Nikikumbuka nacheka tena na tena!

Hii ilikuwa huko maeneo ya kisemvule,mkuranga mkoani pwani.Wazee kama wanne walikuwa katika ubwabwa wa shughuli. Basi mzee mmoja mroho tofauti na wenzie alikuwa akila nyama tu. Mara ghafla yule mzee akaacha kula,akabaki anawaangalia wenzie kwa huzuni huku machozi yakimtiririka.

Mzee mmoja alijua kilichomtokea mzee mwenzao, akampa bonge la mbata ya mgongo, nyama ilifyatuka kama risasi kutoka mdomoni mwa yule mzee. Duh!kumbe yule mzee alikwama na kipande cha nyama kooni.

Hii nimecheka sana mkuu
 
Back
Top Bottom