nikadhani tanga nilikwenda kikazi kumbe ni mvutano wa kuifata damu yangu

Story inafundisha sana ila matukio hayana uhalisia; mfano; simu unazozungumzia hapa sidhani kweli kama zilikuepo miaka kumi na tano iliopita, pili, unasema mliendelea kuwasiliana; je katika kipindi hicho hakuwahi kukujulisha kuwa ana ujauzito? Maana ujauzito ni ndani ya mwezi tu ishajulikana na ndani ya mwezi huu mlikua mkiwasiliana bado! Tatu, alianza lini form one hadi akafika form six? Ukichanganya muda uliokutana nae kisha kumpeleka shule bado haijakaa njema ila hadithi ni nzuri sana, ondoa mambo ya cmu
 
Umeicopy and paste kutoka wapi? Ila duh km ni kweli imeniumiza sana

Huwa sio mtu wa kukomenti kwenye jukwaa hili.
Hii hadithi nimewahi kuisoma katika gazeti la JITAMBUE (nadhani halichapwi tena) la marehemu Munga Tehenan, miaka ya mwanzoni mwa 2000s. Imerekebishwa kidogo sana, lakini kisa ni kile kile
 
habari zenu magreat thinkers wa JF .mbarikiwe saaana kwa kuwa nyie ni sehemu ya maisha yangu maana humu jamvini japo kuna vimbwanga na vituko vya kila leo lakini kwa upande mwingine nimejifunza mengi saaana.shukurani kwa wana JF popote mlipo.
kisa hiki jamani waungwana nimekichomoa mahali yaani copy and paste so wazeee wa madongo msiniumize sura nimetoa taarifa mapemaaa

NANUKUU
mimi ni mfanyakazi wa serikalini katika wizara fulani . kwa kweli bado sijaoa(nina mtoto) ila ndo hvo kimjinimjini ukikutana na mrembo mnamalizana maisha yanaendelea...hyo imekuwa ndo staili ya maisha yangu.Siku 1 nikasafiri kikazi kwenda bagamoyo kwenye semina kama ya wiki mbili hivi.......aaah kwani hata huko bagamoyo nilipitwa basii...kama unaamini hvo ni sawa na kuamini gavana wetu mstaafu balali alikufaga wakati.........mmm tuyaache hayo..ishu ni kuwa nikapata mwanamke hukohuko kwenye semina tukajivinjari sana ,tukala tundi kwa sana na ful KUPIGA PICHA za mikao ya kimahaba na zingine za kawaida.......ila wakati tunakula tundi muda fulani nakumbuka yule mwanamke aliniambia yupo kwenye sku za hatari so aidha nifanye kwa kinga au kama ninaweza yale mambo yetu yale niyamwagie nje.mmmh kinga skutaka kwa kuwa nilisha onja ile kitu yetu ilomzubaisha baba yetu adam na akaingia mkenge matokeo yake ndo haya dunia leo ipo kama ilivo pia kumwaga nje kwa kweli nahisi mtu akiniuliza mimi ni mwanaume..? naweza nikababaika kujibu kwa kutokuwa na uakika lakini akiniuliza unaweza kupiiiz nje? nina uhakika wa 900% kuwa SIWEZI...basi mzee mzima nikaserebuka nae mwanamke wa watu kavukavu.
baada ya wiki kadhaa semina ikaisha (yeye alikuja bagamoyo pia kikazi kutoka kigoma na mimi kutoka dar).kila mtu akarudi katika mkoa wake na ahadi nyiiiingi za kuendeleza mapenzi.kama ujuavyo ndugu yangu mapenzi ya mbali kwa BAADHI yetu hatuyawezi tukaanza kupotezeana mpaka tukawa hatutaftani na huyo mwanamke tena. na nafkiri akabadili namba ya simu sjui maana nikawa simpati.nikamsahau maisha yakaendelea...
ikapita kama miaka 15 hivi bado nikiwa mfanyakazi wa serikalini nikapangiwa kwenda mkoani tanga kikazi kama wiki 3. nikaenda huko tanga ila nikafkia kwa jamaa yangu ili niokoe ela ya hoteli nifanyie mambo mengine.jamaa yangu akanikaribisha vizuri alikuwa akiishi yeye na mkewe na kisichana cha kazi kwa umri kama miaka 14 au 15 kwa kadirio langu
kwa kweli walikuwa wanakatesa sana haka kabinti mana walikuwa wanakatumikisha kama mbwa,bila hata mshahara, kalikuwa hakalali mpaka kamemaliza kazi zoote so kakawa kanalala muda mbovu kama saa 7 au 8 ucku kila siku kwenye stoo ya vyakula au jikoni na hapo jikon penyewe hata mbwa hastahili kulala sasa skuambiii binadamu.kalikuwa kamechakaa kwa mateso ya mule ndani.kila nkikaangalia nakaonea huruma lakini sina la kufanya naona naingilia maisha ya watu.ilikuwa ni kawaida kupitisha hata sku mbili hakajala kwa kuwa wao mara nying walikuwa watu wa kula makazini kwao au hotelini.sku 1wakakaambia kawapikie wali kwa kuwa watakula nyambani kakapika wali kakaunguuza ukawa hauliki na ilitokea hvo kwa kuwa kalisinzia wakati kanapika(nafkir kwa sababu ya uchovu wa kulala masaa machache).weeeee ilikuwa kosaa kalipewa kibano mpaka kakavunjwa mkono. kalilia saana mpaka usku wa manane na chumba changu kilikuwa na hapo anapolala yeye.nikaamka nkamwambia mwenyej wangu aamke tukapeleke hospitali kwa kuwa wamekajeruhi katoto ka watu. si jamaa wala mkewe hakuna aliyejali wala hawakukubali kukapeleka kupata matibabu.niliskia uchungu sana.kesho yake nikawa kuna kazi namalizia pale ndani ili niwah kazini nikiwa nimekaa sebuleni( wenyej wangu walikuwa pia wametoka kwenye mihangaiko yao ya kila siku) nikakaita ..kakaja kwa upole nikaanza kukahoji jina,mahali kalipotokea na kaliletwa na nani hapo..."hapa nililetwa na dada mmoja jirani yetu alinichukua kutoka kwetu kigoma kuja nifanye kazi ,mama yangu alifariki kwa hyo nikawa sina mtu wa kunilea ndo nimekuja huku tanga kutafta maisha" kakanijibu hivyo ....niliskia huruma sana ila nikashangaa kidogo maana kalikuwa kananiangalia kwa jicho kama la kunichunguza au kuniangalia kwa makini.nikaakauliza sababu ya kuniangalia hvo kwa makini kakajibu ... unajua anko nilikuwa cjapata nafasi ya kukuangalia kwa karibu na kwa umakini ila nahisi umefanana na mtu alipiga picha na mama kabla hajafariki.........ah nikaona haka kamechanganyikiwa na kile kipigo na maumivu ya mkono.....akilini mwangu nikachukue nikapeleke hospitali hata kama wenyej wangu watachukia potelea pote....nikakaambia haya kavae twende hospitali na uje na hyo picha unayosema kakaenda kuvaa fresh kakarudi kameshka picha mkononi...haa haaaaaa mwana JF hebu kisia nilichoona kwenye hyo picha....kisia basiii ili stori inogee..aisee nilihisi kuishiwa nguvu nikakaa chini kama nataka kupoteza fahamu...pale kwenye picha nipo mimi na yule mwanamke tuliekutana nae bagamoyooo miaka 15 ilopita.yani ni mimi kabsaaaa na yule mwanamke.na nikakumbuka tulivokuwa tunapga picha nilimwambia picha zile kesho yake mpiga picha akileta ampe yeye huyo mwanamke kwa kuwa mimi si mtu wa kutunza mapicha picha(nafkiri wanaume tulio wengi hatuna desturi hii kwa mawazo yangu).kumbe mwanamke wa watu nilimpa ujauzito akajifungua akalea kiumbe na akachukua picha na kumwambia mwanae " huyu kwenye picha ndo baba yako ila yupo dar sku ya sku huenda MUNGU akawakutahisha".baadae kabisa mwanamke wa watu akafariki mwanae akaja tanga kufata mateso na siyo kazi......nilitoka kwenda hospitali na huyo mwanangu kisha nikapitia kazini kuomba ruhusa kwa maana akili yangu haikuwa sawa mda huo....aisee naomba nikatishe hiii stori ila kwa kifupi ili kujiridhisha baada ya miezi kadhaa nilienda kwa wataalamu wa afya kupima vinasaba(DNA) na kweli nikakuta ni mwanangu halali(of coz hata kama ingekuwa syo mwanangu ngeish nae kwa kuwa ile coincidence ilinitisha sana) kwa sasa naish nae na anasoma kidato cha sita na nina mpango wa kusaka mke mwema atakaenilielea mwanangu kwa upendo kwa kuwa nikikumbuka niliokuwa nayaona sitaki yamrudie........MWISHO WA KUNUKUU

