Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

Kwa kweli ni kiboko, thanks Mtambuzi keep it up,
Hii imenichekesha kweli!
But kuna ukweli mwingi sana katika hili kwa tabia za vijana wanaojipatia umaarufu kwa kuwa wajanja wajanja tu na wengi wao wamekatika na ukimwi kwa kujiona vistar uchwara na kulamaba vibinti bila mipaka...

Hii ya ndoa ya mkeka naona ilikuwa fundisho kwelikweli na ingekuwa mara nyingi linafanyika hivi nadhani lingepunguza kidogo udokoaji wa vibinti.
NATA umeona eh! wengi hawajkui kama hizi simulizi zangu zina mafunzo ndani yake.
Mnaposoma mpembue pumba na mchele.

Mimi nilifanya makosa, ndio, mimi sio malaika...
Hivyo mkisoma hapa mnatakiwa mchukue mazuri na muache yale mabaya,
lakini tatizo lenu nyie mnaacha mazuri mnachukua mabaya........ sasa hiyo ni akili au matope?

pamoja daima......................LOL
 
Last edited by a moderator:
alaaaah, kumbe ndio weweeee...
Kuna dada yetu tuliwahi simuliwa kuwa aliwahi fungishwa ndoa na mpiga mziki kipindi cha ngoma ya mtoto wa mwanakwetu alafu akakimbiwa mara baada ya ndoa na kuachiwa mimba ya mapacha watatu...
Tutafutane ndugu yangu japo tukapate moja moto, moja baridi!!!
Si vbaya ukaja na mkeo wa sasa na kama una binti pia ili tuweze fahamiana vizuri zaidi

Mtaalam mkuu kumbe ni wewe uliyekuwa unashadadia siku zile wakati napigwa ndoa ya mkeka
naamini sasa utakuwa ni mtu mzima maana ulikuwa mdogooo
 
Last edited by a moderator:
Asante sana mzee Mtambuzi kwa visa vyako vizuri ambavyo vinafundisha.
The unseen is illustrated by the seen.
 
lolest kumbe ni weye ulikujaa ukaozwa na shehe jumaa pale kwa mzee Tilikele? uliozeshwa shemejiye omary Tilikele? aitwaye Mwana asha eeh! sasa siku hizi mwanaasha kesha olewa alikauwa anaishi Tandale jirani na mzee Chuche yule mmwera. Alisomeaga kozi ya recods keeping na kwasasa anafanya kazi wizara ya mali asili kama mtu wa records. Labda nikupe namba yake ya simu umpigie lakin anaish Kinyerezi. pOle sana Mtambuzi
gfsonwin ....... Duh, nitasingiziwa mengi humu leo, maana nimeona hata lafudhi yako leo imekuwa ya Kizaramo..................
 
Duh, hapo umeongea mcharazo umeniacha kabisa Muito obrigado!
Mtambuzi , hapo nimesema "huwa nakuja hapa mara kadhaa. Napenda hadithi zako. Zinaelekea ni masimulizi halisi. Je, unaandika vitabu (vya hadithi)?"

Usijali nilikuwa nachangamsha genge tu na kireno cha kuombea maji hicho! Obrigado também!
 
Last edited by a moderator:
Jijengee tabia ya kupenda kusoma.
Wa TZ tunasemwa sana kuwa tu wavivu wa kusoma.
Hebu tuikomeshe hii tabia.lol!

:biggrin1: tungekua wavivu kusoma tusingekua tuna wasomi wengi nchi hii..we unafikiri kupata degree au masters utaipata bila kua unasoma mavitabu..tatizo ni kua kitu muhimu sana kwako utakisoma hata kama ni pg100
 
Hahahaha, mkuu huna haja ya kuogopa maana ni kitambo sana sasa, sidhani hata huyo mkeo mwenyewe anakukumbuka.
Mkuu hivi unajua kuwa yule still ni mkeo halali kabisaa maana you never filed a divorce:dance:

no hawezi kuwa mke hata kama ilifungwa kisheria but kama hakumuingilia basi si mkewe.ndio maana mume akifa pasi na kumuingilia mkewe hata siku moja basi mke hapaswi kukaa uzuka.
 
no hawezi kuwa mke hata kama ilifungwa kisheria but kama hakumuingilia basi si mkewe.ndio maana mume akifa pasi na kumuingilia mkewe hata siku moja basi mke hapaswi kukaa uzuka.

amekwambia alikula usiku kucha, au kwasababu mkeka ulikuwa bado hujatandikwa
 
Hapa aje binti yako kukuokoa tu hamna namna.

images




images



7132_155077878016_572988016_2711707_3354024_n1.jpg
 
yaani nimecheka mpaka nimeishiwa point ya kuchangia.... Sipati picha ulivyotimua vumbi hadi barabara kubwa maana kuna mwendo pale, si bora sasa hivi kumerahisishwa kidogo kuna boda boda.
Da Asia kumbe unapajua Ununio eh,
Vipi ule muembe pale barabarani umekatwa?
Halafu yule mzee Shamte aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji, hivi yuko hai au keshafariki?
 
Last edited by a moderator:
Sasa ukileta kutishiana utaharibu dingi. Niambie tu nilikuwa conceived kwenye ngoma gani. Haiwezekani nikawa sina akili shule kiasi hichi!
I demand to know kabla sijaita kikao cha ukoo

Mwanangu King'asti naomba hii maneno tuimalizie hapa hapa kimya kimya...........
Nakutumia M-Pesa sasa hivi ukanunue ile Blackberry uliyokuwa ukiniulizia kila siku................

Haya mambo ukiyafikisha home kwa mama yako patachiimbika, hebu nisitiri na hii aibu baba yako................LOL
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom