Nikasingiziwa kutembea na kabinti ka shule, kikanuka ukweni….!



Mchumbangu aliniita… “Rudi, hakuna kuwasamehe hawa, hadi mahakamani wakulipe fidia. Hawawezi kuvunjia watu heshima kwa sababu ya ubabe wao.” Mimi sikugeuka wala kurudi. Nilirudi zangu Mwananyamala.

Nasikitika kwamba huo ndio ulikuwa ni mwanzo wa mikosi kuniandama hadi uchumba wangu na Binti Picha ya Ndege
ukavunjika…………..

Story imenihuzunisha ila hapo mwisho imenihuzusha zaidi!!!
 
pole sana, ila hata hivyo inakupasa kumshukuru mungu kwa yote kwani wangeweza hata kukushushia kipigo km cha mwizi
 
ni kama nataka nikutetee hasa nikizingatia historia yako lakini mh hili ni funzo i see!na hii michezo ya watu kukubambikia kesi ilivo mingi siku hizi ?tena bora hao kweli walikuwa hawajui walichukua tu haraka haraka kun amijitu unaisaidia siku hizi kumbe linakuja kukugeuka baada ya muda fulani!
si unakumbuka ile ishu ya mdada pale muhimbili alikuwa anajifanya anaomba watu simu zao aweke line ili ampgie mume wake kuwa mtoto anatakiwa kulaza hapo ana mtoto mgongoni kisha anajifanya kusahau line yake kwako na kuhakikisha anapanda basi moja na huyo aliyemuazimisha simu(tena anakuwa na wenzie kama wawili hivi ambao hatawanotice ) akifika mbele kidogo anapiga kelele ''SIMU YANGU IMEIBIWA JAMANI'' watu haraka haraka hebu teja namba yako akitaja simu inaita kwa jamaa aliyemuazima handset!anapokeaje kichapo mpaka uje ujulikane simu ni yake na wameshamkufanyia utapeli ameshaumia,simu ashaporwa,ameshaaibika lol!

Nikikumbuka ile Sheria ya kukonyeza ilikuwa haitendi haki, mfano hilo liDada pale Muhimbili unaweza shtukia kipigo hasa kabla ya kujitetea, kuwa waangalie majina ktk Phone book

halafu Mchambuzi usikate tamaa endelea kutuelimisha nachokushauri watoto wa Pwani ni sawa na wembamba wa Reli Treni inapita na mizigo yake
 
Last edited by a moderator:
an_innocent_look.jpg

Kalikuwa ni kabinti kadogo kazuri.....!

Ilikuwa ni Jumamosi mwaka 1999, Januari. Nilikuwa natoka nyumbani Mwananyamala kwenda kibaha Picha ya Ndege mkoa wa Pwani. Hapo Picha ya Ndege ndiko kulikuwa na wakwe zangu watarajiwa. Kwa kuwa ilishapelekwa posa na mimi kutambulishwa, nilikuwa na tabia ya kwenda kusalimia na kuonana na mke wangu mtarajiwa.

Nilipofika hapo Picha ya Ndege nilielekea moja kwa moja kwa wakwe zangu ambao walikuwa hawakai mbali sana na barabarani. Nilipokaribia kufika hapo kwa wakwe zangu nilikutana na kasichana ambako umri wake ni kama miaka 12 hivi. Kalikuwa kanatafuta kitu kando ya barabara. Mimi napenda sana watoto, hasa kuwasaidia kutokana na malezi yangu ya utotoni ambapo sikubahatika kupata malezi ya mama kutokana na mama yangu kufariki na kuniacha nikiwa na umri mdogo sana.

Nilipokaona kanatafuta kitu halafu kanajifuta machozi, nikaamua kukauliza kanatafuta nini, na kwa nini kanalia. Kalisema kwa kifupi kwamba kamepoteza hereni yake moja. Nilikakatuliza kwa kukaambia kasilie kisha nikaanza kukasaidia kutafuta hiyo Hereni yake.

Wakati nikiendelea kukasaidia kutafuta hiyo hereni yake, haukupita muda, wakafika vijana wanne pale tulipokuwa. Walinivamia na kunishika kama vile nilikuwa kibaka. “Mshenzi wee, unaharibu watoto wa watu, leo utaona. Jitu zima kutembea na watoto tu.” Mmoja kati yao alisema. Wale wenzie watatu walinikunja na mmoja akamshika yule binti mkono. “Twende serikali za mitaa, halafu Polisi. Lazima mtu apigwe mvua thelathini.” alizidi kusema wakati wananikokota.

Kwa sababu ya mshangao sikuweza kusema chochote. Yule binti alikuwa akijitetea kwa kusema. “Dada mwongo wala hakunikuta naye, mwongo tu…” Sikujua ni kitu gani. Akili ilinijia tulipofikishwa kwenye ofisi za serekali ya mtaa. Niliwauliza. “Nimekosa kitu gani kustahili adha kama hii….?” Mmoja kati ya wale vijana walionibeba msobe msobe alisema. “Hujui eh, utajua ukifika mahakamani, Malaya wee…..”

Sikuelewa kitu. Wakati nashangaa, nilimwona mama mkwe wangu mtaraji na shemeji zangu watarajiwa wawili na mchumbangu nao wakiwa wamefika pale. Mama mkwe mtarajiwa aliniuliza kulikoni. Nikamjibu. “Najua basi, naona jamaa wamekuja na kunishika tu na kunileta hapa…”

Mmoja kati ya wale jamaa alisema, “Mwongo sana huyu jamaa. Huyu anatembea na haka kadogo ketu, ameshakaharibu. Bahati dada yetu leo amemshika wako pamoja njiani muda wa masomo. Dada alipomuuliza, akamshambulia dada yetu akisaidiwa na huyu mdogo wetu mapepe. Dada ameenda kuwaita wazazi waje hapa tuamue.”

Niliposikia hivyo niliogopa na kuona aibu kiasi kwamba, sikuweza hata kusema. Hasira, woga na aibu vikanifanya bubu kabisa. Hadi leo najiuliza namna akili na miili yetu inavyofanya kazi. Wale shemeji zangu watarajiwa, mama mkwe mtarajiwa na mchumbangu walikaa kando kujadili. Niliona kabisa nyuso zao zilivyo na hasira.

Wakati wakinijadili na kunitizama kwa hasira, niliomba ardhi ipasuke niingie chini. Lakini huyo dada anayedaiwa kwamba nilimshambulia alifika akiwa na mwanamke na mwanaume, ambao niliamini ni wazazi wake. Walipofika pale, yule dada aliwauliza wale vijana wababe walionibeba juu juu, “yuko wapi huyo mshenzi?” Mmoja kati ya wale vijana alisema, “si huyu hapa umeshamsahau!” Alisema akinionyesha kidole. Yule dada alisema, “siyo huyu bwana . kwani huyu mmemtoa wapi?”wale jamaa walionekana kushangaa….. “Tulimkuta akiwa pamoja na Furaha, tukajua ndiye yeye.”

Yule dada alishangaa na kusema, “Jamani siyo huyo, mmemwaibisha kaka wa watu bure. Huyu kaka wala simjui. Kaka samahani sana, naomba uwasamehe hawa kaka zangu..” Alisema yule dada. Mimi sikujibu. Nilisimama na kuanza kuondoka. Umati wa watu waliojazana pale kufuatilia sakata langu ulikuwa kimya.

Mchumbangu aliniita… “Rudi, hakuna kuwasamehe hawa, hadi mahakamani wakulipe fidia. Hawawezi kuvunjia watu heshima kwa sababu ya ubabe wao.” Mimi sikugeuka wala kurudi. Nilirudi zangu Mwananyamala.

Nasikitika kwamba huo ndio ulikuwa ni mwanzo wa mikosi kuniandama hadi uchumba wangu na Binti Picha ya Ndege ukavunjika…………..

hahahaaaaaaa pole sana mzee wangu! huu uzi ni wako na tabia hii uache, umezeeka ndugu (joking)!

Pole zake huyo mtu! mambo kamahaya huwa yapo sana hapa duaniani! coincidence huwa zinatokea sana Mtambuzi sema kitu mhimu katika maisha ni kumwomba mungu akulinde tu katika kila sekunde/nukta ya maisha yako!
kuna watu wengi walipigwa mawe kwa bahati mbaya na watu wenye hasira kali wakidhaniwa ni watuhumiwa kumbe kufananishwa tu ama kukutwa katika eneo la tukio!
Ndo maana watu hata kama mtu anajua kitu hawapendi kutoa ushahidi wowote!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom