Nikifa nichomeni moto! Kha!

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Labda ni mzazi wako ama mke/mume au hata mtoto anakwambia NIKIFA NATAKA NICHOMWE MOTO!
Naam nimesikia hiyo wiki hii! Mzee mmoja huko Marangu naskia aliamua kuchomwa moto akifa. Na ndivyo ilivyokuwa!

Jana mji wa Moshi na viunga vyake ilikuwa ndiyo story kuu. Mzee huyo alichomwa moto sehemu wanakochomewa watu wenye asili ya kihindi.

Ingawa ni uamuzi wa mtu lakini inatisha! We ungeambia hivyo ungefanyaje?
 
Asante kwa uzi huu, nadhani ifike wakati sasa watu tujue miili yetu tukishakufa haina umuhimu tena! Wenzetu wamefikia hatua ya kuamua miili yao itumike kwenye majaribio ya kisayansi au viungo kama vile figo, moyo nk vitojewe kuwasaidia wanaovihitaji(mf.umepata ajari na kichwa chako kimesagika sagika)

Hebu ona jinsi raslimali nyingi kama muda, ardhi, mbao,nk zinavyopotea kwa kile kinachohitwa kumsitiri marehemu, mwili wangu nikifa hauna kazi tena, kilichochobaki ni bakteria kuurejeresha- madini yote muhimu yanarudi ardhini yalikotoka.
Huyo mzee ni mfano wa kuigwa.
 
na mi nimewahi kuisikia hii kwa mzee mmoja mwanza.alijisajiri kabisa na singa singa ili achomwe..kuwa uyaone
 
Unafuata matakwa ya huyo anayetaka kuchomwa moto....mfano dada yangu kashasema na anatuambia kila siku apatapo wasaa kuwa akifa angependelea achomwe moto popote pale alipo halafu tuletewe majivu yake ili tuyafukie sehemu kwa ajili ya kumbukumbu (headstone to be precise)...kwa hiyo itakuwa kitu cha kawaida tu hapa bongo siku si nyingi
 
Mi naunga mkono hii, maana idea ya kuoza kaburini unaliwa na wadudu sio nzuri kabisa.

Tena unatumia eneo kubwa sana wakati umeshakufa, waste of space, kuna makaburi bongo hakuna nafasi, kuna siku watu walikuwa wanazika wakati wa kuchimba wakapasua jeneza lengine harufu iliyotoka humo usiombe!
 
Nilisimuliwa kisa cha huyo marehemu ila nawasifu wafiwa kwa ujasiri .Marehemu alikuwa na maagano/kiapo na mzungu mmoja kuwa akitangulia yeye achomwe moto na majivu yake apelekewe huyo mzungu na Mzungu akifa majivu yake yawekwe na yakwake.Kwa kweli tumeshangaa sana maagano ya namna hiyo si mazuri
 
Kibaya zaidi ni pale kanisa la kkkt lilipoungana na maagano hayo ya mungu wa kihindi wa mto ghandi. Kwa sababu maiti ya marehemu ilipelekwa ndani ya kanisa la kijiji cha Kotela na kusomewa ibaada ya mazishi na kuruhusu ikachomwe. Sijui ni vipengele gani wametumia katika biblia kuhalalisha hiyo ibaada ya uchomaji moto. Au labda ni kwa sababu jamaa alikuwa na uwezo? Maana kanisa la kilutheri linaabudu wenye uwezo wa kifedha. Ukitaka kuliburuza kanisa la kilutheri kadri uwezavyo wewe uwe na pesa tu hata kama zimepatikana kwa kuwachinja albino.
.
 
afadhali uamuzi huo utawasaidia, maana siku hizi mnaweka nondo na zege juu, bila kusahau tiles !
Sisi mila yetu ni ya Nabii Ibrahim !
 
afadhali uamuzi huo utawasaidia, maana siku hizi mnaweka nondo na zege juu, bila kusahau tiles !
Sisi mila yetu ni ya Nabii Ibrahim !

Ni kawaida yetu hata nyumba zetu za ibada ni tofauti na za wengine, nyumba zetu za kuishi nazo zina tiles, shule zetu na hata ndevu zetu tunanyoa na kuzitunza vizuri na sio kuziacha holela kama beberu la hitima.

Kwa kifupi ni kawaida yetu kuwa smart na sio kuvaa suruali njiwa.

Tukirudi kwenye suala la kuchoma moto maiti, itasaidia pia makaburi kutozagaa kila kona. Kule kibada kulizagaa makaburi kila kona kiasi ilibidi serikali itumie gharama kubwa kuyahamisha ili zoezi la kupima viwanja lifanikiwe. Hapo ndio niligundua kuwa jamii fulani ya watu, sio tu inazaa hovyo, bali pia inazikazika hovyo. Baadhi ya hayo makaburi yaliyofukuliwa yalikuwa na maajabu. Kuna binti alizikwa miaka 9 iliyopita lkn alipofukuliwa alikutwa bado mbichi, ameoza maeneo ya tumbo tu. NIkajua ni yale mambo yetu ya kienyeji yale
 
Ata mimi ningependa nikifa Nichomwe Moto tu,majivu yapeperushwe juu ya mlima kilimanjaro.
saudi arabia wana mashine ya kuchomea ndani ya dk 38 umekuwa majivu watuletee tukuchome mi sipendi sana kifo kizungumziwe sana
 
Waumini wengine wa dini wanapinga uchomaji moto kwa sababu hauendani na taratibu za dini zao.
 
Biashara ya crematorium za kisasa za kuchoma maiti inaweza kuwa dili miaka ijayo. Siyo mambo ya kuni na mafuta ya taa kama Wahindu.
 
Kibaya zaidi ni pale kanisa la kkkt lilipoungana na maagano hayo ya mungu wa kihindi wa mto ghandi. Kwa sababu maiti ya marehemu ilipelekwa ndani ya kanisa la kijiji cha Kotela na kusomewa ibaada ya mazishi na kuruhusu ikachomwe. Sijui ni vipengele gani wametumia katika biblia kuhalalisha hiyo ibaada ya uchomaji moto. Au labda ni kwa sababu jamaa alikuwa na uwezo? Maana kanisa la kilutheri linaabudu wenye uwezo wa kifedha. Ukitaka kuliburuza kanisa la kilutheri kadri uwezavyo wewe uwe na pesa tu hata kama zimepatikana kwa kuwachinja albino.
.

Aka Lowasa
 
Ni kawaida yetu hata nyumba zetu za ibada ni tofauti na za wengine, nyumba zetu za kuishi nazo zina tiles, shule zetu na hata ndevu zetu tunanyoa na kuzitunza vizuri na sio kuziacha holela kama beberu la hitima.

Kwa kifupi ni kawaida yetu kuwa smart na sio kuvaa suruali njiwa.

Tukirudi kwenye suala la kuchoma moto maiti, itasaidia pia makaburi kutozagaa kila kona. Kule kibada kulizagaa makaburi kila kona kiasi ilibidi serikali itumie gharama kubwa kuyahamisha ili zoezi la kupima viwanja lifanikiwe. Hapo ndio niligundua kuwa jamii fulani ya watu, sio tu inazaa hovyo, bali pia inazikazika hovyo. Baadhi ya hayo makaburi yaliyofukuliwa yalikuwa na maajabu. Kuna binti alizikwa miaka 9 iliyopita lkn alipofukuliwa alikutwa bado mbichi, ameoza maeneo ya tumbo tu. NIkajua ni yale mambo yetu ya kienyeji yale

Hapo red nimecheka kwa loud speaker lol.
 
afadhali uamuzi huo utawasaidia, maana siku hizi mnaweka nondo na zege juu, bila kusahau tiles !
Sisi mila yetu ni ya Nabii Ibrahim !

Si mnao muda ndio maana na kutumia akili kwenu ni gharama. Abraham aliishi enzi hizo wakati hakuna mortuary kwa hiyo kuhifadhi maiti na kuisafirisha ikiwa na uchafu tumboni ilikuwa si rahisi, kwa hiyo walikamuana. Sasa nyinyi leo hii bado mpo bize kuminyana matumbo as if kuna treasure mtu alimeza, loh!

Ila nyinyi ni bora msichomwe manake mtakuwa mnachomeka 'dabal'. Mchomwe duniani haya mkifika langoni tena mchomwe, kweli itakuwa uonevu na mnavyojua kunung'unika si itakuwa zogo mpk sisi wateule tushindwe kuimba zetu mapambio kwa kelele zenu.
 
afadhali uamuzi huo utawasaidia, maana siku hizi mnaweka nondo na zege juu, bila kusahau tiles !
Sisi mila yetu ni ya Nabii Ibrahim !

Huna lolote mwongo wewe, Abraham unamjulia wapi wewe!

Sema unaogopa videvu vyako vya sunna pamoja na chawa na m'ba wote vitateketea na moto na kwa imani yenu jinsia huonekana kidevuni.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom