Kura huwa zinaibwajwe? hili swali nimeisha liuliza mara kwa mara humu jamvini , ila hakuna mwenye majibu , may be ww ukawa mwarobaini wa swali hil
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi, alipoulizwa:
Kama yuko tayari kumsimamisha kazi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda ili kupisha uchunguzi huo alisema ndani ya tume hiyo kuna Naibu Kamishna wa Polisi; hivyo kamanda huyo ambaye cheo chake ni Kamishna Msaidizi hana ubavu wa kuharibu uchunguzi huo.
Kuhusu askari aliyempiga bomu Mwangosi kama anashikiliwa na Polisi au bado yuko nje, alisema atachukua hatua mara baada ya tume hiyo au ile ya Polisi, iliyoundwa na Mkuu wa Polisi, IGP Said Mwema kukamilisha uchunguzi wake.
Kuhusu kama atajiuzulu iwapo ripoti itabaini kuwa polisi ndio waliofanya mauaji hayo, alisema Nikijiuzulu mtampata wapi Waziri kama mimi? (kicheko) Shauri yenu lakini nawahakikishieni kuwa ukweli utaanikwa wazi.
Kwamba Polisi wanatumiwa kukikandamiza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kwa manufaa ya CCM, alisema hataruhusu hali ya namna hiyo na akasisitiza kuwa Polisi wamekuwa wanatekeleza agizo la Msajili wa Vyama vya Siasa la kupiga marufuku mikutano ya kisiasa katika kipindi hiki cha Sensa ya Watu na Makazi. Alipotolewa mifano ya namna ambavyo wanachama wa CCM wamekuwa wakifanya mikutano yake bila kuingiliwa na Polisi, Dkt. Nchimbi alisema alipata taarifa hizo na akamjulisha Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama ambaye alimhakikishia kuwa hakuna mkutano wa hadhara unaofanywa na chama chake badala yake wanafanya vikao vya ndani, Mikutano ya ndani haikupigwa marufuku, kilichokatazwa ni mikutano ya hadhara na ninaomba wenzetu wawe wastahimilivu kwani zimebaki siku nne tu za sensa.
Source: http://www.wavuti.com
My Take: Hatuna Viongozi.
Alipokuwa anatangaza tume ya kuchunguza mauaji ya Marehemu D. Mwangosi, Nchimbi aliulizwa endapo yuko tayari kujiuzulu kama itabainika kwamba polisi ndio wanahusika na mauaji haya, akasema tena kwa kejeli 'nani ajiuzulu, nikijiuzulu mtapata wapi waziri kama mimi'.
My Take:
hizi ni dharau na kejeli kubwa sana kwa watanzania, sijui anaweza kutuambia lolote la maana alilofanya toka amewekwa kusimamia wizara hii, ninachokiona kwake ni kuratibu mauaji yanayoendeshwa na Polisi akishirikiana na Mwema. Nchimbi please swallow your pride and step down.
Tanzania has lot of pending leaders- he has done somthing but not true that he is the only one...very disapointng