Nikaishi wapi Dar hii, nikimbie hizi foleni?

Imekuwa ni adha na tabu ya kila siku kwa wakazi wa dar kutumia masaa mawili na zaidi kwenye misururu ya magari ambayo inachosha na kuharibu mipango mingi ya maendeleo,mimi nauliza hali hii mwisho wake lini au wanajamii hatuoni kero hii?

Mwanzo wa utatuzi wa tatizo ni kukubali kuwa hilo ni tatizo ndipo utatafuta njia za kuondokana nalo, lakini katika hili nimesikia kama mara mbili mkulu haoni kama hili ni tatizo bali "MAENDELEO" kwa mtazamo huo wadhani nani anaweza kufanya mkakati wa kuondoa "MAENDELEO" ya bongo??????????????

no one, ndo maana Pombe kafungwa spidi gavana maana alitaka kuondoa "MAENDELEO yetu"

Yaani bongo kukaa kwenye foleni masaa manne mpaka sita kwa siku na kufanya kazi masaa manne ndo maendeleo,
this is very funny

Bongo, I love you anyway.
 
Si mkulu ****** alisema kunaneema ya barabara za juuu tusubili tafadhali tumpe muda!
 
Imekuwa ni adha na tabu ya kila siku kwa wakazi wa dar kutumia masaa mawili na zaidi kwenye misururu ya magari ambayo inachosha na kuharibu mipango mingi ya maendeleo,mimi nauliza hali hii mwisho wake lini au wanajamii hatuoni kero hii?

Kwani mnataka kuwahi wapi yahee, no harry in tz bana. After all chadema inatufanya tushindwe kutawala nji sasa unadhani tutapata wapi pesa za kununua mabomu na risasi kisha tuweze pia kujenga barabara.
 
Kama wameshindwa barabara za chini hizo (flyover) za juu kwa juu sijui Mathalan ukiziangalia barabara mitaa ya Kariakoo centre ya biashara katika nchi za maziwa makuu ni kichekesho sidhani kama mkoloni angekuwepo sehemu hii ingekuwa na barabara za udongo zinazojaa madimbwi ya maji na zenye lami zinazotiririka maji taka Haieleweki kama jiji lina madiwa achilia mbali meya Kariakoo ni sehemu ya pekee yenye mkusanyiko mkubwa wa watu lakini angalia pale shule ya uhuru wameshindwa kuweka mifuniko ya mitaro ya maji machafu na maji yenye uvundo yametuama Giza likiingia ndio balaa taa zote haziwaki mitaro iko wazi nisikilizie patashika walalahoi tunagombania daladala kwenye giza wakutumbukia kwenye majitaka wakuibiwa wakuumizwa waheshimiwa madiwani maofisini ni business as usual bajeti ni chai na magazeti kweli tutafika?
 
Imekuwa ni adha na tabu ya kila siku kwa wakazi wa dar kutumia masaa mawili na zaidi kwenye misururu ya magari ambayo inachosha na kuharibu mipango mingi ya maendeleo,mimi nauliza hali hii mwisho wake lini au wanajamii hatuoni kero hii?

Wakati wa kampeni last year mkuu wa nchi aliahidi kujenga metro train/subway hapo Dar ili kupunguza foleni. Nahisi ujenzi umeshaanza. Wazo zuri, kwani hakuna mtu atapanda daladala
 
Hali ni mbaya sana, traffic wana tija yoyote ni bora taa ziongoze magari kuliko hawa jamaa. Jambo la kushangaza hata katika masaa ambayo hakuna magari mengi wao hutaka kuongoza magari. Mwanzoni sikujua skuwa kuongoza gari kwenye taa ni deal , mpaka siku moja nilikuwa ndani ya gari ya jamaa mmoja tukiwa maeneo ya fire alimuuliza alimpigia simu jamaa yake akajua nani yupo magomeni, akampigia simu gari zilifutwa wacha baada ya dk tano tukawa tumevuka. Akaniambia hivyo ndiyo vijana wengi wa mjini wanafanya, malipo wakikutana kwenye viwanja- bia, nyama choma, hata hela ya vocha.

Hali kwa sasa ni mbaya sana Shekilango rd, Sokota- Buguruni na katika ya mji sorry ''jiji''
 
Mnazungumzia barabara na magari.. Vipi kuhusu hizo building permit zinazotolewa kwa maeneo ya mjini kila uchao, ile Posta ya Karimjee, Gymkhana mixa Ikulu ni mwendo wa nyavu za kijani.., vipi kuhusu serikali kuhamishIa maSTK yake Dodoma maana nayo yanachangia foleni, vipi kuhusu bandari kuu kuhamishiwa Bagamoyo ili upakuzi wa shehena ufanyikie huko badala ya ile mi-Semi trailer kujaza Barabara ya Mandela? Hata zijengwe flyovers, sijui treni za subway, tatizo litarudi baada ya muda mfupi.
 
Jamani msiwaone traffics kuwa hawafai kuvuta magari. Ngoja watoke kwa masaa sita tu. chamoto mtakiona. Hizo taa hazitoshi. kuna barabar zingine magari yanapita mawili mawili lakini ghafla yanakuwa moja. mf.Morogoro rd kuingia mjini pale inapokutana na Bibi Titi. bila trafics kusaidia, sielewi. Lakini ni sisi hawa hawa tunaoupinga mpango wa bomoa bomoa kupisha upanuzi wa barabara.
 
kikubwa mimi nadhani kwanza kuanzishwa kwa miji mipya ambapo shughuli zote muhimu zinapelekwa huko mathalani ukiweka mji mpya kibaha au chalinze na shughuli ambazo zilikuwa zinafanywa maeneo ya katikati ya jiji sidhani kama tatizo la foleni litakuwa tuchukue mfano wa nigeria walivyohamisha shughuli nyingikutoka loagos na kuanzisha abuja hadithi ya foleni ambayo walikuwa nayo ya mpaka kupanga namba za magari kutembea zimekwisha.

Pili zile STK zingehamishwa katika huo mji wanaotuambia makamo makuu ya chama na serikali DODOMA nadhani hakuna mfanyakazi wa taasisi yoyote kutoka mkoani kuja dar es salaam sababu wote wangeishia DODOMA na kurejea maeneo yao kazi, lakini hii hadithi ya kuhamia DODOMA naona watapita watawala wote na hadithi itabaki hiyo hiyo ya kuhamia huko, sababu tu siasa imetawala kila nyanja hata zile za msingi nazo zimemezwa na siasa. KWA HILI HATUFIKI POPOTE TUNABAKI NA LIFOLENI LETU LA KILA SIKU AMBALO KILA KUKICHA LINAZIDI KUWA TU
 
Vilevile suala na kufufua zile njia ambazo ziko mitaani kwa kuziwekea kama si kiwango cha lamio basi hata changalawe ingetosha kupunguza msongamano wote huo, kidogo walijitahidi mitaa ya magomeni kufufua ile barabara ya mwembechai mpaka mikumi kwa kiasi fulani inaeza kuwa imesaidia, hivyo hivyo wangefanya hata zile za kijitonyama na kwingineko kuzifufua na kuweza kupunguza foleni katika barabara kuu za jijini dar es salaam.
 
Bei ya Lita Moja ya Diezel na Petrol kwa Gari ambazo si za ABIRIA IWE SHILINGI 12,000 KUANZIA TAREHE 01 JUNI 2011.
 
Fikiria vizuri ndugu yangu kabla ya kupost topic,wewe mwenyewe unajua kuwa mafuta yakipanda kufikia hiyo bei uliyoitaja vitu vyote hapa nchini vitapanda kuliko maelezo.
 
Hayo ni mawazo yako,lakini wadau mkumbuke kua miaka ya nyuma Magari Ndogo (za starehe) hazikuruhusiwa kutembea siku za Wikiendi na maisha yalikua yanabana sana.
 
kinachopendekezwa hapa ni kupandisha bei ya mafuta hayo kwa gari zisizo za abiria. Hii maana yake ni kuwa bei ya mafuta haitabadilika ila kama unatumia gari ambalo kazi yake si kubeba abiria wala mizigo itabidi ulipe shilingi 12,000 tu kwa kila lita ya mafuta utakayo nunua na kwa daladala na taxi wao wataendelea kununua mafuta kwa bei ya sasa. Hii itasaidia kupunguza sana magari binafsi na ya serikali katika barabara zetu hivyo kumaliza tatizo la foleni hapa nchini. Pia itatoa fursa nzuri ya kuwa na usafiri bora na wa uhakika wa umma.
 
Hayo ni mawazo yako,lakini wadau mkumbuke kua miaka ya nyuma Magari Ndogo (za starehe) hazikuruhusiwa kutembea siku za Wikiendi na maisha yalikua yanabana sana.

utatumia usafiri wa umma kama wengine tufanyavyo kwa sasa.
 
fikiria vizuri ndugu yangu kabla ya kupost topic,wewe mwenyewe unajua kuwa mafuta yakipanda kufikia hiyo bei uliyoitaja vitu vyote hapa nchini vitapanda kuliko maelezo.

sijasema mafuta yapande bali ni kwa gari zisizo za abiria tu. Hivyo kama una taxi au daladala bado utaendelea kununua mafuta kwa bei ya sasa.
 
Back
Top Bottom