Nikasababisha kifo cha mke wangu kwa sababu ya penzi la kahaba………….!

black-man-thinking.jpg

Bado inaniumiza sana moyoni, japo siku zimepita,. Mimi ni mwanaume mwenye miaka 46 hivi sasa, kazi yangu ni udereva wa malori yanayosafirisha mizigo nje ya nchi. Naomba niwasimulie habari yangu ili nanyi mpate kujifunza zaidi, ili msije mkafanya makosa niliyofanya mimi.

Nilioa mwaka 1996 na kufanikiwa kupata mtoto wa kwanza mwaka 1998 na katika ndoa yangu na mke wangu tulikuwa tunaishi kwenye nyumba yetu tuliyojenga kwa amani na upendo. Tukiwa na mtoto wetu huyo wa kiume ambaye tulimpenda na kumpa malezi mema, Mungu alitujalia tena na ilipofika mwaka 2001 mwishoni wakati mtoto wetu wa kwanza akiwa na miaka mitatu na nusu mke wangu alipata ujauzito mwingine na ilipofika mwaka 2002 mke wangu alipokuwa akikaribia kujifungua, alikwenda kwao Turiani Morogoro.

Baada ya mke wangu kipenzi kuondoka na mtoto wetu wa pekee kwenda kusubiri muda wa kujifungua, ndipo hapo yalipoanza matatizo ambayo yalisababishwa na mimi mwenyewe. Matatizo hayo ndiyo yaliyosababisha kifo cha mke wangu ambacho hadi leo bado kinaniumiza sana moyoni. Baada ya mke wangu kwenda kwao, nilianza uhusiano wa kimapenzi na Binti mmoja wa Kichaga, ambaye baada ya mwezi mmoja tu tangu mke wangu kuondoka nilijikuta tumezoeana na kumhamishia nyumbani kwangu kama mke halali, huku nikijua kabisa mke wangu ambaye alikwenda kujifungua huko kwao Turiani hakuwahi hata mara moja kunisaliti.

Japokuwa nilikuwa nikiishi na mwanamke mwingine ndani, lakini nilimkumbuka kumtumia pesa za matumizi mke wangu mara kwa mara, na kumjulisha kwamba sitaweza kwenda kuwatembelea kama nilivyoahidi kwa sababu nimebanwa kazini kwangu, kumbe nilikuwa nimebanwa na mwanamke na huyo ambaye naweza kumwita shetani. Lakini kadiri siku zilivyozidi kwenda nilijikuta nikiacha kabisa kumtumia pesa mke wangu na hata barua nikawa sizijibu. Lakini mke wangu mpenzi hakijali hilo, alijua niko safarini, kwani anaelewa kazi yangu ilivyo, ya kusafiri sana.

Baada ya miezi mitatu kupita tangu mke wangu aondoke, nililetewa taarifa za kujifungua kwake, lakini sikujali wala kutaka kujua hali ya mtoto na mama. Niliendelea kula raha na mwanamke huyo wa Kichaga ambaye nilimwona anayajua mapenzi kumbe mnafiki na alikuwa amenishika haswa. Ilipofika mienzi mitano baadae, ikiwa ni Julai 2002, mke wangu alirudi nyumbani, siku aliyorudi hakunikuta kwani nilikuwa nimekwenda kazini na alimkuta mwanamke huyo wa Kichaga ambaye alikuwa akiishi hapo nyumbani kama kwake. Mwanamke huyo alimpokea mke wangu kwa matusi na kejeli na kumtaka aondoke. Lakini mke wangu alimjibu kuwa angenisubiri nirudi ili ajue ukweli wote. Mke wangu alikaa nje akiwa na mtoto wetu mchanga hadi niliporudi usiku sana.

Nilimkuta nje, lakini sikushtuka kwa kweli, na wala sikutaka kujali kumwona mtoto wetu mchanga. Badala yake, bila huruma nilimfukuza na watoto wetu wawili. Mke wangu hakuamini hata kidogo. Alikuwa hajawahi kuniita kwa jina langu zaidi ya honey, dear au baba fulani, lakini siku hiyo aliniita kwa jina na kuniuliza, Hasani, kweli unanifukuza kama mbwa?

