Nigeria court order Shell BP to hand over Land..

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,772
8,958
Mahakama ya Nigeria imepitisha hukumu kwa kampuni ya Shell BP kuwarudishia wananchi wake ardhi ambayo ndiyo yenye mradi mkubwa wa uchimbaji mafuta!...Hii ilikuwa moja ya ahadi ya rais wao mpya ambaye aliiweka wakati akipigania kiti cha Urais!..nilimsikia akihojiwa ktk kipindi cha Hard Talk - BBC.

Source:- Morningstar - Dow Jones & Company, Inc.: Nigeria Court Tells Shell To Hand Over Land Near Bonny Terminal

Jamani kumbe inawezekana!...Sasa nadhani Barricks na wawekeshaji wengine wote ktk madini inabiudi twende kwa mtindo wa Nigeria..Shell wameahidi kukata rufaa..
 
Safi sana hii labda hii itawafumbua macho 'mafisadi' walio madarakani waache kuwanyang'anya ardhi yao Watanzania na kuwakabidhi 'wachukuaji' toka nchi za kigeni.
 
Mahakama ya Nigeria imepitisha hukumu kwa kampuni ya Shell BP kuwarudishia wananchi wake ardhi ambayo ndiyo yenye mradi mkubwa wa uchimbaji mafuta!...Hii ilikuwa moja ya ahadi ya rais wao mpya ambaye aliiweka wakati akipigania kiti cha Urais!..nilimsikia akihojiwa ktk kipindi cha Hard Talk - BBC.

Source:- Morningstar - Dow Jones & Company, Inc.: Nigeria Court Tells Shell To Hand Over Land Near Bonny Terminal

Jamani kumbe inawezekana!...Sasa nadhani Barricks na wawekeshaji wengine wote ktk madini inabiudi twende kwa mtindo wa Nigeria..Shell wameahidi kukata rufaa..

Actually kamishna wa madini Dk. Kafumu ametoa mapendekezo mengi ya kufanya something similar; lakini mafisadi walioko juu; ambao ndiyo hasa wenye uwezo wa kufanya haya mambo yafanyike wameamua kukaa kimya .... nadhani bado tuna safari ndefu lakini Insha'Allah tutafika.
 
Mahakama ya Nigeria imepitisha hukumu....

...Hii ilikuwa moja ya ahadi ya rais wao mpya ambaye aliiweka wakati akipigania kiti cha Urais!..nilimsikia akihojiwa ktk kipindi cha Hard Talk - BBC.

Mkandara, hiki kitu haijakaa vizuri. Unless, Rais nae alikuwa kwenye jopo la majaji.

Katika nchi zenye demokrasi za separation of powers, Rais ana nguvu za aina mbili, moja ni kusukuma legislation bungeni, mbili ni kutumia Maagizo ya Wakuu (executive order) -ambayo haipitii kwenye mahakama.

Kama huyu Rais wa Nigeria aliisukuma Mahakama iamue anavyotaka yeye kama alivyoahidi kwenye kampeni mimi simtaki Rais kama huyo, hata kama atakuwa anajaribu kuzuia ufisadi wa mali za nchi.

Mtu anaetetea haki zangu kwa kukanyaga misingi ya demokrasia na sheria za nchi kuna siku atanirudia na kunigeuka mimi mwenyewe!!

Naomba uanishe vizuri ulichomsikia Rais wa Nigeria anakisema. Nitashangaa kama atakuwa aliahidi kwamba majaji wa mahakama zake wataamuru Shell warudishe ardhi, ikiwa ni ahadi ya kampeni.
 
Back
Top Bottom