kujenga nyumba uitakayo kidogo kidogo hadi ikaisha hasa ukiwa na vyanzo vizuri ama shughuli zinazokuingizia kipato kuongezea gharama za ujenzi huo.
 
Hiyo pesa inatosha kujenga nyumba rooms 3 , kimoja master ,sebule dinning ,public bathroom pamoja na jiko as long u
na kiwanja tayari
Mchanganuo
Matofali 2000 x 1000 = 2 M
Cement 50 bags = 0.7M
Mawe na mchanga 0.7M
Ufundi mpaka lenta= 1.5M
Nondo za lenta =0.8 M

Kupaua
Bati za south 12000 kwa mita bati 90 =3.3M
Kofia. 0.6 M
Mbao za kupaua 3M
Fundi wa kupaua 0.6M

Piga hesabu hadi kupaua alafu imebaki ngapi ntakuja na finishing calculations
 
Hiyo pesa inatosha kujenga nyumba rooms 3 , kimoja master ,sebule dinning ,public bathroom pamoja na jiko as long u
na kiwanja tayari
Mchanganuo
Matofali 2000 x 1000 = 2 M
Cement 50 bags = 0.7M
Mawe na mchanga 0.7M
Ufundi mpaka lenta= 1.5M
Nondo za lenta =0.8 M

Kupaua
Bati za south 12000 kwa mita bati 90 =3.3M
Kofia. 0.6 M
Mbao za kupaua 3M
Fundi wa kupaua 0.6M

Piga hesabu hadi kupaua alafu imebaki ngapi ntakuja na finishing calculations

40m nyingi sana kaa humu.
 
mwaya wasikudanganye - 40m ni mahela mengi -
Hata kigorofa cha chati unaweza - jipange tu - uachane na mambo ya "contractor" kwani atajenga ya kwako na yake
chukua mafundi wazoefu wa kawaida tu - nunua materials zako kwenye maduka bei nafuu ...... yaani utajenga na zitabaki kidogo za soda.:smile:
 
Aspen,

You are very right and you seem to be trustworth,,,,,watu wanacheza na 40M nadhani ni kwa sababu tu wanatamka, hawana in hand,,,,ila najua for sure 40M inajenga Nyumba kali sana hapa dar,,,,

Wanao - comment kwamba haitoshi ni wale waliozoea kusimamia ujenzi wa Barabara na nyumba za Serikali na hivyo wanachakachua,,,

Mdau ukitaka kujenga wewe tafuta Archtect akutengenezee Ramani Standard,, tafuta fundi mwenyewe muweke Site, then kuwa na usimamizi wa Karibu,,,kwa kiasi fulani nimekubaliana ha hesabu za Aspen....Aspen kama wewe ni Mtaalam wa mambo ya ujenzi utafika mbali maana inaonekana ni mwaminifu
 
Aspen umeashau mbao za kufungia lenta kama 0.7M misumari ya kufungia mbao kama 30,000TZS na kokoto ndogo tripu 2 0.3M...

Duh yaani 40M ni hela nyingi mno
 
Nimemjengea mtu nyumba tegeta ya vyumba vitau na masta moja dining jiko na stoo, varanda mbili tena zote zimemwagwa zege....shiling mil30 imetumika mpaka sasa na imebaki rangi, alluminium, na gypsum tu.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom