Nikijiuzulu hamtapata waziri kama mimi - Nchimbi

Haya ndo majibu mepesi kwa maswali magumu. Hataki kabisa kushughulisha ubongo wake.
 
Nchimbi anapata wapi ujasiri wa kusema " mtapata wapi waziri kama mimi kama nikijiuzuru” ? wizara iliyojaa rushwa, mauaji ya raia, kupandikiziana kesi,askari hawana nyumba wanaishi kwenye vibati.

Jamani! hivi "ukimchekesha kuku ili uyaone meno yake inawezekana?" Huyo ni mtoto wa Polis na kwenye mapolis yeye ndiye aliye afadhali!!
 
Akili yake na CCM yake inamtuma kujibu hivyo bro ni mfumo ndio unaotuumiza hapa.

Tusisahau kuwa alikuwa M/Kiti wa Vijana hao wa Chlorophyll (Rangi ya Majani) na hivyo akili yake ya sasa na ya akina Shigela hazitofautiani hata chembe na alichokuwa anatetea 'wakati wake' hakijapotea, na nafasi aliyo nayo sasa ni ktk kusimamia yale aliyokuwa akifanya akiwa M/Kiti wa Vijana hao wabovu!
Pia tukumbuke kuwa anaongoza JESHI MBOVU NA 'POLISISIEMU'...The Useless sect so far!
 
Huyu si ndo aliiwakilisha nchi kwenye mazishi ya hayati Prof. Saittoti na akaacha aibu ya kutosha. Shame on him
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi, alipoulizwa:

Kama yuko tayari kumsimamisha kazi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda ili kupisha uchunguzi huo alisema ndani ya tume hiyo kuna Naibu Kamishna wa Polisi; hivyo kamanda huyo ambaye cheo chake ni Kamishna Msaidizi hana ubavu wa kuharibu uchunguzi huo.

Kuhusu askari aliyempiga bomu Mwangosi kama anashikiliwa na Polisi au bado yuko nje, alisema atachukua hatua mara baada ya tume hiyo au ile ya Polisi, iliyoundwa na Mkuu wa Polisi, IGP Said Mwema kukamilisha uchunguzi wake.

Kuhusu kama atajiuzulu iwapo ripoti itabaini kuwa polisi ndio waliofanya mauaji hayo, alisema “Nikijiuzulu mtampata wapi Waziri kama mimi? (kicheko) Shauri yenu… lakini nawahakikishieni kuwa ukweli utaanikwa wazi.”

Kwamba Polisi wanatumiwa kukikandamiza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kwa manufaa ya CCM, alisema hataruhusu hali ya namna hiyo na akasisitiza kuwa Polisi wamekuwa wanatekeleza agizo la Msajili wa Vyama vya Siasa la kupiga marufuku mikutano ya kisiasa katika kipindi hiki cha Sensa ya Watu na Makazi. Alipotolewa mifano ya namna ambavyo wanachama wa CCM wamekuwa wakifanya mikutano yake bila kuingiliwa na Polisi, Dkt. Nchimbi alisema alipata taarifa hizo na akamjulisha Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama ambaye alimhakikishia kuwa hakuna mkutano wa hadhara unaofanywa na chama chake badala yake wanafanya vikao vya ndani, “Mikutano ya ndani haikupigwa marufuku, kilichokatazwa ni mikutano ya hadhara na ninaomba wenzetu wawe wastahimilivu kwani zimebaki siku nne tu za sensa.”

Source: wavuti - wavuti

My Take: Hatuna Viongozi.


MAJIBU KWA MUJIBU WA NCHIMBI
1. Kamuhanda alivyoua Songea ilikuwa halali. Huyo ndiye Excutioner wa Serikali iliyomadarakani
2. Picha zinazomuonyesha askari aliyemuua Mwangosi zimepigwa na camera ya CDM hivyo ni za kizushi. Lazima Tume iundwe ili baada ya mwezi mmoja kupita, askari husika asemekane kafa/katoroka nchini.... the case is dismissed. Tume za aina hiyo hadi sasa hazijaleta majibu. Bado zinatafuta ushahidi. This is a bad joke.
3. Nchimbi anajiona ni kidume....Kioo ukutani, nambie nani mzuri kama mimi syndrome.
4. Mikutano ya hadhara CCM ruksa.....Vyamavingine, fanyieni kwenye vyumba vyenu vya kulala.... msilete longolongo hapa!

UNATEGEMEA JIPYA LIPI KAMA WAZIRI TU MWENYEWE HATA KWATA HAKUPIGA? Gombea Urais 2015 nawe uweke washkaji kwenye madaraka. Nchi hii ni ya kutesa kwa zamu.

LAKINI DAWA YENU CCM IKO JIKONI....... NI PALE MTAKAPOKOSA HATA MUDA WA KUJICHUBUA NYUSO ZENU ILHAL NI WANAUME NA KUWEKA DAWA ZA KUTOA MVI...... ANGALIA, WAZIRI GANI ANA MVI KICHWANI? WHAT DO YOU EXPECT FROM THESE INSECURE MINDS?
 
Nchimbi ni boga lile,unafiki umemjaa yeye mwenyewe aliwachakachua chadema kwenye matokeo ya ubunge 2010 sasa anajua songea mjini 2015 hana chake ndio maana anakazana kukivuruga cdm ili hakose mpinzani songea mjini 2015,jamaa bonge la kilaza na bichwa lake ametumia tu kufuga nywele.....siku zake nae zinahesabika bado miaka 2 tu,anadhani ni mbalia sana chadema un stopable kwasasa ukishindana na chadema utakuwa tahira........
 
Huyu ni mmoja kati ya watu waliolewa madaraka na wanaamini bila wao hakuna wanaoweza kuongoza nchi hii,shame on you muuaji kwa kisingizio cha chadema,kule mara polisi wameua ,songea na kwingineko bado mnajiita hakuna wengine wa kuongoza hizo wizara nani amewaambia tunataka kuongozwa na wauaji?
 
Nchimbi hana busara kabisa.. Yaani nimeshangaa alivyokuwa anaongea hovyo pomaja na kuwatuhumu viongozi wenzake waziwazi kitu ambacho sio health kwa team work leadership. Yaani nimemwondoa kabisa maanani na ninamweka kwenye kundi la wauaji kuanzia leo. Maana hata kule kwake Songea alishazoea kuua..
 
Hata kulewa madaraka mtu aliye sawa sawa hawezi kuongea maneno haya. Mawazo yangu inawezekana huyu jamaa alianza kutoka na masaburi wakati wa kuzaliwa kwake.
 
View attachment 63926View attachment 63927View attachment 63928View attachment 63929

hapa ni bububu, ccm wakifanya uzinduzi wa uchaguzi mdogo shughuli iliyoongozwa na makamu wa rais dk bilal. Hii ilikuwa ni tarehe 2 september, siku ambayo cdm walipotaka kufungua tawi na kufanya mkutano wao wa ndani pale nyororo (mfindi) na baadaye polisi kuleta vurugu na kusababisha mauaji ya kinyama ya mwandishi wa habari daudi mwangosi.

ccm ni mashetani tena weusi wasio na utu i hate youuuu
 
Tunaona namna majizi yanavyotumia kodi za watanzania vizuri kwa kuwapa jezi wafuasi wao lkn bado haitoshi wanaua raia wasio na hatia ili waendelee kuwaabudu wao wezi .maskini tanzania
 
Back
Top Bottom