Nilimjibu kwa kumwambia, nikukumbuke wewe ni nani hasa, Mungu wangu au mzazi wangu!
Siyo siri, maneno yale aliyoyatamka marehemu mke wangu yananijia mara kwa mara kichwani na kunifanya niangushe chozi hadi leo hii

Mke wangu hakulala pale, aliondoka na watoto wake na kuomba hifadhi kwa majirani kwani tayari ilikuwa ni usiku sana, asingeweza kutoka tabata Kisukulu hadi kwa mjomba wake Kijitonyama usiku ule akiwa na watoto na mizigo. Asubuhi aliondoka na kurudi kwao Turiani. Alipofika huko kwao wazazi wake walimwambia akae atulize akili huku wao wakitafakari nini wafanye ili kutatua tatizo hilo, lakini marehemu mke wangu hakuwa na moyo wa subira kwani aliwaaga wazazi wake anaenda kupumzika chumbani. Badala ya kujipumzisha, aliamua kujiuwa na kuacha ujumbe uliosema. Nimeamua kujiuwa ili kuikimbia aibu iliyonikuta, sikutegemea kama ningefanyiwa unyama huu na mume wangu, kwani tumetoka mbali sana.

Nilipopata taarifa za msiba sikushtuka wala kujali. Nilijua ameamua mwenyewe basi na iwe hivyo, lakini baadhi ya marafiki zangu walinishauri niende kwenye msiba kwani haitakuwa vyema kutokwenda kwa sababu nilikuwa sijampa talaka, alikuwa bado ni mke wangu. Wakati tunajadili hilo mara simu ikapigwa. Alikuwa ni shemeji yangu akinitaka kuwahi nilikuwa nasubiriwa mimi ili wajue watazika wapi.

Niliamua kwenda Turiani na nilipofika kwenye msiba, nilikuwa kama mgeni japokuwa wakwe zangu na shemeji zangu walinipa heshima kama mume wa marehemu. Unajua kuna wakati hiki kitu tunachoita mapenzi kinatufanya tunakuwa kama vichaa. Yaani mtu kajiuwa kwa sababu yangu, halafu naenda macho makavuuu.! Nikikumbuka jambo lile, naona aibu sana.

Tulimaliza msiba na kujadili kuhusu watoto ambapo tulikubaliana wakae kwa bibi yao kwanza na mimi nitakapooa mke mwingine nitawachukuwa na kuwalea. Wakwe zangu walinisisitizia nisijali, kwani kifo cha mke wangu ilikuwa ni ahadi ya Mungu. Niliumia sana waliposema hivyo.

Nilirudi Dar na mambo yangu yaliendelea kuwa mazuri. Nilifanikiwa kumfungulia hawara yangu huyo wa Kichaga maduka mawili ili ayaendeshe, moja la vyakula na jingine la vipodozi.

Hata hivyo mambo yalibadilika, kwani baada ya miezi saba tangu kufa kwa mke wangu mpenzi, yule hawara yangu alianza kuniletea wanaume zake ndani ya nyumba yangu wakati ninapokuwa safarini kikazi. Majirani waliponieleza niliwadharau na kuwaona ni wagombanishi. Ilifikia kipindi nikawa sipati safari mara kwa mara, hivyo kila akiwaleta wanaume zake nyumbani ananidanganya kuwa ni ndugu zake na walikuwa wanalala pale pale kwangu.

Kumbe alichokuwa anafanya, usiku anavizia nimelala, halafu ananitoroka na kwenda chumba cha wageni alipolala huyo mwanaume wake ambaye siku hiyo yumo ndani. Nasema hivyo kwa sababu walishakuja kama watano hivi na sijui kwa nini nilikuwa sishtuki kwamba, kwao ana ndugu wa kiume tu..!

Wahenga walisema za mwizi ni arobaini. Siku hiyo kama kawaida yake aliniacha nimelala na kutoka huku nyuma nilishtuka nikajikuta niko peke yangu. Nilidhani amekwenda chooni lakini nikaona saa zinakatika. Nilitoka hadi chooni sikukuta mtu, nikaenda sebuleni, napo sikumkuta. Nilianza kuwaza, nikijiuliza wapi amekwenda usiku kama ule, tena bila kuaga.

Niliamua kwenda kwenye chumba cha mgeni ili nimwamshe tusaidiane kumtafuta dada yake. Lakini kabla sijagonga mlango, niliamua kuchungulia kupitia tundu la funguo kwa kuwa nilisikia miguno isiyo ya kawaida kama watu wanaofanjya mapenzi. Kwa kuwa taa ya chumba hicho ilikuwa inawaka, hivyo niliweza kuona kila kitu. Niliwaona wakiwa katikati ya mapenzi. Sikuamini macho yangu na nilihisi kama ninayeota tu.
Niliamua kushika kitasa na mlango ulifunguka, nikaingia na kuwagutusha. Hawara yangu alianza kulia na kuniomba msamaha. Nilimsameha na kumfukuza yule kijana. Sijui nililogwa au vipi.!

Baada ya miezi miwili ya fumanizi kupita, nilisafiri kikazi kwenda nchini Malawi. Hapo ndipo nilipompa nafasi, mwanamke huyokufanya umaaluni wake, kwani niliporudi nilikuta nyumba imefungwa na funguo kaweka kwa jirani. Nilipoulizia niliambiwa kuwa aliondoka siku tano tu baada ya mimi kusafiri. Na aliaga kwamba nilimtumia ujumbe nikimtaka anifuate. Nilishangaa sana, lakini niliondoka kwa jirani yule aliyenipa taarifa nikijua nitakuta ujumbe ndani kama kuna tatizo.

Niliingia ndani na kuangaza huku na kule bila kuona ujumbe wowote. Nilianza kukagua vitu vya ndani nikakuta kachukua vitu vyangu vingi vya thamani na pesa zote kachukua. Redio kubwa ya cd tatu pia kachukua pamoja na vito vya dhahabu ambavyo vilikuwa ni vya marehemu mke wangu. Nilibaini pia kwamba alikuwa kafilisi maduka yangu yote mawili. Nina uhakika kama angeiona hati ya nyumba, angaiuza pia.

Toka siku hiyo huwa maneno ya marehemu mke wangu yananijia kichwani. Ni yale maneno aliyoyasema siku ile usiku wakati namfukuza kama mbwa. Mpaka leo najutia kitendo changu hicho na ninahisi mimi ndiye niliyemuua mke wangu. Nilimuua bila kukusudia.
Dahhh!bonge la darasa aisee!so huko ukweni unawakumbuka na kuwapa msaada wowote?na vp ulishaoa mke mwingine?na mkeo unamuenzi vp?kama wewe ni islamic tubu kwa mola wako kisha jenga japo "madrasa"then ipe jina la mkeo kisha ikabidhi kwa waislam ili waitumie ktk kupata elimu.
 
Kwenye thread kama hii kwa sababu mbaya ni mwanaume utasikia "wanaume wabaya sana", "wanaume acheni mahawara".Ikija story ya mwanamke nao wataonekana wabaya sana.

Kumbe katika jinsia zote kuna makatili
 
Hakuna hawara ambaye ameshawahi kuleta mafanikio. Acheni wachune hadi tubaki mbavu na siku hizi ni ukimwi tu. Ni fundisho pia kwa wale tunaothamini hawara kuliko mke aliyekuwezesha kupata mali na utajiri mwingine na hela then siku mmoja unambatiza mbwa, takataka, shenzi, huna adabu, n.k But malipo hapa hapa duniani.
 
black-man-thinking.jpg

Bado inaniumiza sana moyoni, japo siku zimepita,. Mimi ni mwanaume mwenye miaka 46 hivi sasa, kazi yangu ni udereva wa malori yanayosafirisha mizigo nje ya nchi. Naomba niwasimulie habari yangu ili nanyi mpate kujifunza zaidi, ili msije mkafanya makosa niliyofanya mimi.

Nilioa mwaka 1996 na kufanikiwa kupata mtoto wa kwanza mwaka 1998 na katika ndoa yangu na mke wangu tulikuwa tunaishi kwenye nyumba yetu tuliyojenga kwa amani na upendo. Tukiwa na mtoto wetu huyo wa kiume ambaye tulimpenda na kumpa malezi mema, Mungu alitujalia tena na ilipofika mwaka 2001 mwishoni wakati mtoto wetu wa kwanza akiwa na miaka mitatu na nusu mke wangu alipata ujauzito mwingine na ilipofika mwaka 2002 mke wangu alipokuwa akikaribia kujifungua, alikwenda kwao Turiani Morogoro.

