Nifanyeje?

Ennie

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
7,137
4,122
Nina miaka 7 kwenye ndoa na watoto wa2. Niligundua mume wangu ana cheat akakiri na kuomba radhi. Mwezi sasa sitaki anisemeshe kwa mapenzi au hata aniguse nakumbuka kilichotokea na naona na huko alikuwa anafanya hayo hayo. Naumia badala ya ku enjoy. Nifanyeje niweze ku respond normal kama zamani?
 
Pole sana kwa yaliokukuta bi mkubwa Ennie lakini kama uliamua kusamehe then do that with a pure heart.i'm sure kama unampenda then ukijaribu tu kumpa nafasi nyingine automaticaly utasahau yaliyotokea na kurudisha uhusiano mzuri na mwenzi wako
 
mwambie akupe muda u heal,asikubughudhi kama yuko understanding atakuelewa tu unahitaji muda wa kupona:sick:
 
Hujamsamehe mama,ulimwambia tu umemsamehe.....

Naona una mume mwenye busara kwamba amekiri kosa,ushauri wangu usizidi kumuumiza hata kama bado inakuuma usiache hadi kumsemesha.......unless humhitaji tena,zungumzeni tu....na pengine utajua mengi na kwanini hilo lilitokea na ufanyeje lisitokee......we do not marry angels from heaven my dear.......but living necessary.........

Pole sana,kweli inaumiza hasa kama umekuwa ukitimiza wajibu wako na hukustahili hilo,ila usimpe shetani nafasi ya kumpa mumeo matamanio ya kwenda nje tena........Muombe pia Mungu akusaidie kusamehe, kikweli kwa uwezo wa kibinadamu ni ngumu.....
 
Mama si lazima kukaa na mtu usiempenda!!nadhani kwa sasa huna mapenzi nae hata kidogo kwa hiyo jitahidi uachane nae na ukaanze maisha kwengine!!
jamani hamuoni wenzenu wazungu!!!???kula unachopenda mama!!Muachie mitoto yake aisome!!
 
Haaaahhh hebu soma hii "NIMEKUSAHAU LAKIN SITASAHAU" Hii ndo unatumikia dada. Yaani watu wanajua kutesa wenzao.
Pole mpenzi ndoa ndo zilivyo dear vumilia utaacha wangapi my dear?? Wote wako hivyo hivyo!! Ila wengine huwa na heshima unaweza usimshitukie hata kidogo
 
Tatizo la mume kwenda nje kwa wanawake ni sawa na kujikwaa cku iz. Lisikufikirishe sn. Wenzio unaowaona wana raha kiukwel wanawastiri tu waume zao.
 
Nina miaka 7 kwenye ndoa na watoto wa2. Niligundua mume wangu ana cheat akakiri na kuomba radhi. Mwezi sasa sitaki anisemeshe kwa mapenzi au hata aniguse nakumbuka kilichotokea na naona na huko alikuwa anafanya hayo hayo. Naumia badala ya ku enjoy. Nifanyeje niweze ku respond normal kama zamani?

Amekukosea kwa kiwango cha juu kabisa. Amekuomba samahani na wewe nadhani umeikubali samahani yake. Kama ndiyo hivyo basi msamehe na kufanya hivyo kutakuwezesha hata wewe kuweza tena kuenjoy tena kama ilivyokuwa zamani kila mnapokuwa pamoja...kusamehe ni therapy ya aina yake ambayo pia humsaidia aliyekosewa kuweza kumove on na maisha yake ya kila siku. Kumbuka kosa moja haliachi mke.
 
Mama si lazima kukaa na mtu usiempenda!!nadhani kwa sasa huna mapenzi nae hata kidogo kwa hiyo jitahidi uachane nae na ukaanze maisha kwengine!!
jamani hamuoni wenzenu wazungu!!!???kula unachopenda mama!!Muachie mitoto yake aisome!!

Utaacha wangapi?hao wema wasio cheat wako wapi???kama unawajua muagizie aende direct.....usijitahidi kuachana na mtu ambaye ulimpenda sana,kumbuka kwa nini ulikubali yeye akuoe na si wengine.....na kamwe hata yakikushinda usimuachie mumeo watoto wako watalelewa na hao waliokutoa kwa ndoa,hata upate shida gani labda hujiwezi......wanao wape first priority.....

Nakushauri kama ukiachana nae uwe unatarajia kwenda kuishi mwenyewe maisha yako yote na wanao,otherwise you are likely kumpata ananye-cheat na wala msamaha haombi...... sijui bana labda hao wadhungu anaosema dada......:sad:
 
ulisema hayo kumridhisha lakini ndani ya moyo wako bado hukutoa msamaha wa kweli,nakushauri msamehe usifikiri utakutana na malaika tena bora huyo inawezekana alikuwa anafanya kiistarabu wengine mmh hayo ndio masha yetu ya sasa usifukunyue sana yalijificha kabatini utapata heart attach uache watoto wanateseka.
 
Mke mwema huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. Nakanuni ya kusamehe ni kusamehe na kusahau, inaonekana hujasamehe ndo maana inakusumbua. Samehe na usahau jamani ili u enjoy na mumeo usimkaribishe shetani, si unajua mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe? Ijenge nyumba yako usiibomoe pia samehe ili na mungu akusamehe unayo koseaga.
 
Nina miaka 7 kwenye ndoa na watoto wa2. Niligundua mume wangu ana cheat akakiri na kuomba radhi. Mwezi sasa sitaki anisemeshe kwa mapenzi au hata aniguse nakumbuka kilichotokea na naona na huko alikuwa anafanya hayo hayo. Naumia badala ya ku enjoy. Nifanyeje niweze ku respond normal kama zamani?
NINA IMANI KABISA PAMOJA NA KWAMBA AMEKIRI NA KUOMBA MSAMAHA, INAWEZEKANA PIA ALIKUA KWENYE INITIAL STAGE YA CHEATING, KUFANYA HIVYO UNAVYOFIKILIA, ILIKUA BADO AJAVUNJA AMRI ILE YA SIX, HIVYO NAOMBA UWE NA AMANI NA APETAIT IWE PALEPALE DADA YANGU, SASA KUENDELEA KUMNYIMA NAONA NI HATARI ZAIDI.....:rain:
 
Mama si lazima kukaa na mtu usiempenda!!nadhani kwa sasa huna mapenzi nae hata kidogo kwa hiyo jitahidi uachane nae na ukaanze maisha kwengine!
jamani hamuoni wenzenu wazungu!?kula unachopenda mama!!Muachie mitoto yake aisome!!

Uliyosema yanaweza kua choice moja wapo akishindwa kumsamehe kabisa!Ila swala la kumuachia watoto sio busara hata kidogo...kisa cha kuwapa watoto adhabu ya kubaki na baba tu au kuja kulelewa na mama wa kambo?Hawakushiriki kuvunja ndoa yao
 
ahsanteni friends kwa ushauri mzuri. Nitajitahidi kusamehe completely na kusahau kwani bado nampenda sana. Pengine kweli anahitaji nafasi nyingine. Ikibidi kuachana siwezi kumuachia watoto.
 
ahsanteni friends kwa ushauri mzuri. Nitajitahidi kusamehe completely na kusahau kwani bado nampenda sana. Pengine kweli anahitaji nafasi nyingine. Ikibidi kuachana siwezi kumuachia watoto.

AMEN Ennie,all the best dear.....:coffee:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom