Nikijiuzulu hamtapata waziri kama mimi - Nchimbi

Alipokuwa anatangaza tume ya kuchunguza mauaji ya Marehemu D. Mwangosi, Nchimbi aliulizwa endapo yuko tayari kujiuzulu kama itabainika kwamba polisi ndio wanahusika na mauaji haya, akasema tena kwa kejeli 'nani ajiuzulu, nikijiuzulu mtapata wapi waziri kama mimi'.

My Take:
hizi ni dharau na kejeli kubwa sana kwa watanzania, sijui anaweza kutuambia lolote la maana alilofanya toka amewekwa kusimamia wizara hii, ninachokiona kwake ni kuratibu mauaji yanayoendeshwa na Polisi akishirikiana na Mwema. Nchimbi please swallow your pride and step down.

Mkuu Kapotolo, mimi ninamuunga mkono huyo Nchimbi wao kubakia kuwa waziri wa mambo ya ndani kwa kuwa wizara hii imebadiri matumizi yaka na kuwa wizara ya mambo ya mauaji. Songea anakotokea Nchimbi wanaijua vizuri sana wizara hii.
 
Kupitia chama gani, kwa mauaji haya hata kuiba kura kimiujiza CCM hawataweza kwani hata shetani ashawakimbia.

Kura huwa zinaibwajwe? hili swali nimeisha liuliza mara kwa mara humu jamvini , ila hakuna mwenye majibu , may be ww ukawa mwarobaini wa swali hil
 
Nchimbi yuko sahihi kabsa...hamuwez pata waziri dhaifu kama yeye atakae kua kwenye serikali dhaifu..
 
damu za watu zinamtesa huyo nchimbi.ashukuru Mungu anakiongozi dhaifu,yaani kuwa na waziri kama nchimbi ni aibu kubwa kwa taifa hili ni kwamba hatuna tu pa kusemea,na kwakuwa kafanya kazi kubwa ya kumsaidia kiwete kuua watu wengi kama kafara,ndiyo maana alimteua.lakini nchimbi hana sifa hata ya kuwawa mwenyekiti wa mtaa.labda kiongozi wa majambazi na wachawi.
 
Alipokuwa anatangaza tume ya kuchunguza mauaji ya Marehemu D. Mwangosi, Nchimbi aliulizwa endapo yuko tayari kujiuzulu kama itabainika kwamba polisi ndio wanahusika na mauaji haya, akasema tena kwa kejeli 'nani ajiuzulu, nikijiuzulu mtapata wapi waziri kama mimi'.

My Take:
hizi ni dharau na kejeli kubwa sana kwa watanzania, sijui anaweza kutuambia lolote la maana alilofanya toka amewekwa kusimamia wizara hii, ninachokiona kwake ni kuratibu mauaji yanayoendeshwa na Polisi akishirikiana na Mwema. Nchimbi please swallow your pride and step down.


Hakuna dharau yoyote hapo, mie naona ww ndio umejichanganya kwani Nchimbi alichosema ni dhahiri shahiri sahihi.Tatizo la cdm mlilo nalo sasa ni kuwa hakuna viongozi wakutosha wakuongoza dola
 
Damu ya mtu haipotei bure wako wapi madikteta waliotikisa dunia hii akina HITTLER,SADDAM HUSSEIN NK .HIVI HAWA madikteta vichanga wanajivunia nini?kama si kubebana na mwema wake na watawala. MALIPO mTAYAPATA HAPA hapa DUNIANI NA MWISHO MBELE ZA HAKI.WATAWALA WOTE NAWAKABIDHI KWA MUNGU MWENZA WA YOTE YOTE.
 
Na hutokoma, kwa kuwa we ni dhaifu...kwa sababu mnamkataba na watanzania wote kuwa mtatawala milele ,laana nyie na vizazi vyenu.
Safi sana waeleweshe hao wabishi kama wako toilet na nchimbi ndiye prime minister kwenye serekali 2015
 
Nilimfahamu jina na sura tu lakini mwaka 2010 nilistaajabu kwa kiwango cha ufahamu wake!! Alikuwa naibu waziri wa ulinzi. Kulikuwa na military brief ya operations za majeshi katika nchi moja ambapo majeshi yetu yanafanya kazi za kulinda amani. Kama mgeni mkuu wa ujumbe wa wizara, alipwaya kiasi cha kushangaza wenyeji wake. Nilishangaa na kuona aibu sana.