Baada ya mke wangu kipenzi kuondoka na mtoto wetu wa pekee kwenda kusubiri muda wa kujifungua, ndipo hapo yalipoanza matatizo ambayo yalisababishwa na mimi mwenyewe. Matatizo hayo ndiyo yaliyosababisha kifo cha mke wangu ambacho hadi leo bado kinaniumiza sana moyoni. Baada ya mke wangu kwenda kwao, nilianza uhusiano wa kimapenzi na Binti mmoja wa Kichaga, ambaye baada ya mwezi mmoja tu tangu mke wangu kuondoka nilijikuta tumezoeana na kumhamishia nyumbani kwangu kama mke halali, huku nikijua kabisa mke wangu ambaye alikwenda kujifungua huko kwao Turiani hakuwahi hata mara moja kunisaliti.

Japokuwa nilikuwa nikiishi na mwanamke mwingine ndani, lakini nilimkumbuka kumtumia pesa za matumizi mke wangu mara kwa mara, na kumjulisha kwamba sitaweza kwenda kuwatembelea kama nilivyoahidi kwa sababu nimebanwa kazini kwangu, kumbe nilikuwa nimebanwa na mwanamke na huyo ambaye naweza kumwita shetani. Lakini kadiri siku zilivyozidi kwenda nilijikuta nikiacha kabisa kumtumia pesa mke wangu na hata barua nikawa sizijibu. Lakini mke wangu mpenzi hakijali hilo, alijua niko safarini, kwani anaelewa kazi yangu ilivyo, ya kusafiri sana.

Baada ya miezi mitatu kupita tangu mke wangu aondoke, nililetewa taarifa za kujifungua kwake, lakini sikujali wala kutaka kujua hali ya mtoto na mama. Niliendelea kula raha na mwanamke huyo wa Kichaga ambaye nilimwona anayajua mapenzi kumbe mnafiki na alikuwa amenishika haswa. Ilipofika mienzi mitano baadae, ikiwa ni Julai 2002, mke wangu alirudi nyumbani, siku aliyorudi hakunikuta kwani nilikuwa nimekwenda kazini na alimkuta mwanamke huyo wa Kichaga ambaye alikuwa akiishi hapo nyumbani kama kwake. Mwanamke huyo alimpokea mke wangu kwa matusi na kejeli na kumtaka aondoke. Lakini mke wangu alimjibu kuwa angenisubiri nirudi ili ajue ukweli wote. Mke wangu alikaa nje akiwa na mtoto wetu mchanga hadi niliporudi usiku sana.

Nilimkuta nje, lakini sikushtuka kwa kweli, na wala sikutaka kujali kumwona mtoto wetu mchanga. Badala yake, bila huruma nilimfukuza na watoto wetu wawili. Mke wangu hakuamini hata kidogo. Alikuwa hajawahi kuniita kwa jina langu zaidi ya honey, dear au baba fulani, lakini siku hiyo aliniita kwa jina na kuniuliza, “Hasani, kweli unanifukuza kama mbwa?”

Nilimjibu kwa kumwambia, “nikukumbuke wewe ni nani hasa, Mungu wangu au mzazi wangu……!”
Siyo siri, maneno yale aliyoyatamka marehemu mke wangu yananijia mara kwa mara kichwani na kunifanya niangushe chozi hadi leo hii………

Mke wangu hakulala pale, aliondoka na watoto wake na kuomba hifadhi kwa majirani kwani tayari ilikuwa ni usiku sana, asingeweza kutoka tabata Kisukulu hadi kwa mjomba wake Kijitonyama usiku ule akiwa na watoto na mizigo. Asubuhi aliondoka na kurudi kwao Turiani. Alipofika huko kwao wazazi wake walimwambia akae atulize akili huku wao wakitafakari nini wafanye ili kutatua tatizo hilo, lakini marehemu mke wangu hakuwa na moyo wa subira kwani aliwaaga wazazi wake anaenda kupumzika chumbani. Badala ya kujipumzisha, aliamua kujiuwa na kuacha ujumbe uliosema. “Nimeamua kujiuwa ili kuikimbia aibu iliyonikuta, sikutegemea kama ningefanyiwa unyama huu na mume wangu, kwani tumetoka mbali sana.”

Nilipopata taarifa za msiba sikushtuka wala kujali. Nilijua ameamua mwenyewe basi na iwe hivyo, lakini baadhi ya marafiki zangu walinishauri niende kwenye msiba kwani haitakuwa vyema kutokwenda kwa sababu nilikuwa sijampa talaka, alikuwa bado ni mke wangu. Wakati tunajadili hilo mara simu ikapigwa. Alikuwa ni shemeji yangu akinitaka kuwahi nilikuwa nasubiriwa mimi ili wajue watazika wapi.

Niliamua kwenda Turiani na nilipofika kwenye msiba, nilikuwa kama mgeni japokuwa wakwe zangu na shemeji zangu walinipa heshima kama mume wa marehemu. Unajua kuna wakati hiki kitu tunachoita mapenzi kinatufanya tunakuwa kama vichaa. Yaani mtu kajiuwa kwa sababu yangu, halafu naenda macho makavuuu….! Nikikumbuka jambo lile, naona aibu sana.

Tulimaliza msiba na kujadili kuhusu watoto ambapo tulikubaliana wakae kwa bibi yao kwanza na mimi nitakapooa mke mwingine nitawachukuwa na kuwalea. Wakwe zangu walinisisitizia nisijali, kwani kifo cha mke wangu ilikuwa ni ahadi ya Mungu. Niliumia sana waliposema hivyo.

Nilirudi Dar na mambo yangu yaliendelea kuwa mazuri. Nilifanikiwa kumfungulia hawara yangu huyo wa Kichaga maduka mawili ili ayaendeshe, moja la vyakula na jingine la vipodozi.

Hata hivyo mambo yalibadilika, kwani baada ya miezi saba tangu kufa kwa mke wangu mpenzi, yule hawara yangu alianza kuniletea wanaume zake ndani ya nyumba yangu wakati ninapokuwa safarini kikazi. Majirani waliponieleza niliwadharau na kuwaona ni wagombanishi. Ilifikia kipindi nikawa sipati safari mara kwa mara, hivyo kila akiwaleta wanaume zake nyumbani ananidanganya kuwa ni ndugu zake na walikuwa wanalala pale pale kwangu.

Kumbe alichokuwa anafanya, usiku anavizia nimelala, halafu ananitoroka na kwenda chumba cha wageni alipolala huyo mwanaume wake ambaye siku hiyo yumo ndani. Nasema hivyo kwa sababu walishakuja kama watano hivi na sijui kwa nini nilikuwa sishtuki kwamba, kwao ana ndugu wa kiume tu…..!

Wahenga walisema za mwizi ni arobaini. Siku hiyo kama kawaida yake aliniacha nimelala na kutoka huku nyuma nilishtuka nikajikuta niko peke yangu. Nilidhani amekwenda chooni lakini nikaona saa zinakatika. Nilitoka hadi chooni sikukuta mtu, nikaenda sebuleni, napo sikumkuta. Nilianza kuwaza, nikijiuliza wapi amekwenda usiku kama ule, tena bila kuaga.

Niliamua kwenda kwenye chumba cha mgeni ili nimwamshe tusaidiane kumtafuta dada yake. Lakini kabla sijagonga mlango, niliamua kuchungulia kupitia tundu la funguo kwa kuwa nilisikia miguno isiyo ya kawaida kama watu wanaofanjya mapenzi. Kwa kuwa taa ya chumba hicho ilikuwa inawaka, hivyo niliweza kuona kila kitu. Niliwaona wakiwa katikati ya mapenzi. Sikuamini macho yangu na nilihisi kama ninayeota tu.
Niliamua kushika kitasa na mlango ulifunguka, nikaingia na kuwagutusha. Hawara yangu alianza kulia na kuniomba msamaha. Nilimsameha na kumfukuza yule kijana. Sijui nililogwa au vipi…….!

Baada ya miezi miwili ya fumanizi kupita, nilisafiri kikazi kwenda nchini Malawi. Hapo ndipo nilipompa nafasi, mwanamke huyokufanya umaaluni wake, kwani niliporudi nilikuta nyumba imefungwa na funguo kaweka kwa jirani. Nilipoulizia niliambiwa kuwa aliondoka siku tano tu baada ya mimi kusafiri. Na aliaga kwamba nilimtumia ujumbe nikimtaka anifuate. Nilishangaa sana, lakini niliondoka kwa jirani yule aliyenipa taarifa nikijua nitakuta ujumbe ndani kama kuna tatizo.