jamani nafkiri hilo ni angalizo kuwa kwa wale wazee wa kupga kazi za nje bila kinga kila mnapoenda semina mjaribu kufatilia usikute mna watoto wenu wanahenyeka na dunia wakijua hawana baba kumbe nyie mpo na VISHTOBE vingine au wake zenu mnakula raha kumbe damu zenu zinateseka.....asanteni wana jf kwa usikivu na poleni kwa urefu wa kisa...cheers

Hata km inaweza kuwa ni ya hadithi ya kutunga, still inagusa sana kwa walio na mioyo ya kibinadamu tu!
 
Nashkuru kaka eli kwa mchango.Kama nlivoongezea kwenye coment baadh ya vi2 nimeongezea tu kunogesha mambo.Niwie radh kwa kutokuwa na mpangilio mzur wa kiuandish. Pia idimi nashkuru kwa kunikumbusha.Ni gazet la jitambue ndo nilisomaga humo ila matukio meng nimeongezea kujaribu ivutie.Thanx for your comments
 
Inasikitisha, heb just imagine km ungekatongoza hlf kakubali ndo uje ungundue ni mwanao ungefanyaje?
 
Hii stori imegusa saaana na kunitoa machozi! Ni kama sinema za kihindi vile lakini kuna ukweli ndani yake.
Haya wanaume! Tafakari ; Chukua hatua.
 
Duh, pole san ndugu yangu. sasa jambo lilobaki uoe ila sidhani kama utapata mwanamke wa kukutunzia huyo mwanao. Nakushauri kama bado atakuwa anasoma wakati ambao wewe unaoa basi ni vema umpeleke boarding ili. coz akija kukaa hapo na huyo mke wako mpya itakuwa ni mateso kwake na hata kwako hutakua na amani.
 
Hadithi hii inatufundisha kwamba ni muhimu kutumia kinga imagine ungekuwa na wife home pangechimbikaje?
 
Hii story unaweza tengenezea movie ni fundisho kwa wale chapa ilale na kusahau kabisa...
 
Bora umekiri mapema kwamba hii stori umeitoa mahali maana nakumbuka sana kuisoma.La sivyo ningekudondoshea madongo makali.Stori hii ni fundisho kwa wanaume wanaopanda mbegu na kuishia.Hatari hasahasa ni pale unapokutana na dogodogo unaivamia kumbe ni binti yako kabisaaa
 
Story nzuri na inafikirsha sana, ngoja nirudi Lindi
 
Nashkuru kaka eli kwa mchango.Kama nlivoongezea kwenye coment baadh ya vi2 nimeongezea tu kunogesha mambo.Niwie radh kwa kutokuwa na mpangilio mzur wa kiuandish. Pia idimi nashkuru kwa kunikumbusha.Ni gazet la jitambue ndo nilisomaga humo ila matukio meng nimeongezea kujaribu ivutie.Thanx for your comments

Ni mahubiri tosha kwa jumapili hii ntakapokua naongoza ibada na pia ni mhadhara mzuri sana nitakapokua pale kwenye viwanja vya Bakhersa Manzese!!!
 
Watoto wengi wa mtaani na wanaoomba barabarani ni matokeo ya wazembe kama wewe...ila nakusamehe kwa sababu hukujua kuwa umezaa.

Ila sasa ndiyo haujaoa mpaka leo? Una hatari. Na usiendekeze ngono zembe tena.

Mwisho, pole sana.


Kweli kabisa,watoto wa mitaani wana wazazi wao,tena utakuta wengine wanaendesha magari makubwa na watoto wao,wanaomba hata mia 200 ili wafute kioo cha gari!!
Inatisha!!Tuangalie wapi tumekosea turekebishe mambo!!
 
Hii stori ni nzuri, mimi binafsi sipendi kuacha mtoto sehem yeyote ile hata kwa gharama zozote zile lazima nimfuatilie na kumtunza hata kama sita oa mama yake.
 
Back
Top Bottom