Nelly Huyu
Member
- Mar 31, 2011
- 35
- 3
Asalam aleykum wadau wote, mimi ni kijana mwezenu na nimeoa miaka 3 iliyopita na nimejaliwa Mtoto mmoja wa Kike wa kuzaa..kilichonisukuma kuandika mada hii ni kupata ushauri kutoka kwenu kwani licha ya kuwa na mke na mtoto pia nina ishi na mtoto wangu wa kufikia. The thing is, wakati nafunga ndoa Mke wangu alikuwa tayari ana mtoto wa miaka mitano (5) nashkuru Mungu kwani hakunificha kuhusu swala hilo I mean ni jambo ambalo nilikuwa nalifahamu tangu tulipokuwa wachumba tu, na wakati tunapanga mipango ya kuishi pamoja alisema katu mtoto hawezi kuwa kikwazo kwetu kwani mtoto yule ni wa babu yaani baba yake mzazi na atakuwa anaishi kwa babu kwani kwani baba wa mtoto si msaada..by then dogo alikuwa anaishi kwa babu..nilitaka kujua kama mtoto atakuwa kikwazo kwasababu baba wa mzazi yupo hai japo si msaada kwa mwanaye licha yakuwa anajimudu kiuchumi lakini alisema hataki kuona mtoto wake analelewa na baba mwingine. Niliamini alichoniambia, tukafunga ndoa na mwaka wa kwanza ulienda vizuri mpaka pale aliponiambia kuwa anata akae na mtoto kwasababu akiangalia afya yake si nzuri kutokana na kukosa uangalizi..nilimkubalia kwani alisema kuwa litakuwa jambo la muda mfupi..sasa nimekuwa nikiishi naye kama mwanangu since then, sina tatizo kuhusu hilo kwani kimsingi yule ni mwanangu..kinachonikwaza ni yeye mke wangu anavyomdekeza mtoto kwani kila anapokosea na ukijaribu kumuongoza kwa kumsema au ikiwezekana kumchapa basi ataingilia kati na kukujengea mazingira kuwa unamchukia mwanaye, hii inapunguza heshima toka kwa mtoto kwenda kwa baba haswa ukichukulia kuwa anamiaka tisa, sasa swali langu ni kwamba kama namchukia mtoto kwanini hataki kumpeleka kwa baba yake..isitoshe jamaa yaani baba wa mtoto anadharau sana, zakujishow off kuwa anauwezo wa kumlea mwanae ila mke hataki, je ni haki kulea mtoto wa mwanaume mwenzio ambaye yupo hai na anadharau....ni vyema kwa mke wangu kunipandikizia chuki kwa mtoto? Nifanyeje?