Baadae aliandaliwa chakula cha mchana kwa heshima ya nchi ile. Nikapewa nafasi ya kukaa pembeni yake. Nilimuuliza anawezaje kufanya kazi na majeshi ambayo yana military structure ambayo inamuondoa yeye (kumbuka amiri jeshi mkuu ni Rais). Alinijibu kijinga "Wao ndio wanapaswa kujifunza kufanya kazi na mimi".

Kwa mara nyingine ninasikia "mimi" kwa mtu very incompetent ukiachia mwonekano wake wa nje!! My foot!!!
 
ukiona hivyo ujue aliyemuweka kamhakikishia kuwa hata mpiga chini
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi, alipoulizwa:

Kama yuko tayari kumsimamisha kazi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda ili kupisha uchunguzi huo alisema ndani ya tume hiyo kuna Naibu Kamishna wa Polisi; hivyo kamanda huyo ambaye cheo chake ni Kamishna Msaidizi hana ubavu wa kuharibu uchunguzi huo.

Kuhusu askari aliyempiga bomu Mwangosi kama anashikiliwa na Polisi au bado yuko nje, alisema atachukua hatua mara baada ya tume hiyo au ile ya Polisi, iliyoundwa na Mkuu wa Polisi, IGP Said Mwema kukamilisha uchunguzi wake.

Kuhusu kama atajiuzulu iwapo ripoti itabaini kuwa polisi ndio waliofanya mauaji hayo, alisema "Nikijiuzulu mtampata wapi Waziri kama mimi? (kicheko) Shauri yenu… lakini nawahakikishieni kuwa ukweli utaanikwa wazi."

Kwamba Polisi wanatumiwa kukikandamiza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kwa manufaa ya CCM, alisema hataruhusu hali ya namna hiyo na akasisitiza kuwa Polisi wamekuwa wanatekeleza agizo la Msajili wa Vyama vya Siasa la kupiga marufuku mikutano ya kisiasa katika kipindi hiki cha Sensa ya Watu na Makazi. Alipotolewa mifano ya namna ambavyo wanachama wa CCM wamekuwa wakifanya mikutano yake bila kuingiliwa na Polisi, Dkt. Nchimbi alisema alipata taarifa hizo na akamjulisha Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama ambaye alimhakikishia kuwa hakuna mkutano wa hadhara unaofanywa na chama chake badala yake wanafanya vikao vya ndani, "Mikutano ya ndani haikupigwa marufuku, kilichokatazwa ni mikutano ya hadhara na ninaomba wenzetu wawe wastahimilivu kwani zimebaki siku nne tu za sensa."

Source: http://www.wavuti.com

My Take: Hatuna Viongozi.

 
Mkuu nkyalomkonza kwani wewe ulidhani tunaviongozi, chama cha magamba tunawaganga njaa tuu!
 
Last edited by a moderator:
viazi tu hawa wanategemea ushirikina kuongoza nchi ndoo maana tupo hapa tulipo
 
Hatushangai majibu hafifu ya namna hii kutoka kwa Nchimbi. Kwanza ni mtu aliyelewa madaraka siku nyingi sana tangu akiwa Mwanafunzi IDM Mzumbe. Anapenda ukubwa na ndiyo maana alijipachika PhD na ilipopigiwa kelele akaenda kuisafisha Mzumbe (PhD laundering). Kwasasa anandoto kubwa ya kuja kuwa Rais wa nchi hii, na kwa upofu wake wa fikra, anafikiri watanzania wote ni wajinga na ahkuna bora zaidi yake.

Hatujaona na maana sana na cha kumsifu tangu achaguliwe kuwa waziri wizara zote, kote anavurunda tu. Hebu tumuulize lile vali za Taifa limepotelea wapi?? Na huku alipo sasa kila kukicha ni mauaji ya raia wasio tishio la amani. Amepachikwa pale ili waweze kutumia nguvu ya dola kuhakikisha wanabaki madarakani kwa nguvu, badala ya kujisafisha na kujijengea imani kwa wananchi. Kwasasa tumeshakuwa wakimbizi ndani ya nchi yetu.
 
kama Nchimbi ndio aina ya viongozi wanaomshauri rais, basi ni halali kufika tulipofikia..,jamaa hajui diplomasi,taaluma,siasa wala itifaki kiujumla hana lugha ya kiungozi.
 
Nchimbi anapata wapi ujasiri wa kusema " mtapata wapi waziri kama mimi kama nikijiuzuru" ? wizara iliyojaa rushwa, mauaji ya raia, kupandikiziana kesi,askari hawana nyumba wanaishi kwenye vibati.
 
Back
Top Bottom