Niliingia ndani na kuangaza huku na kule bila kuona ujumbe wowote. Nilianza kukagua vitu vya ndani nikakuta kachukua vitu vyangu vingi vya thamani na pesa zote kachukua. Redio kubwa ya cd tatu pia kachukua pamoja na vito vya dhahabu ambavyo vilikuwa ni vya marehemu mke wangu. Nilibaini pia kwamba alikuwa kafilisi maduka yangu yote mawili. Nina uhakika kama angeiona hati ya nyumba, angaiuza pia.

Toka siku hiyo huwa maneno ya marehemu mke wangu yananijia kichwani. Ni yale maneno aliyoyasema siku ile usiku wakati namfukuza kama mbwa. Mpaka leo najutia kitendo changu hicho na ninahisi mimi ndiye niliyemuua mke wangu. Nilimuua bila kukusudia…………………….

Ulianza
 
Ulianza vizuri Bongo movie yako, then hapo katikati ukayakoroga. Anyway, movie yako inatoa mafunzo mazuri ktk jamii.
 
Dahhh!bonge la darasa aisee!so huko ukweni unawakumbuka na kuwapa msaada wowote?na vp ulishaoa mke mwingine?na mkeo unamuenzi vp?kama wewe ni islamic tubu kwa mola wako kisha jenga japo "madrasa"then ipe jina la mkeo kisha ikabidhi kwa waislam ili waitumie ktk kupata elimu.

Vulgar!
 
Lol Mtambuzi wewe umepitia visa na mikasa mingi! Nakumbuka kisa cha ndoa yako ya
mkeka kule Ununio!! Halafu pia ulifanikiwa kutimka na kumwacha mkeo. Au ndio ilikuwa laana/mkosi
wa kile kibinti ulichokiacha?
 
Last edited by a moderator:
Lol Mtambuzi wewe umepitia visa na mikasa mingi! Nakumbuka kisa cha ndoa yako ya
mkeka kule Ununio!! Halafu pia ulifanikiwa kutimka na kumwacha mkeo. Au ndio ilikuwa laana/mkosi
wa kile kibinti ulichokiacha?

Mkuu huu mkasa ni wa kweli lakini haunihusu mimi, kuna mdau aliusimulia na mimi nimeona ni vyema niweke hapa ili watu wapate kujifunza
 
Cha ajabu trend ni ile ile na hatujifunzi?
Mdingi, inabidi tukupeleke ukacheki na hiv, nna wasiwasi!

Mwanangu huu mkasa ni wa kweli na unamuhusu msomaji wa Gazeti la Jitambue, niliwahi kuuandika katika gazeti hilo miaka sita iliyopita.......................Wakati huo mtoa ushuhuda akiwa na miaka 40.
Mkasa huu sio miongoni mwa vile visa vyangu vya UNUNIO............LOL
 
Ntambuzi story ya leo kali hasa ulipomtumia huyo dada wa kichagga nimecheka sana, yaani anafilisi duka na kuwaingiza kaka zake ndani. Story ninpale uliposema ww ni dereva halafu ukabaki na hawara kwa nini usisafiri naye au kumpangia chumba.
hata hivyo safi sana na nakuogopa kwa uchambuzi wako wa Hekima usisahau na kesi kubwa kubwa za mahakamani wiki hili tumwagie
 
Story nzuri...lakini duuuh ndefu sana. Kwa mimi hapa ninaona mambo matatu

-Wanawake wa kichaga matapeli wa mapenzi na wafilisi

-Wanaume wa kileo hawaheshimu ndoa zao hata kama mmeanza mbali akipata mjuzi zaidi huna chako.

-Wanawake wajinga, wanataka elimu zaidi ili wajikomboe. Huyo dada wa Turiani aliyejiua kwa sababu ya aibu ni aibu gani hiyo. Hizo ndio challenges za wanawake zinazowakuta, mambo ya kuogopa jamii itawaweka katika category gani.
 
I see kumbe mtambuzi ulikuwa unaandikia jitambue?aisee ndo mana,kwanza shikamoo.umenikumbusha nikiwa Primaryto O level hilo gazeti nilikuwa nahakikisha hailinipiti nakumbuka lilikuwa linatoka jumanne cjui na cku gani baadae likapoteaga nikasikitika kweli manake huwa sinaga mazoea ya kunua magei mengine.ukweli hata hapa napenda kusoma unachoandika najifunza mengi sanna hongera kama sio babu basi baba manake jitambue nimesoma nikiwa naanza kufunguka macho.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom