Niishi vipi na huyu jamaa yangu

goodhearted

JF-Expert Member
Feb 15, 2015
944
1,110
Bila shaka mu bukheri wa afya,

Kuna jamaa yangu ameniomba sana niishi nae ktka nyumba ya kupanga ambayo anaishi yeye na mkewe na mtoto wao mmoja.

Kisa kiko hivi, hiyo nyumba alikuwa anaishi na mwenye nyumba ambae amefariki kama wiki mbili hivi. kwa kuwa nyumba ni kubwa jamaa yangu kanimba nichukue na mimi chumba hapo kisa yeye anaogopa kuishi hapo peke yake na et nkikataa hata yeye atahama.

kwa kuwa hata mimi nilikuwa ninaharakati za kutafuta nyumba nyingine ya kupanga nikaona nimkubalie kwani nyumba yenyewe ina kiwango kizuri.

Tatizo lililonifanya niombe ushauri ni hivi, toka nihamie hapa tumekuwa tukishea chakula means nakontribute then shemeji anapika chakula cha wote. Lakini jana shemeji kanifuta usiku wakati nakula cha chakula cha usiku akaniuliza swali ambalo nilishindwa kumjibu papo kwa hapo, kaniuliza hivi "Shemu tutaendelea kula pamoja au utaanza kujipikia chakula chako?" kwa kweli nilimwambia anipe muda nitafakari! Huku nikiwaza amefikiria nini kuniuliza swali kama lile!!

Kujipikia sio tabu lakini sasa kwa jinsi tunavyoishi na huyu jamaa yangu cjui atanielewaje. Maana tunashea sebule na kila kitu tulichokikuta hapo, mi naingia chumbani kwangu nae anaingia kwake.

ushauri wenu wadau. Ingekuwa ww ndo mimi ungechukua uamuzi gani katika hili!!?
 
mkuu ningekuwa na wazo nisingeomba ushauri, ndo maana nimeomba ushauri ili niufanyie kazi!!
 
Kuishi na watu nyumba moja halafu kila mtu awe anajipikia ni hali nisiyoipenda kabisa.

Inaleta awkwardness flani hivi.

Siwezi kabisa kuishi namna hiyo.

Ningekuwa wewe ningehama. Kwanza wala hata nisingehamia.

Ningetafuta sehemu yangu niishi mwenyewe kwa uhuru zaidi.

Mambo ya kuchangia chakula na watu mwishowe huwa yanaishia pabaya tu.

Hapo umeulizwa hivyo usikute wenzio wameshakusoma na kukuona labda unakula mno kuliko unavyochangia.

Kwa hiyo jiongeze mwenyewe hapo.
 
Mkuu kama umeulizwa hivyo ina maana shemeji yako anatamani uanze kujipikia. Ebu jipikie tu. kwani shida iko wapi?
 
Bila shaka mu bukheri wa afya,

Kuna jamaa yangu ameniomba sana niishi nae ktka nyumba ya kupanga ambayo anaishi yeye na mkewe na mtoto wao mmoja.

Kisa kiko hivi, hiyo nyumba alikuwa anaishi na mwenye nyumba ambae amefariki kama wiki mbili hivi. kwa kuwa nyumba ni kubwa jamaa yangu kanimba nichukue na mimi chumba hapo kisa yeye anaogopa kuishi hapo peke yake na et nkikataa hata yeye atahama.

kwa kuwa hata mimi nilikuwa ninaharakati za kutafuta nyumba nyingine ya kupanga nikaona nimkubalie kwani nyumba yenyewe ina kiwango kizuri.

Tatizo lililonifanya niombe ushauri ni hivi, toka nihamie hapa tumekuwa tukishea chakula means nakontribute then shemeji anapika chakula cha wote. Lakini jana shemeji kanifuta usiku wakati nakula cha chakula cha usiku akaniuliza swali ambalo nilishindwa kumjibu papo kwa hapo, kaniuliza hivi "Shemu tutaendelea kula pamoja au utaanza kujipikia chakula chako?" kwa kweli nilimwambia anipe muda nitafakari! Huku nikiwaza amefikiria nini kuniuliza swali kama lile!!

Kujipikia sio tabu lakini sasa kwa jinsi tunavyoishi na huyu jamaa yangu cjui atanielewaje. Maana tunashea sebule na kila kitu tulichokikuta hapo, mi naingia chumbani kwangu nae anaingia kwake.

ushauri wenu wadau. Ingekuwa ww ndo mimi ungechukua uamuzi gani katika hili!!?
Nikionacho
1. Kwa sasa una wasiwasi na namna jamaa yako atakavyokuelewa, lakini kumbuka jamaa yako si yeye anayepika
2. Mwanamke kukuuliza swali hilo maana yake hapendi akupikie hivyo usipoelewa anaweza akakusingizia lolote kwa mumewe
3. Kwa kawaida huwa tunakula chakula alichopika mwanamke, kama huyo mwanamke ni mama yako, mkeo, dada yako au ndugu yako, mama mama ntilie. Kwa mazingira yenu na kushea kwenu sebure mwabamke hapendi...
4. Achana na kushea sebure na mtu mwenye familia. Kama na wewe umeowa sawa lakini kwmq bachela ipo siku mwanamke atataka umgegede halafu ukikataa akusemee kwa jamaa..
5. Mwambie jamaa yako kuwa unahama lakini useme hayo baada ya kutafuta pa kuishi. Na uhame kweli.
6. Kwa kushea sebure, maana yake siku ukichelewa kurudi, eidha jamaa yako, mkewe au mtoto wao akufungulie mlango. Hilo litageuka kuwa kero baada ya muda
7. Kwa kushea sebure, mana yake kila mgeni anayeingia na kutoka Chumbani kwako anaonana na yeyote wa familia ya jamaa yako... hapo maana yake hata demu wako.. sasa nke wa jamaa kama anakutaka Utaishi kwa shida sana

HAMA HIYO NYUMBA KABLA HAYAJAKUWA MAKUBWA, KAMA NI JAMAA YAKO UTAKUJA KUMTEMBELEA UKITOKEA KWAKO KWINGINE
 
dah! hii imekuwa shughuri
 
Dawa ni kuhama mkuu, uhuru mzuri sana. Si unaona mambo ya kubanana yamesababisha ukuta tarehe 1.
 
Hapo hama mana shemeji anajua unapenda mteremko na vilevile huwezi jua jamaa yako akiwa pekee yake na mkewe huwa anamwambia kitu gani kuhusu wewe mana mnaweza kuwa mnacheka vizuri lakini jamaa akiwa pembeni anakung'ong'a.Vilevile anakulemaza ili uchelewe kuoa maana utakuwa unaona kama haina haja hata uhuru wa kumleta mpenzi wako ndani unapungua
 
Sio ujipikie naa wewe lin utaoa upikiwe na wa kwako yeye kachoka kupikia waume wawili
 
Mkuu kama umeulizwa hivyo ina maana shemeji yako anatamani uanze kujipikia. Ebu jipikie tu. kwani shida iko wapi?
Ishu wanashare sebule moja, wakati wakula jamaa atatoka nje au kujifungia chumbani?
 
dah! hii imekuwa shughuri
Usikute jamaa yako anamwwmbia mkewe kuwa..
1. Anakulisha
2. Huchangii chochote
3. Pango anakulipia... maana mtu kushea sebure anasheaga na watoto wake au ndugu anaomtembelea
4. Anakusaidia kwa muda kushi hapo utaondoka hivi karibuni
 
Tafuta girlfriend uishi nae awe anafanya yale ambayo ni ya muhimu kama kupika,kusafisha nyumba hasa choo na bafu na pia kuact kama stabilizer maana nasense trouble huko mbeleni. Leo umeulizwa kama utaendelea kula nao au utajipikia,kesho utaulizwa kwanini huwa husaidii kufagia uwanja, keshokutwa itakuwa bafu na choo halafu baadae utaambiwa mbona huoi, au unamtaka shemejio au shemeji yako atasema unamtongoza.
Ukishindwa,nakushauri uhame tu. Rafiki yako kuna uwezekano alikuwa na nia njema na akadhani na mkewe pia ana mtazamo huo,lakini kitendo cha huyo mwanamke kuanza kukujia na maswali yasiyo na tafsiri rahisi iliyo wazi,ni dalili kuwa kuna swala limeanza kutokota.
 
Dah!!! Jamani saa zingine mtu ufikrie kabla ya kufanya jambo...yani umekosea sanaaa kuhamia nyumba moja na rafiki yako...Siku zote kama unataka urafiki wenu uishe, bas kaeni nyumba moja. Ingekuwa ninyi wote ni mabachela wala hakuna shida..lakini mmoja kaoa? Au wote mmeoa?? Urafiki lazima uvunjike....
Yani kitakacho kusaidia ili urafiki na heshima iendelee ni wewe kuhama hapo...tumia akili yako yote kama kweli unataka urafiki uendelee....tatizo halitakua kwenye chakula tu...
 
Ulifanya kosa kubwa sana kuhamia kwa huyo rafiki yako.Wewe ni mtu mzima sasa unatakiwa uishi maisha yako independent uwe na vitu vyako vya ndani na sio kitumia vitu vya marehemu. Ukikaa hapo nakuhakikishia akili yako itadumaa,pia mtaanza kukwazana na huyo jamaa au mke wake,nakushauri kwa nia njema kuwa wewe kama mtoto wa kiume unahitaji kujijenga,unahitaji kuwa na privacy yako,unahitaji kuwa na samani mbalimbali na kwa kumalizia unatakiwa kujitegemea. Mambo ya kukaa wanaume wawili kubebana yameshapitwa na wakati. Grow up brother.
Hama. kuanzia hii wiki tafuta ustaarabu wa kuhama fasta. yaani isiwe ombi na hauhitaji kuburgain na rafki yako. Wewe ni mtu mzima una haki ya kufanya maamuzi sahihi wakati sahihi ambao ndio huu.
 
Back
Top Bottom