Nijuzeni tofauti ya maneno haya!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,649
Yananichanganya sana haya maneno hasa juu ya tofauti iliyopo kati yake. Naomba tu mniaeleze ili nami nijue tofauti yake. Maneno yenyewe ni haya:

Umalaya, uasherati, uzinzi na ukahaba. Nini tofauti ya haya maneno? Nijuzeni tafadhali!

Nawasubiria!
 
Wajuzi wakuchambua maneno kama karanga nishawaita wanakuja subiri kiduchu manake wana funga zawadi za Valentine.
 
Uzinzi-Ni kitendo cha mtu aliye kwenye ndoa kufanya ngono nje ya ndoa na mtu yeyote yule.

Uasherati-Ni kitendo cha mtu ambaye hajaoa au kuolewa kufanya ngono na mtu yeyote yule.

Ukahaba-Ni kufanya ngono kwa minajili ya kujipatia kipato(kujiuza).

Umalaya-Ni mazoea sugu ya kuwa na mahusiano ya kingono na mtu mmoja au zaidi .Uasherati na uzinzi vikiwa sugu ndio umalaya wenyewe.

Disclaimer:
Hizi sio tafsiri za kwenye kamusi.
 
Pamoja na maelezo mazuri ya Ambitious, maneno haya yanakaribiana sana, kiasi kwamba unapolitumia moja, linaweza kujihusisha na jengine.
Hizi hapa maana kwa mujbu wa Kamusi la Kiswahili Sanifu la TUKI:
Uasherati: Tabia ya kupenda kuzini, dondoo, kiranga.
Ukahaba: Mwenendo wa m'me au m'ke wa kushiriki uasherati kama biashara yake; umalaya, uteleleshi, uzinifu, uzinzi
Umalaya: Ukahaba
Uzinzi: Hali ya ukware, uasherati, uzinifu, dondoo.
**************************************
Kama kidokezo tu, hii inanikumbusha jambo moja. Waeskimo wana majina mengi kwa ajili ya barafu, kwa sababu ndio waliyonayo nyingi. Vilevile Waswahili tuna majina mengi ya matumizi ya maji (kukoga, kunawa,kutawaza, kufua, kuchanyata, kujisafisha....), pengine kwa sababu tunayo mengi.

Kuhusu maneno haya: uasherati, ukahaba, umalaya na uzinzi, kama utaaangalia yote yanahusiana na ngono isiyo halali. Jee hakuna uwezekano wa kuwa tuko kama walivyo Waeskimo na barafu, sisi na ngono isiyo halali?
 
Ngamia, nguruwe na punda vyote haramu. Usishangae mmoja anakula ngamia na kuita halali lakini nguruwe anamwta haramu. Uzinzi,ukahaba, uasherati vyote haramu. Atendaye moja kati ya hayo hatouona ufalme wa mbinguni.
 
Uzinzi-Ni kitendo cha mtu aliye kwenye ndoa kufanya ngono nje ya ndoa na mtu yeyote yule.

Uasherati-Ni kitendo cha mtu ambaye hajaoa au kuolewa kufanya ngono na mtu yeyote yule.

Ukahaba-Ni kufanya ngono kwa minajili ya kujipatia kipato(kujiuza).

Umalaya-Ni mazoea sugu ya kuwa na mahusiano ya kingono na mtu mmoja au zaidi .Uasherati na uzinzi vikiwa sugu ndio umalaya wenyewe.

Disclaimer:
Hizi sio tafsiri za kwenye kamusi.
hapo kwenye umalaya ingekaa vizuri ikisomeka kama ifuatavyo:

Umalaya-Ni mazoea sugu ya kuwa na mahusiano ya kingono na mtu mmoja au zaidi ambae si mwenzi wa ndoa.
kwa maana wanaume wa kiislamu wanaruhusiwa kuoa wake wanne(4) na hivyo mahusiano hayo hayawezi kuitwa umalaya!

 
Back
Top Bottom